Wabunge wote wa CCM wameshindwa kutetea maslahi ya wamachinga nchi nzima. Nini maana yake?

Ndugu wanaJamiiForums habari za asubuhi.

Ni jambo la kushangaza tena sana, kwamba ktk majiji ya Tanzania hasa Dar es Salaam na Mwanza majiji yanayokuwa kwa kasi sambaba na fursa nyingi za kiuchumi na biashara.

Katika majiji haya hivi karibuni na hata sasa wamekuwa wakibughudhiwa na serikali kwa kuwataka wahamie maeneo mengine na waache kupanga biashara zao kwenye hifadhi za barabara.

Pamoja na taratibu zote ambazo zinaendelea kumeonekana uvunjwahi wa haki za wafanyabiashara hawa ikiwemo kuharibiwa biashara zao na mitaji yao. Huku wamachinga wasijue la kufanya na hakuna aliyeko upande wao.

Ile CCM ya wanyonge iko wapi? Wale wabunge na wapiga kura wao umoja mbona hauonekani?

Je, ndio kusema urafiki wa wabunge hawa na wananchi wao upo tu wakati wa kupiga kura?

Dar es Salaam pekee kuna wabunge wasiopungua 8. Mwanza na maeneo mwngine wahunge woote ni wa CCM.

Hiki kigugumizi cha kutoishauri Serikali namna bora ya kuwahamisha huku tukipunguza madhara makubwa kwa wajasirianali hawa kinatokana na nini?

Ndio kusema wao hayawahusu as long as account zao zinasoma kila mwezi?

CCM kalaghabaho. Waliingia bila kuchaguliwa na wananchi kwa hiyo msitarajie msaada wowote wenye maana kutoka kwao.

Jamaa kareem
Ulitaka nini kifanyike?, maamuzi ni ya serikali na kumbuka wamachinga wengi hawalipi kodi na wanavunja sheria za nchi.

Wametolewa walipokuwa ili wajipange upya. Ni vurugu mechi kila sehemu iliyo wazi kufanyiwa biashara.
 
Back
Top Bottom