Wabunge wetu hawa wana bongo ngapi kichwani?

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Siasa si mchezo wa vichekesho. Siasa ni kazi maalum yenye mchango wake katika maendeleo ya taifa letu kama madaktari, mabwanashamba, wanajeshi nakadhalika. Tunapokwenda kwenye uchaguzi tunakuwa tunatafuta watu watakaofanya kazi maalum kwa maendeleo ya taifa letu.

Tumechagua wabunge ili waweze kufanya kazi kama wabunge na wawakilishi wa wananchi katika kuisimamia, kuishauri serikali.

Tumeletewa mfumo wa siasa za vyama vingi na kwa kweli wakati wa awamu iliyopita pale serikali ilipokuwa imelala tumeona manufaa yake.

Haya. 2015 tukafanya uchaguzi. Tukampata rais anayeyaangalia matatizo ya wananchi kwa makusudi ya kuyatatua. Tumelitengeneza bunge. Tukaongeza idadi ya wabunge wa vyama vya upinzani. Tukatarajia kuona nguvu ya upinzani ikiisaidia serikali hii inayoonekana kuyaangalia matatizo yanayogusa wananchi.

Ninaanza kuwa na matatizo na mambo ninayoyaona yakiendelea bungeni. Kuna wabunge hawaoni ulimwengu unachoona kikifanywa na serikali. Ndani na nje ya Tanzania kila mwenye akili kamili anaona serikali ya Magufuli inachokifanya na kila kona anapongezwa.

Niongelee moja kama sio mawili: Serikali ilipotangaza kuwa mwaka ujao wa fedha (2016/17) inatarajia kutumia fedha za kitanzania Trilion 29 kutoka trillion 22 za mwaka unaoisha. Viongozi wetu walisimama kidete kuikatalia serikali kuwa haiwezi kuzikusanya fedha hizo kwa hiyo bajeti hii ni kiini macho.

Binafsi nilielewa wanalolisema japo niliielewa serikali kuwa kwa juhudi inazoonyesha za kukusanya kodi na kubana matumizi inaweza kuzifikisha. Kilichonitisha ni pale wakati wabunge hao hao wakijadili bajeti za wizara wanaibuka na kutaka budget za wizara zisipitishwe kwa sababu wizara zimetengewa fedha kidogo. Nashindwa kuwaelewa wawakilishi wetu.

Wanapendekeza wizara ziongeze fedha (kwa kuwa hazitoshi) ambazo zinatokana na budget wanayotaka ipunguzwe (kwa kuwa haziwezi kupatikana). Kuna bongo ngapi vichwani mwao? Sielewi. Lakini mbunge mwingine ambaye anaheshimika sana anasema wabunge watamkumbuka JK. Watamkumbuka kwa sababu hakuwahi kuwazuia kumsema.

Kazi ya bunge ni kumsema rais au kuisaidia serikali? Mbunge huyo anasema hivyo kwa sababu bunge limemzuia kumbambikiza Magufuli ujinga kuwa aliuza nyumba za serikali. Wabunge hawajui kuwa Magufuli hakuwahi kuuza nyumba hizo bali serikali iliuza nyumba zake kwa uamuzi wake na Waziri (Magufuli) akatekeleza uamuzi wa serikali.

Anaambiwa aondoe neon magufuli na aweke neon Serikali nanasema hawezi kusoma maoni ya kambi ya upinzani. Upumbavu huu naulinganisha na ule ambao watu wazima walifafanuliwa zaidi ya mara nyingi kuwa Dr. Slaa alisema ataanzisha mchakato wa katiba ndani ya siku 100.

Wao wakaendelea kusema alisema atalipatia katiba Taifa ndani ya siku 100. Nauita upumbavu kwa sababu hawakuelewa kabisa licha ya kufafanuliwa. Ni huo ambao watu wanalinganisha uuzaji wa nyumba na kashfa ya Richmond.

Wabunge wanaotaka mijadala ambayo inaisha baada ya kujadiliwa wataua upinzani. Tunatarajia wajadili mambo yatakayoleta matunda baada ya kujadiliwa. Kutaka kujadili nyumba zilizouzwa na serikali kunatarajia kuleta faida gani baada ya mjadala.

Mtu mmoja ameniuliza kuwa sababu ilizotoa serikali kutoonyesha mijadala ya bunge live ni sahihi? Nikamjibu kuwa sio sahihi. Sababu ni kuwa serikali ilitaka kuliondolea taifa aibu kutokana na mijadala kamahi kama ambavyo watu fulani huwaficha watoto walemavu ili kuficha aibu za familia.
 
Haaa sasa jamaa kajipinda kaandika yote hyo mmempuuzia.

Mtamfanya mwenzenu akose buku 7.
 
Nchi masikini hii mkuu kuwa mzalendo japo kidogo kwa mustakabali wa Taifa lako mimi,wewe na hao viongozi unaowapamba kila kukicha wanapita tuu ila Tanzania itabaki kuwa Tanzania tuwe na nyuzi za kujenga Taifa na si kubomoa au kuwatenga Watanzania..
 
Wabunge hawa wa Upinzani wamebaki Na sifa moja YA VITA KUMTETEA MGOMBEA WAO ALITENDEWA NINI NA BUNGE NA KWA NINI VIONGOZI WA SERIKALI YA CCM WASITENDEWE NAO NA BUNGE.HILI NDILO NINALOLIONA WAO KILA KUKICHA NI KWA NINI KWA NINI!!!!! BADALA YA KULETA HOJA AMBAZO HOTUBA ZA BAJETI ZA WIZARA ZINAGUSA MAJIMBO YAO KWA MASLAHI YA WAPIGA KURA WAO HATA KUPENDEKEZA VIFUNGU FULANI VIBADILISHWE.WAO WAMEBAKI NA HOJA AMBAYO NDIYO KETE YAO YA KUHAKIKISHA SERIKALI YA AWAMU YA TANO INASHINDWA KUITEKELEZA ILANI YAO.HAWA WAHESHIMIWA WAJIREKEBISHE TUNAJUA WAKO MJENGENO KUMTETEA MTU FULANI NA SIYO WAPIGA KURA WAO BAADA YA KIONGOZI WAO KUKOA NAO KUAMBUKIZWA KIKOZI.HUU NDIYO UKWELI NJE YA MJENGO MAGAZETI TV TUONAVYO WAPIGA KURA.
 
Back
Top Bottom