Wacha Maneno weka viwanda

Negan The Dead

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
340
994
Salam Wote
Nimebahatika kusikiliza hotuba ya mh rais wakati akiwaapisha watu wake.Nimesikitishwa na hotuba yake yenye kuonyesha hasira na chuki dhidi ya vyombo vya habari.

Kwa ufupi sana nilitegemea angesema mpaka sasa tuna viwanda vingapi na vimebaki vingapi na vimeongeza ajira kiasi gani.Angenipa takwimu ya ukuaji wa viwanda na kujibu hoja kua kwa nini wizara fulani fulani budget yake ni zaidi ya 200% wakati wizara nyingine ni chini ya 15%.

Mtukufu Magufuli ameonyesha hasira za wazi wazi kwenye mitandao ya kijamii,Alishasema kua hafanyii kazi taarifa za mitandao sababu ni udaku, kwa nini leo?Kama amefanya uchunguzi na kugundua kua taarifa za mitandao ni uzushi mf taarifa ya Kinana na Mwakyembe je ile ya Bashite ameishia wapi?

Hivi kweli rais alitaka aweke headline kwa kushtua watu bandarini?Hayo mambo ya mishtuko watu wameshayachoka kwa sababu hayana tija.Kuna wafanyakazi wangapi kutoka bandari hati kwa rais?Kama hawamsaidii kwa nini asiwatumbue kunusuru pesa za mavuja jasho?

Rais alishasema asipangiwe mambo yake japo sisi wananchi ndio tumemwajiri.Aendelee kufanya mambo yake kana kwamba nchi hii ni yake.Atambue kwamba mitandao ya kijamii sio adui wa rais.Mitandao ya kijamii ndio ilifanya watu wanjue Daudi na vyeti vyake alivyoazima au kuiba.

Kwa ufupi mh rais, tuambie mpaka sasa umetengeneza viwanda vingapi?umeajiri watu kiasi gani na hizo ajira unatangaza wapi.
Vile vile utuambie rais,Nape alifanya kosa gani hadi atolewe bastola hadharani.
Mwisho nikutakie kazi njema na ukumbuke kua "Huu mchezo hauhitaji hasira"
 
Back
Top Bottom