Wabunge wetu na kushangilia kusiko na tija

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,479
2,000
Amani ya bwana iwe nanyi. Siku mbili hizi kuna picha inatembea mitandaoni ikimuonyesha mwanamama mbunge akipiga ama akigonga meza kuonyesha kuunga mkono matamshi yaliyomo ndani ya hotuba ya Mama Suluhu.

Ni haki yake kufanya vile, lakini unajiuliza je kulikuwa na ulazima wa kufanya vile?!. Bunge ama Wabunge wetu wamekuwa na tabia ya kushangilia pale wanapokosoleea.

Rejea kauli ya kudemka haiukuwa kauli nzuri kufikishwa kwa Bunge tena na mkuu wa nchi wengi mliona Naibu Spika akishangilia kwa kupiga makofi.

Ajabu sana. Ile kauli ilitakiwa ukumbi uwe kimya ili ile sindano iliyokuwa na dawa ya kudemka iweze kupenya maungoni mwa mgonjwa (Bunge/wabunge), kama kuna kozi ya ushangiliaji basi inabidi ipelekwe bungeni.
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,127
2,000
Katika mihimili mitatu ya nchi Bunge ndilo linawatu vilaza zaidi. Lakini wale ni wawakilishi wa wananchi, hili linasema nini kuhusu waanchi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom