Habari wana MMU,
leo nina maswali kidogo kuhusu hili kabila la waburunge. Kwanza kabisa naomba ieleweke kuwa ninauliza maswali haya kwa sababu sikuwahi kujua kuwa kuna kabila linakwenda kwa jina hili hadi hapo jana.
Ni kwamba katika pitapita zangu nimekutana na binti mmoja mrembo sana, sasa katika kuzungumza ikafikia mahali akanijulisha kuwa yeye ni Mburunge na kwa mujibu wa maelezo yake hii kabila inapatikana Manyara. Sasa basi ninaomba kwa wale wenye habari kuhusu hii kabila watusaidie mwanga zaidi hapa hususani katika eneo la mahusiano.
Maswali yangu ni kama ifuatavyo:
Najua kuna watu mtasema muulize mwenyewe. Kifupi ni kwamba nimeshamuuliza lakini nimeona niulize na humu maana huenda kuna watu wana habari muhimu na sahihi kuhusu waburunge kuliko hata huyu msichana.
Haya jamani uwanja ni wenu.

- Je, tamaduni zao zikoje kwenye suala la mahusiano?
- Je, wanafanya tohara kwa wanawake? Na pia wana kitu chochote kinachofanana na jando?
- Najua kila mmoja ana tabia zake lakini kuna zile tabia za jumla zinazotokana na tamaduni na malezi yanayopatikana katika kabila fulani. Naomba kujua ni zipi tabia za kabila hili hususani katika mahusiano.