Wabunge wote wa CCM wameitwa dharura kikao cha DOWANS kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wote wa CCM wameitwa dharura kikao cha DOWANS kesho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kenge (Eng), Jan 19, 2011.

 1. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 498
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Habari za kuaminika sasa hivi wabunge wote wa CCM wameitwa Dodoma kuandaa na kuweka mkakati wa pamoja juu ya Dowans. Nia ni kuzibwa midomo na imetamkwa kwamba DOWANS ina masilahi gani na kila jimbo la mbunge.

  BARAZA la mawaziri limeazimia hakuna kujadili suala hilo.

  Taarifa hizi nimepata toka kwa mmoja wa wabunge akiwa anajiandaa kuelekea DODOMA.
   
 2. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 617
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  hata Mzee wa viwango bunge la tisa na msaidisi wa waziri wa mabarabara?


  mmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhh
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,684
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Wabunge tumewaamini tukawachagua kutetea maslahi ya majimbo yenu na watanzania kwa ujumla ikiwemo kutolea ufafanuzi suala la DOWANs. Ninawaomba MSITUSALITI JAMANI msiingie mtego wa collective responsibility kwani hiyo ni DHAMBI na kumbukeni kwamba Mungu hatawahukumu collectively bali kwa uamuzi utakaofanya binafsi wa kuamua kuunga mkono UFISADI na kujichafua kwa kukitetea chama. Kumbukeni kusimama kwenu kidete kama alivyofanya Mh. Anne Kilango wakati wa Richmond ina dhawabu kubwa Mbinguni na pia kwa wapiga kura wako.
  Chondechonde nendeni Dodoma mkiwa na hofu ya Mungu na mkumbuke matokeo ya dhambi ya DOWANS yatakapoanza kuadhiri uchumi wa Tanzania na kuongeza vifo vya maskini wasio na hatia hamtakwepa hukumu ya MUngu. Simameni Imara mjue walioko upande wenu ni wengi kuliko walio kinyume nanyi.

  Mungu awape ujasiri na udhubutu wa kusimamia haki kwa mustakabali wa nchi yetu na maendeleo ya wapiga kura wenu. Kukubali kughilibiwa ni kupoteza credibility kama mwakilishi wa wananchi.
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,617
  Likes Received: 1,109
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimepata tetesi kwamba tusidhanie zile pesa atakula R Aziz peke yake, yeye ni kama njia tuu ya kuzipitishia inasemekana eti, miaka yoote sisiem inazoa pesa kifisadi toka B.O.T kwa ajiri ya kughalamia chama, lakini uchaguzi huu wa October2010 ilishindikana kuiba pesa za kuendeshea kampeni kupitia mradi wa vitambulisho vya Taifa hivyo pesa za kughalamia kampeni ziliazimwa kwa RA na kwingineko Hivyo hizo pesa zinachukuliwa ni kwa ajili ya chama ili iweze kulipa deni la hawa waheshimiwa.Na kwa mantiki hiyo kila mbunge wa sisiem bila kujijua atakuwa amenufaika na hilo fungu jimboni kwake maana zilitumika kuweka mabango ya mkulu pembeni mbunge. Ndo maana AR ana nguvu sana nchi hii.
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 8,519
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hivi hakuna njia ya kumfukuza mbunge baada ya kumchagua?? Wajuzi wa katiba tusaidieni.................... Nafikiri some of these MPs have to be recalled.
   
 6. A

  African Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The principle of collective responsibility= we sink together we float together!
   
 7. A

  African Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutategemea nini bunge lililojaa mapedejee kama Hon abdul mteketa, professor maji marefu, na pedeshee amos makala?
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,467
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hakuna. Labda umfukuze kwenye chama kilichompa tiketi ya kugombea.
   
 9. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mmmh! Haka ka-Nchi kananuka rushwa. 2005 India wakaleta magari kwa sisi "M", wananchi tukafaidi mkataba bomu wa RITES na kupanda kwa gharama karibu zote kwa asilimia 200 hadi 500. 2010 tukaona helkopta tatu za hicho chama zikipishana angani kama maonyesho ya vita na suzuki tele kwa watendaji wake; wananchi tunachomekewa malipo ya "Do-Once" na ongezeko la umeme na kupanda kwa gharama mbalimbali. Natamani kufa! Mnisamehe jamani ni hasira tu.
   
 10. B

  Batale JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 803
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Hakuna namna MR. Zero kwa mjibu wa katiba yetu labda chama chake kimvue uanachama, nafikiri kubwa hapa ni maandamano ya kitaifa tu kwa serikali na pia kuwazomea wabunge wenye kuendekeza uchama.
   
 11. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Another disappointing news! Siku yangu imeshaharibika tena!
   
 12. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,277
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mkuu haya ni maneno mazito sana,na baada ya kikao hicho basi waende kuwaeleza wapiga kura wao kuwa pesa tuzohongana ndizo tunazilipa kupitia DOWANS.
   
 13. l

  limited JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 297
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nani amewaita?
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,617
  Likes Received: 1,109
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu yangu. nakunea imani
   
 15. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,280
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wabunge mlio wachagua baada ya kuhongwa kofia, tshirt, pombe na khanga mnategemea nini? Wacha wafanye vitu vyao. Spika Makinda atakuwa mkali kama pilipili. Hakuna cha wapambanaji wala nini, Chadema watapiga keleleeee mwisho kura...halafu wengio wameshinda. Nchi hii inalika kirahisi wandugu...rais fisadi unategemea nini?
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,105
  Likes Received: 523
  Trophy Points: 280
  waende wakajadili then waweke kando maslahi ya taifa..........sisi tupo na wala wasidhani hatuoni ......nani alijuia tunisia yatatokea !!!

  na huyu wa kwetu hapa jamani lazima tufanye namna hadi 2015 ni parefu mno.....atatuua huyu
   
 17. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Napata shida kuamini hili....
   
 18. P

  Popooo Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Uovu huo uta wageukia. Ole wao walikunywa damu ya walala hoi.
  tutakutana 2015.
  Mtatueleza kama mmeburuzwa au mmhiari.

  Tume choka. :frusty:
   
 19. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,003
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli inatishaaa!! Ila naamini kati yao kutakuwemo na wacha MUNGU! Wabunge wetu wapendwa msikubali kuendeshwa kama bodabodaa!! Tambueni kuwa nanyi mnapaswa kusikilizwa na hao wanaowaiteni!katu msiendeshwe jaribun kutambua thamani yenu vinginevyo mtaonekana TABULA LASA na waliowachagueni!!
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 20,608
  Likes Received: 3,094
  Trophy Points: 280
  Wale walioshindwa uunge nao itakuwaje?....wataitwa nao au vipi?
   
Loading...