MaryGeorge
Member
- Aug 20, 2010
- 62
- 14
wabunge tumewaamini tukawachagua kutetea maslahi ya majimbo yenu na watanzania kwa ujumla ikiwemo kutolea ufafanuzi suala la dowans. Ninawaomba msitusaliti jamani msiingie mtego wa collective responsibility kwani hiyo ni dhambi na kumbukeni kwamba mungu hatawahukumu collectively bali kwa uamuzi utakaofanya binafsi wa kuamua kuunga mkono ufisadi na kujichafua kwa kukitetea chama. Kumbukeni kusimama kwenu kidete kama alivyofanya mh. Anne kilango wakati wa richmond ina dhawabu kubwa mbinguni na pia kwa wapiga kura wako.
Chondechonde nendeni dodoma mkiwa na hofu ya mungu na mkumbuke matokeo ya dhambi ya dowans yatakapoanza kuadhiri uchumi wa tanzania na kuongeza vifo vya maskini wasio na hatia hamtakwepa hukumu ya mungu. Simameni imara mjue walioko upande wenu ni wengi kuliko walio kinyume nanyi.
Mungu awape ujasiri na udhubutu wa kusimamia haki kwa mustakabali wa nchi yetu na maendeleo ya wapiga kura wenu. Kukubali kughilibiwa ni kupoteza credibility kama mwakilishi wa wananchi.
agreed!!!! & suppported!!