Wabunge19 Viti Maalum wanaojitambulisha kwa jina la CHADEMA washitakiwe

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Uongozi wa CHADEMA.

Ni miezi 8 sasa tangu Wabunge wa Viti Maalum 19 kuwa Wabunge kwa mwavuli wa CHADEMA. Lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa CHADEMA.

Naomba mtafute wanasheria wazuri wafungue mashitaka kwaniaba ya taasisi ya CHADEMA, sio tatizo wakishirikishwa Wananchi kuchangia kwa ajili ya kuendesha kesi.

Ikiwa zilichangwa zile Million 300 kuwalipia kesi mlizobambiwa. Hili ni dogo sana. Hasira iliyoko ndani na nje ya Bunge ni kubwa sana.

LINDA CHAMA
 
Kafanye kazi kijana na achana na hawa wabunge 19! CHADEDMA kama chama kikuu kinalilia maridhiano ya kitaifa na chama tawala na serikali yake kinashindwa nini kuridhiana na wabunge hawa kwa kuwasamehe? Kwani wabunge hawa wameua mtu? Chadema iache kushupaza shingo, iache mambo yaendelee!
 
DJ makengeza ndiyo kiongozi wa hii mishen hakuna mtu ataenda kushitaki hapo unafikiri kwanini rufaa haikai na unafikiri wameshindwa kweli kuwatoa? tumia akili planned mission
 
Jamani,ukisema hao dada zetu washitakiwe mtakuwa mnawaonea
Bunge lote kikatiba ni batili OVER
 
CHADEMA mchezo wote wanaufahamu kama ingekuwa kweli ni maamuzi ya chama hao wabunge covid 19 wangeshashtakiwa na hatua zingeshachukuliwa, hiyo ishu viongozi wa chadema wanafahamu rejea maneno ya mzee Halima alisema wanabaraka za mwenyekiti na akamdhihaki katibu mkuu Mnyika kwa kumuita bwana mdogo.
 
CHADEMA wafungue mashtaka ya nini, wao walishamaliza kwa KUWAFUKUZA Uanachama, sio wanachama wao watawashtaki kama nani? Ni hao wabunge ndio wamekata rufaa na kwa kimya hiki cha Chadema ni kuwa rufaa yao haikufanikiwa! kama ni kushtaki basi ni sisi wananchi tunaowalipa mshahara a posho kule bungeni!
 
Nawe kwa busara zako unaamini kwa dhati kuwa Chadema - iliyosheheni wanasheria kadhaa wabobevu - hawajui kuhusu hilo unaloshauri? Confidence ya akina Halima Mdee wanaipata ndani ya Chadema na sio kwa NEC wala Ndugai.
Kwahiyo unachotaka kusema hapa ni kwamba hao COVID 19 wanalindwa na kina MBOWE?
 
Acheni wivu, cha muhimu kazi iendelee tupate maendeleo🤣🤸🐒
20210615_215028.jpg
 
Chadema wafungue mashtaka ya nini, wao walishamaliza kwa KUWAFUKUZA Uanachama, sio wanachama wao watawashtaki kama nani? Ni hao wabunge ndio wamekata rufaa na kwa kimya hiki cha Chadema ni kuwa rufaa yao haikufanikiwa! kama ni kushtaki basi ni sisi wananchi tunaowalipa mshahara a posho kule bungeni!
wanaweza kuwashtaki sababu ni wabunge hewa kwa mwamvuli wa CHADEMA
 
Kafanye kazi kijana na achana na hawa wabunge 19! Chadema kama chama kikuu kinalilia maridhiano ya kitaifa na chama tawala na serikali yake kinashindwa nini kuridhiana na wabunge hawa kwa kuwasamehe? Kwani wabunge hawa wameua mtu? Chadema iache kushupaza shingo, iache mambo yaendelee!
Haiwezekani kushirikiana na msaliti
 
Chadema mchezo wote wanaufahamu kama ingekuwa kweli ni maamuzi ya chama hao wabunge covid 19 wangeshashtakiwa na hatua zingeshachukuliwa,hiyo ishu viongozi wa chadema wanafahamu rejea maneno ya mzee Halima alisema wanabaraka za mwenyekiti na akamdhihaki katibu mkuu Mnyika kwa kumuita bwana mdogo.
tena alimuita katibu bwana mdogo aliyekwenda chadema na kandambili yaani aisee halkafu jamaa hajawahi kuijibu hiyo wana cofidence kubwa tu
 
Back
Top Bottom