Wabunge

Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
52
Mheshimiwa Philip Marmo katangaza kuwa wabunge wote ambo ni Wakurugenzi kwenye Mashirika ya Umma wataondolewa ili Kupisha accountability yao bungeni.
Ya kweli haya ama ni kiini macho kama kawaida?
 
actions are better than words ... lets wait for action and see if it doenst take 100yrs to accomplish
 
actions are better than words ... lets wait for action and see if it doenst take 100yrs to accomplish

Actually it will take the whole millenium I hope hat wenye mashule na mubizinezi wataambiwa wavunge kidogo.
 
tunashangaa na vijineno vya wabunge wetu? ni wazuri wa kufikiria, lakini utendaji wao ni mtupu. itachukua miaka kadhaa hadi hilo kufikiriwa kuchukuliwa hatua seuze kutekelezwa
 
itachukua miaka??they wil keep it pending til 2010 ili wakija tena kuomba kula....wakwambie u see we are on the process kutimiza hili we have jus started giv us 5 mo yrs tumalize!!!
 
Haya maneno sijui kama wataweza kuyatengeleza watakuwa wanatuzuga tu bila shaka kama kawaida yao ngoje tusubili natuone jinsi gani watakavyo jiengue kwenye hayo makampuni.
 
Mheshimiwa Philip Marmo katangaza kuwa wabunge wote ambo ni Wakurugenzi kwenye Mashirika ya Umma wataondolewa ili Kupisha accountability yao bungeni.
Ya kweli haya ama ni kiini macho kama kawaida?

Ni kawaida yetu kuwa na maneno matamu kama asali, matendo yetu hayalingani na tunayoyazungumza, tusubiri baada ya utawala huu kwa kuwa wakija watakuja watu wa SERA nyingine (YAANI WAZIRI atakayemrithi MARMO).
 
Tatizo letu hatujui kama sisi ni wajamaaa, mabepari wa soko huria, wakomunisti wa ubepari beberu au tunaganga njaa tu bila mwelekeo wala dira kama alivyosema marehemu Kolimba.

Huwezi kutoa msimamo kama huu wa serikali au bunge linaloongozwa na CCM bila kujua CCM inafuata siasa gani.Tunafuata Azimio la Arusha, la Zanzibar au tamko la juzi la Kikwete ambalo nalo halijatafsiriwa likaeleweka.

Kuna watu wanaweza kusema wabunge wanahitajika katika mashirika ya umma ili wawe na uelewa wa kweli wa jinsi gani mambo yanaenda, na ndiyo sababu rais anateua wabunge wengi katika bodi za makampuni / mashirika ya umma.

Kuna wengine wanasema huu ni ukiritimba na kupeana ulaji tu, wabunge ni wanasiasa, tuwaache professionals wafanye kazi za professionals na wabunge wawe watunga sheria.

Vipi kuhusu walio wakurugenzi katika makampuni binafsi? Wao hawatakiwi kujiuzulu? Wao hawana issue ya accountability na conflict of interest?

Je, mbunge mwanasheria anayewawakilisha Barrick Gold Mines hawezi kuwa na conflict of interest na accountability issues katika kuuliza na kuchangia hoja zinazohusu biashara ya madini?

Mimi nilifikiri mashirika binafsi ni issue kubwa kuliko mashirika ya umma na kama kuna move ya wabunge kuacha ukurugenzi basi ingeanza huko.Kama bado wajamaa that is.

Kama mabepari of course you just let the market decide.
 
Hakutangaza Hivyo Kwani Alisema Kuwa Ataenda Kulifanyia Kazi.

From what I gathered that was what exactly he said he was going to deal with it kwa sababu siyo jana wala juzi suala la kutenganisha siasa na shughuli binafsi kuzua mjadala.
 
Hawana jipya hao,

alianza kilanja wao "biasisa No" ameingia mitini hakuna kinachoendelea na huyo Marmo naye anajua anazuga tu!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom