Wacha wananchi waumie, lakini ongezeko la umeme ni palepale-waziri ngeleja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wacha wananchi waumie, lakini ongezeko la umeme ni palepale-waziri ngeleja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chamajani, Dec 24, 2010.

 1. c

  chamajani JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kauli za kejeli zinazidi kutolewa na viongozi wetu baada ya Waziri ngeleja kuueleza umma kupitia TBC kuwa hata kama wananchi wataumia kiasi gani, gharama za umeme lazma zipande. Akazidi kueleza kuwa gharama zenyewe ni kati ya sh. 9-11 na.., so hakuna haja ya watanzania kuhamaki na kuchukua hatua za nguvu umma kwa ongezeko hilo.
  Lakini ni kweli 18.5% ni asilimia ndogo kwa wanaojua mathematics?
   
 2. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata kama itakuwa ndogo vyovyote vile, bado ni nyongeza ya mzigo wa mateso kwa watanzania wengi. Hasa ikizingatiwa kuwa kwao hakuna nyongeza yoyote ya kipato, zaidi ni kuzidi kuporomoka kila uchao. YANA MWISHO!!!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,605
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Wacha wafanye madudu kwani hayo ni mambo yatakayowapiga na kuwagaraza 2015,yaani hizo ni kura za ccm zinahama tu ,we wacha tu !
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 3,653
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  Sio swala la kushangaza yaani sioni jipya. Serikali inajulikana kuwa haipo kwa manufaa ya wananchi ila kwa kundi la watu wachache. Kwa ujumla nchi imetekwa. Tunazungwa kwa uchaguzi kisha kikundi kile kile kinarudi kwa kasi, hari na nguvu zaidi. So hayo ndio matunda ya kutoelewa kwa wengi wetu.
   
 5. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 492
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Unajua jana wakati namsikiliza Ngeleja na jamaa toka Tanesco na Uwura, nilikumbuka hadith ya mke mmoja wa mfalme huko ufaransa. Wananchi walipokuwa na hali ngumu ya maisha waliamua kufanya mgomo na mke wa mfalme akauliza hawa wanapiga kelele za nini?? Mumewe ambaye ni mfalme akamjibu mkewe kuwa wanalalamika kuwa bei ya mkate imepanda hivyo wanataka ishuke. Mkewe akamwambia si wale keki???. Ndio hii kesi ya jana, Ngeleja anasema bei yenyewe iliyopanda ni sh 9 hadi 28 tu, anaziona ni ndogo saana. Sh 28 kwa uniti moja, kama nina nunua unit 250 kwa mwezi ni sawa na ongezeko la sh 7000/= kwa mwezi. Je hiki kiwango ni kidogo??? yeye anasema ni 28 tu?? Jamani kwa kuwa yeye halipi bei ya umeme ndio maana haoni kama ni ghali. Ngeleja analipiwa kila kitu na serikali, Anausafiri wa umma, mafuta ya serikali, nyumba ya serikali, maji na umeme serikali inalipa mshahara wake ni wa masuala yake binafsi hivyo haoni uzito wa kupanda kwa bei ya umeme. Ni kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
   
Loading...