Wabunge Wote Ni Mafisadi.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,609
1,736
Kama tuonavyo muungano wa vyama vya upinzani umevalia njuga ubadhirifu wa fedha za walala hoi,kama ni kupotea kwa fedha nyingi kwa matumizi yasiyojulikana basi hata Bunge linakula fedha tena nyingi sana kuliko hata hizo zilizopotea BOT.
Ushirika wa wapinzani ulikuwa uwe wa kwanza kupinga posho ,kiwango cha mshahara na kiinua mgongo baada ya kumaliza awamu ya miaka mitano.
Hebu mliopo Ulaya tuulizieni mbunge au mwakilishi anapokea kiasi gani kwa mwezi,halafu turudi na hessabu za wabunge wetu wanaopiga makofi na kugonga meza,ambao kazi yao kubwa ni kuzungumzia maambukizo ya ukimwi,mambo yao vichekesho vitupu,yaani hata mtu hahusiki na wizara ya afya anakwenda kuzungumzia mambo ya ukimwi huu kama si wizi wa kimacho macho ni kitu gani ?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,345
38,995
di ndiyo hapo, halafu mtu kashasema "wabunge wote ni mafisadi" siyo swali wala nini, ni statement of fact, sasa unauliza watu wakufanyie homework ya nini?
 

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
253
11
Mi sijakuelewa, inaonekana umesahau Slaa alikuwa mbunge wakwanza kukubali mapato yake yakatwe kodi, wale walio wengi toke chama cha kijani, wakapinga.
 

Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,132
1,333
...nipo hapa basement natunga kibao kikali sana kuhusu mafisadi nikimaliza nitakipost mkisikilize you know nina kipaji kikali sana cha kuimba na kutunga nyimbo
 

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,609
1,736
Mi sijakuelewa, inaonekana umesahau Slaa alikuwa mbunge wakwanza kukubali mapato yake yakatwe kodi, wale walio wengi toke chama cha kijani, wakapinga.
Sina uhakika kama alisema hayo,na kama alisema basi alikuwa katika kufurahisha wengine mbona pia yupo Mbunge huko huko upinzani aliedai wabunge waongezewe chochote au hukumsikia huyo.Nikirudi kwa Slaa huyu nimemweka katika hesabu za magoigoi ukimlinganisha na Shujaa Zitto ambae hakurudi nyuma,Slaa kama si goigoi asingeliondoa moyo wa kuibua ufisadi ndani ya bunge .lakini akasema eti anaepuka kama yaliyomkuta Zitto ,ila huo ni uwongo mkubwa kuliko yote,hapa anaona mshahara na posho havitakuwepo,na kama hiyo hoja yake ya kutaka wakatwe fedha basi yeye angechukua kiasi kile anachoona kinastahiki kupata na kilichozidi akapiga makelele kwamba si haki yake na irudishwe huko huko bungeni,hapo angefahamika na kueleweka.
 

Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,984
1,589
hili neno Ufisadi tumelichukua toka kwa jirani zetu Kenya. Nakumbuka jinsi rais wa zamani huko Kenya alivyokuwa akipiga kelele kuhusu ufisadi wa watendaji wake.
 

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,609
1,736
Hata wewe unaweza kuuliza maswali haya badala ya kuleta uvivu na kutaka ufanyiwe kila kitu kama kitoto kichanga!

Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu ,sasa kila kitu nikifanya peke yangu itakuwa ndo ndo ndo.
 

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
28
Pamoja na hoja nzuri kwamba wabunge wote mafisadi lakini tukumbuke yafuatayo.
1. Wabunge wa upinzani ni wachache na mara nyingi wamekuwa wakitete hoja mbali mbali kwa kukataa kuinga mkono na walio wengi wanapitisha.

2. Issue ya mishahara na marupurupu mengine ya Ubunge hata kama wapinzani wakipinga bado ikipitishwa na wengi, wao watafaidika (Free riding problem).

3. Mafisadi kama ilivyochaguliwa ni mtu anayechukua au anajipatia au jinuifaisha Moja kwa moja kwa kufanya maamuzi ambayo anajua kwa maamuzi anayofanya ataidika aidha moja kwa moja ama kupitia mtu mwingine. Nachelea kusema wabunge wote ni mafisadi.
 

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,131
40
Kha, Nyani wee... Mimi mbunge wangu hata kama ni wa CCM sio fisadi. Barabara anabaniwa tu kwakuwa alimzidi kete mwenzake ambaye huenda ndiye fisadi. Well done mbunge wangu Kamala


Nyoooo!

we mnyoo kweli kweli...eti worm-unamzungumzia yule mwenye Phd fake?

Asha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom