Wabunge wengine wahongwa tena; Baadhi waogopa, wazisalimisha kwa Spika

hili bunge letu ni kimeo, makinda kazi imemshinda bora sita alikuwa anajaribu jaribu.
Ndio tatizo la kuendekeza siasa za fitna badala ya kuangalia uwezo na uadilifu wa mtu.
 
wabunge wasipojihadhari watakuwa vichaka vya wenye nacho maana umaskini wa wabunge wetu ndio unapelekea kufanya haya na kujisahau kuwa wamechanguliwa na wananchi kwa ajili ya kutetea masirahi ya taifa wala si kikundi fulani
 
Huyu atakuwa ni Manji tu hakuna mwengine, kwanini huyu Manji hakamatwi su ndio Serikali ya kulinda na Mr dhaifu
 
Hii nimeipenda sana.
'Miongoni mwa waliokataa mwaliko na hundi hizo ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). “Nakuhakikishia kuwa sikupokea, mimi ni masikini jeuri, nilikataa kwenda kwa sababu nilijua ni masuala ya rushwa,” amesema Mdee'.

VIVA Halima, ubarikiwe sana
 
Aiseee babaangu huyu jamaa ndie anamiliki ile timu inayovaa jezi zi njano kama za magamba
 
Harufu yake siyo nzuri hata kidogo. Wamepokea, halafu wakakaa nazo, tena wakazipeleka kwa Makinda.

Harufu ipo lakini bahati mbaya TAKUKURU inasubiri chaguzi za ndani za CCM.
 
Halafu, hivi kwanini Wahindi wanapenda sana kutoa toa rushwa? Mimi nafikiri kwasababu ni wezi wa kila kitu, wanahamisha mapato kupeleka nje, na ndio maana wanashikia bango suala la uraia wa nchi 2 au zaidi waruhusiwe ili iwe rahisi kwao kusepa.

Rushwa nchini India ni jambo la kawaida mno. Huenda wamerithi kutoka kwao!
 
Huyu atakuwa ni Manji tu hakuna mwengine, kwanini huyu Manji hakamatwi su ndio Serikali ya kulinda na Mr dhaifu

Mkuu ulizipata na kuzisoma zile nyaraka za Kagoda? Uliuona uhusika wa Manji ulivyokuwa mkubwa? Je mpaka sasa Kagoda wana kesi? je unategemea Manji awe na kesi? Jioni njema mkuu kama uko Bongo!
 
Tundu Lisu, Tundu Lisu tunakuita wanajamii tuambie ulipokea hukupokea??? Tuambie Mh. Tundu Lisu
 
Makubwa haya!!! Ngoja nipite!!! TAKUKURU dhaifu na legelege, sijui nao wako kwenye pay roll!!?
 
Hili ni jungu kubwa, mpaka nione copy ya hundi iliyotoka kwa manji ndoo nitaamini. Every detective must produce evedince of his findings. Otherwise this is sheer nosense.
 
Mh! nashindwa kuelewa tungepata ufafanuzi lengo kuu la hao wabunge kupatiwa hizo fedha ni nini, huyu mfanya biashara alikuwa anatarajia kusaidiwa nini na hao wabunge, hapo nikipata majibu moja kwa moja nitakuwa na uhakika hiyo ilikuwa rushwa lakini kama hakutakuwa na maelezo ya kina inawezekana kwa mapenzi yake mwenyewe kaamua kufanya hivyo bila kutarajia kitu chochote kutoka kwao.
 
Hii sentensi umeielewaye?

Mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia amewahonga wabunge kadhaa wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, JAMHURI imethibitishiwa.

Kuna tatizo kubwa sana la kuelewa matumizi ya aina za maneno [Parts of Speech kwa baadhi ya GTs hapa jukwaani] Baadhi hawaelewi matumizi ya vivumishi na vielezi. Kuna haja ya kuanzia Jukwaa la Lugha moderators.
 
Aliewapa Rushwa ni mwenyekiti wa club moja maarufu(jina tunalo) ambayo ni watani wajadi na Club ya Simba,ambae alikua ana kesi na mmiliki wa kampuni ya IPP MEDIA Bwana Mengi,na akaomba mahakamani Mengi amlipe fidia ya shilingi moja tu,Club hiyo Maarufu makao makuu yake yapo pale yalipohitimishwa maandamano ya Waandishi wa habari(jina tunalo).....!
 
Huyo mfanyabiashara ni mwenyekiti wa moja ya klabu kongwe ya mpira wa miguu. Tusubiri rafu na rushwa itakayo itikisa soka la Tanzania hivi karibuni.

atapenyeza rupia had ynga iwe timu ya kwanza afrika kucheza UEFA.
 
Back
Top Bottom