Wabunge wenu na hoja zisizo na masilahi kwao!

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Zitto akwama bungeni

na Sauli Giliard, Dodoma



MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), jana alikumbana na wakati mgumu baada ya wabunge kugoma kuunga mkono hoja yake ya kutaka kuwazuia wabunge kuwamo katika bodi za mashirika ya umma.


Zitto alitaka yafanyike marekebisho katika muswada wa korosho uliowasilishwa jana bungeni na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, ambapo alibainisha kuwa ni vema kipengele cha kuwazuia wabunge kikajumuishwa.
Alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wanasiasa kutoingizwa katika bodi za mashirika ya umma, ikiwamo korosho, ili kuepusha migongano ya kimasilahi.
Pendekezo hilo aliliwasilisha jana asubuhi, lakini jioni wakati wa uhitimishaji, wabunge hawakumuunga mkono, hali iliyofanya kutupwa kwa marekebisho hayo.
Katika utetezi wa kutaka kukubalika kwa hoja yake, Zitto alibainisha kuwa katika Bunge kuna wabunge 322, lakini waliomo kwenye mashirika hayo ni 35 tu, ambao wengine wamekuwa wakizunguka katika bodi zaidi ya moja. Alisema madhara ya wanasiasa kuwamo katika bodi hizo kuna sababisha mgongano wa kimasilahi wakati wanapofanya maamuzi kadhaa katika mashirika ya umma, jambo ambalo kimsingi linaathiri ufanisi wa chombo husika.



“Kuna umuhimu wa wanasiasa kuondolewa katika bodi hizi. Huwa tunapopita katika mashirika ya umma tunapata matatizo makubwa kwa Kamati yetu ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Mashirika ya Umma,” alilieleza Bunge. Zitto alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utoah, alishawahi kupendekeza jambo hilo ili kuleta ufanisi katika mashirika hayo. “Hili jambo si geni, ni ukweli usiopingika kuwa kuwapo kwa wabunge katika bodi za mashirika ya umma kwa namna moja au nyingine kunashusha uwajibikaji wa mashirika hayo,” alisema Zitto.


Pamoja na utetezi huo, bado Zitto hakuweza kupata uungwaji mkono wa wabunge.
Mwenyekiti wa Bunge, Job Ndugai, ambaye alikuwa akiendesha kikao hicho cha jioni, alimtaka Zitto akubaliane na matokeo, kwa kuwa hoja yake haikuungwa mkono na wabunge. “Mheshimiwa Zitto, ulitoa hoja ya kuwapo kwa marekebisho katika muswada wa korosho lakini kutokana na kutoungwa mkono na wabunge, pendekezo hilo haliwezi kuwa halali,” alisema Ndugai.



Awali, Zitto alibainisha kuwa anashangazwa na muswada huo mpya kutoweka bayana kuhusu suala hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likisababisha mkanganyiko wa utendaji kazi, hasa unapofika wakati wa kufanya maamuzi yenye kuiwajibisha bodi ya shirika fulani.


......................................................

Kama kawaida maslahi binafsi mbele.......ya taifa baadaye....

 
Hili ndilo linaloongeza umuhimu wa mabadiliko. Asante sana ndugu Kabwe maana umetimiza wajibu wako. Jukumu ni kwetu wapigakura kutimiza majukumu yetu kwa kuwaondoa hawa wabinafsi na wadhalimu. Bunge lililojaa mafisadi wa chama kimoja kamwe haliwezi pitisha chochote kinachowaondolea maslahi binafsi. Lazima watanzania tujue nafasi yetu katika kuleta mabadiliko ya kisera na utawala nchini na tutimize wajibu wetu kama Zito alivyofanya.

Maana naamini fika kwamba Zito alitabiri vikwazo lakini uthubutu na utambuzi wa majukumu yake kwa uma na ustawi wa taifa hili amekua akitetea hoja mbalimbali za maslahi kwa taifa hili.

Swali ni je, wewe na mimi tunafanya nini katika kutimiza majukumu kwa taifa hili? Tutazungumza nini mbele ya wajukuu zetu watakapo tuuliza tulilitendea nini taifa hili? Hatma ya nchi hii tunaiweka mikonioni mwa nani? Tunafanya nini kuelimisha wenzetu ambao hawajapata nafasi yakuona na kuyatambua haya tuyaonayo tuliobahataki kuyajua (disadvantaged group)?

Haya ni mapambano ya dhati na yanahitaji jitihada hata zaidi ya mapambano ukimwi na mapambano yanaanza na wewe na mimi maana kwa pamoja tutaihamisha dunia.

Tusipo wajibika na kuthubutu taifa hili litaendelee kudumazwa na hatutakua na wakumlaumu maana tutakua tumejichagulia wenyewe.

Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi wenyewe. si kwa upanga wala Kombeo ila kwa kila mmoja kutambua wajibu wake na kuutekeleza. 2010 hiyoooo..... tutarudia kuongelea yale yale... wakati wenzetu wanasonga mbele. Tuweke jitihada za maksudi kubadili sura za bunge letu.

Hongera kwa watanzania kwa mabadiliko japo kidogo yalojitokeza kwa serikali za mitaa, ila kasi ni ndogo sana na hairidhishi. Kwa kasi hii mabadiliko yatakuja baada ya karne.


Yetu Macho
 
Back
Top Bottom