Wabunifu wa mitaa na barabara zetu kwenye majiji mnaziwazia boulevards za kisasa?

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,288
17,730
Mimi siyo mtembezi Sana kwenye majiji na miji yetu ya Tanzania.

Katika utembeaji wangu sehemu chache nilizotembelea sijaona mitaa yenye barabara pana kwenye mitaa ambazo zimepambwa na majengo mazuri na safu za miti mizuri pembezoni au kati kati ya barabara kwa mtindo ule unaoitwa boulevard kama mitaa ya majiji ya wenzetu huko nchi za magharibi.

Nimeleta mada hii ili wahusika waliangalie suala hili kwenye majiji mapya kama Dodoma, au sehemu kama Kigamboni maana majiji ya Dar (kwa ujumla wake), Mwanza, Mbeya na Arusha tumeshachelewa kuna ujenzi holela.

Jambo hili lingewezekana kwa jiji la Dar wakati wa upanuzi na maboresho ya barabara za Ally Hassan Mwinyi na Sam Mnujoma, hasa hapo Samnujoma ingekuwa rahisi zaidi kuweka mashariti ya majengo ya pembezoni yawe ya namna gani kwa vile bado kuna maeneo wazi.

Usanifu wa majengo kama Hostel za Magufuli za UDSM pembezoni mwa barabara ile inayobeba sura ya jiji ni matumizi mabaya ya ardhi, ule ni ubunifu wa hali ya chini mno.

Kwanini hatuwazi kuandaa mitaa na barabara za miaka 100 au zaidi ijayo?

Mipango miji na watu wa ardhi mnakwama wapi?

Nitawashangaa kama Dodoma na Kigamboni Dar nako tutakosa boulevards.

Najua tumejaribu jaribu kidogo kubuni boulevard kule Morogogoro road toka mjini hadi Ubungo mataa, Sam Mnujoma road, Nyerere road na Ally Hassan Mwinyi lakini bado majengo ya pembeni yametuangusha sana.

Sijui kwanini upanuzi wa Morogoro road toka Kimara hadi Kibaha haujaiga viwango vya ubunifu wa toka City centre hadi Ubungo mataa??!!

Tunabuni ovyo kisha akija raisi mpya tunavunja barabara hiyo hiyo na kujenga upya, ilitakiwa tuongezee kitu kwenye ubunifu bora wa zamani.
Extension iwe maboresho siyo kuvunja barabara au vituo vya mwendokasi.

Morogoro Road ilivunjwa wakati wa Mkapa miaka ya 2000 ika vunjwa tena wakati wa Kikwete kujenga BRT, kisha pale Shekilango hadi Kibo Ubungo pakavunjwa wakati wa Magufuli kujenga flyover, Kituo cha BRT kikavunjwa pale Ubungo Maji/TANESCO.

Hali ni hiyo hiyo Ally Hassan Mwinyi na Kawawa Road vunja vunja tu ndani ya miaka michache. Kilwa road nako imevunjwa na kujengwa ndani ya muda mfupi. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, kodi zetu.

Unaweza kuona mfano wa boulevard kwa kutafuta google andika boulevard kisha ujionee mwenyewe.
 
Changamoto yetu kubwa kabisa ni kukosa dira na muelekeo wa pamoja. kwa wale walioko madarakani.Kila mmoja anakuja na jambo lake analolithamini.

Tunapaswa kua na dira na uelekeo ambao kila kiongozi wa nchi ni lazima aufate unaolenga miaka 100 mbele bila kujali itikadi ya chama tawala. Mipango ya mrefu inawezasaidia.

Wenzetu wanafanya kitu chao leo wakiwa wamelenga miaka 200 mbele. Sisi tuna mipango ya miaka mitano mitano inabidi tujitafakari kwenu eneo la mipango tuondoe ubinafsi kabisa.
 
Watoto wanakaa chin matako yakiwaka moto mashulen...panadol hakuna mahospitalin ..unaongelea boulevards?

Hapo hapo malaria inawatafuna watu na ukimwi..

Mkuu niaje
 
Watoto wanakaa chin matako yakiwaka moto mashulen...panadol hakuna mahospitalin ..unaongelea boulevards?

Hapo hapo malaria inawatafuna watu na ukimwi..

Mkuu niaje
Mipango tu na ubunifu.
Gharama tunazotumia kujenga ovyo ni kubwa sana, ukijumlisha na jenga bomoa jenga tena.

Si lazima ukamilishe kama ilivyo kwenye plan yote, unaweka kitu kwa awamu kisha unaongezea pembeni au kati kilichoachwa mwanzo kutoka kwenye plan original.
 
Mipango yetu ni ya zima moto, kila mtu anakuja na mhemko wake wenyewe ndio tutaona tuna viongozi!
 
Back
Top Bottom