Wacha mimi niongeze tuzo yangu ya Kocha bora wa Mashindano ya Kagame | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wacha mimi niongeze tuzo yangu ya Kocha bora wa Mashindano ya Kagame

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Jul 30, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa mtazamo wangu:-
  View attachment 60315
  Tom Saintfiet Mkuu wa benchi la ufundi la Yanga: Kocha bora wa mashindano.

  Vigezo vya ku'support hili:-
  1. Ni kocha pekee kati ya makocha wote waliokuwa na team shiriki aliyekaa na team yake kwa muda mfupi (siku 11 tu)kabla ya kuanza kwa mashindano,hii ilimpa tabu hata kwenye kutafuta kikosi cha kwanza (1st Eleven) ikumbukwe alivyopanga kikosi cha kwanza kwenye mechi ya kwanza ya ufunguzi ambayo team yake ilipoteza sivyo ambavyo alipanga mechi zilizofuata,kikosi cha kwanza amekipatia humohumo kwenye mashindano.
  2. Ni kocha pekee aliyekuwa akiwatumia wachezaji ambao hakuhusika kuwasajili completely, hii ilimwongezea ugumu katika upangaji wa kikosi cha ushindi na wote tumeshuhudia jinsi alivyokuwa akibadilibadili nafasi za Wachezaji katika kuhakikisha ana'utilize uwezo wa mchezaji husika katika kutafuta ushindi wa team nzima.
  3. Pamoja na team yake kuandamwa na majeruhi kwa baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza mfano Juma Abdul,Nizar Khalfani na Yaw Berko ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika kuhakikisha anaziba nafasi zao pasipo kuiathiri team,tumeona akiwachezesha nafasi tofauti baadhi ya wachezaji ambao siyo sisi washabiki tu ambao hatukutarajia kuwaona wakizicheza hata wao wenyewe walikuwa hawakuwahi kufikiria kama wanaweza kutumika katika nafasi hizo kiufasaha, rejea left wing aliyokuwa akipiga Mwasyika na baadaye David Luhende,rejeeni pia namba 7 aliyopiga Taita mechi na APR bila kusahau namba 2 aliyopiga Mwasyika (ambaye ni left footer) siku ya fainali na kuwadhibiti akina Kipre Tchetche utafikiri Nsajigwa enzi zake...kila mtu atakubaliana nami kuwa katika hili "Mt Tom" amedhihirisha yeye ni gwiji katika masuala ya ufundishaji soka,na bila shaka anafaa kuigwa kwa maendeleo ya soka la nchi hii mfano Mkuu wa benchi la ufundi la watani zetu angekuwa na akili kama ya "Mt Tom ange'test kumchezesha mbele Shomari Kapombe ambaye alionekana yuko very aggressive katika mechi yao dhidi ya Azam badala ya Kapi (am sorry to say this) lake Sunzu,pengine wasingepatwa na fedheha ya kiasi kile....kila kitu kinawezekana aisee.
  4. Ni Kocha pekee aliyeonekana (kabla hata mashindano hayajaanza) kujua anachokifanya vizuri.
  Wakati Yanga ilipopeleka team B kwenye mashindano ya ujirani mwema yaliyoandaliwa na Chama cha soka cha Zanzibar,wengi waliongea maneno ya ajabuajabu wapo waliosema Yanga imeogopa fedheha ambayo wangeipata tena endapo wangekutana na Simba,kumbe Tom Saintfiet Mkuu wa benchi la ufundi la team hiyo alishaona mashindano yale yasingekuwa na faida yeyote kwa team yake kama ilivyodhihirika kwa Azam,Simba na Mafunzo ambazo zilishiriki mashindano yale na zilipokuja kwenye Kagame zikaambulia patupu.
  Kila mtu amekubali anachokifanya na sasa hv baadhi ya wakuu wa mabenchi mengine ya ufundi katika team nyingine wameshatangaza kuzitoa team zao kwenye mashindano yaliyochomoza tena ghafla kama Urafiki Cup.
  5. Ni Kocha aliye na courage ya kuwaponda wachezaji wake pale wanapoonekana kucheza vibaya au kinyume na maelekezo yake na kuiathiri team,ndo maana amewatangazia mapema kuwa wachezaji wote wanaojiooona hawana viwango vya kuichezea Yanga au wana tabia ya kutojituma kwa maendeleo ya team waanze kutafuta team mapema kabla hajapeleka majina yao kwa Viongozi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa kwaajili ya kuchwa au kupelekwa kwa mkopo team nyingine,amesisitiza ni afadhali abaki na wachezaji wachache wenye machango kwa team badala ya kundi kubwa la mizigo.Kocha huyu ameonyesha kutokuwa na mpango wa kule mizigo kabisa, tayari gazeti 1 la leo limeandika habari za Jerry Tegete kujaribu kuulizia nafasi kwa watani zetu.....well done..mizigo sampuli ya Sunzu kwao iwe ni Msimbazi siyo Jangwani.
  6. Ni kocha pekee aliyeonekana kuheshimu team zote,hata aliponukuliwa wakati team yake ikijiandaa kucheza na Vibonde Wau Salaam hakuonekana kuwadharau,aliheshimu kila team shiriki tofauti na makocha wa Attletico,APR na Vita walioonekana kuponda baadhi ya team shiriki pasipo kujua kuwa team zao zingekuja kutolewa na hizohizo team walizoziponda.
  7. Pale team yake iliposhindwa kufanya kile alichokitegemea/kilichotegemewa na wapenzi wake alikuwa anatoa sababu za kitaalamu badala ya sababu za kujitetea kama alivyofanya Mkuu wa benchi la ufundi la Watani zetu,APR,Vita na wengineo, rejeeni statement yake baada ya mechi ya nusu fainali na APR.
  8......

  Wacha nijenge Taifa kwanza lkn zipo sababu nyingi zinazomweka Tom Saintfiet Kocha wa Mabingwa wa kusakata kabumbu ukanda mzima wa Africa ya Mashariki na kati katika nafasi ya Kocha bora wa mashindano ya Kagame Cup yaliyomalizika hivi karibuni,hizo 7 ni baadhi tu ya factors hizo.
  Big up Uncle Tom,big up Yanga hakika kuna kila dalili la Taifa kunufaika na utaalamu wako endapo watakuwa wanau'apply.
   
Loading...