Wabunge wetu VS MaRC na MaDC; Mpambano Taarifa za Njaa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,469
2,000
Wabunge wa majimbo tuliwachagua mtusemee kwa heri na shari, nyie ndio vinywa vyetu. Maeneo mengi sana nchini kuna upungufu mkubwa wa chakula kwa maana halisi ni njaa.
Wakuu wa mikoa na wilaya wamepewa maagizo hili jambo kutolisema la sivyo kazi hawana. Na hawa watu hayo maeneo yao ya kazi sio kwao bali ni ajira tuu imewapeleka huko hivyo wanalinda ajira zao. Jee nanyi Wabunge mtaogopa kusema ukweli kuhusu hali ya wananchi wenu kuponea maembe eti kwa sababu wakubwa hawataki hayo yasemwe? Kwani nyie Wabunge waajiri na wakubwa wenu ni nani kama sio hao wananchi wenye njaa?
Njaa katika nchi ni njaa haijalishi kuwa imeletwa na ukame, mbegu mbaya au uvivu. Watu wanahudumiwa then kama kuna uvivu sheria za nguvu kazi zinafuatia. Ni sawa na mtu aliyekunywa sumu anahudumiwa kwanza kesi baadae na haachwi afe eti kwa vile kanywa mwenyewe..
Wabunge sasa ni wakati wa kuonyesha kuwa RC na DC hawana faida yeyote kuwepo maeneo yenu kama wataficha njaa na nyie kama hamtasema hali mbaya ya chakula maeneo yenu tutawatangaza kwa majina ili wananchi wajue kuna haja gani kumchagua mbunge wa aina hiyo ambaye anafanya kazi kwa kufuata maagizo kama DC.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom