Wabunge wengine wahongwa tena; Baadhi waogopa, wazisalimisha kwa Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wengine wahongwa tena; Baadhi waogopa, wazisalimisha kwa Spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uhalisia Jr, Sep 11, 2012.

 1. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia amewahonga wabunge kadhaa wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, JAMHURI imethibitishiwa.

  Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wabunge na Ofisi ya Spika zinasema kwamba rushwa hiyo ilitolewa kama "asante" kwa wabunge hao baada ya kuzuru moja ya vitegauchumi vya mfanyabiashara huyo kilichopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, wiki kadhaa zilizopita.

  Mfanyabiashara huyo, ambaye ni mpenzi wa michezo nchini, pamoja na kuwahonga wabunge, amekuwa akituhumiwa kuwaweka baadhi ya waandishi wa habari kwenye malipo ya kila mwezi. Mkakati huo umemsaidia kutoguswa na vyombo vingi vya habari.

  Miongoni mwa wabunge wanaotuhumiwa kupokea hundi ya Sh milioni moja kutoka kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala; Pindi Chana. Hata hivyo, mbunge huyo amekataa kukubali au kukanusha taarifa hizo zinazoihusu Kamati yake.

  Habari zaidi zinasema baadhi ya wabunge walipokea hundi, lakini baadaye wakashituka na kuzisalimisha katika Ofisi ya Spika. Pamoja na Kamati hiyo, kuna habari kwamba wajumbe wa Kamati nyingine kadhaa nao walialikwa na kupewa kitita cha fedha. Hundi hizo ziliambatanishwa na barua za kuwashukuru wabunge hao kwa kuzuru eneo hilo la biashara.

  Lakini cha kushangaza ni kwamba hata wabunge ambao hawakushiriki ziara hiyo, nao wanadaiwa kupelekewa hundi za Sh milioni moja kila moja, na barua za shukrani. Hatua hiyo, pamoja na kutokana na msukumo wa kimaadili miongoni mwa wabunge hao wachache, inaelezwa kwamba ilitokana na hofu ya vita dhidi ya rushwa iliyowaingia wabunge.

  "Baadhi ya wabunge waliona hili ni ‘bomu', wakaamua kusalimisha hundi hizo kwa Spika, lakini wengine wakatulia nazo," amesema mbunge mmoja. Miongoni mwa waliokataa mwaliko na hundi hizo ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). "Nakuhakikishia kuwa sikupokea, mimi ni masikini jeuri, nilikataa kwenda kwa sababu nilijua ni masuala ya rushwa," amesema Mdee.

  Mwingine anayesemekana kuzikataa fedha hizo ni Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM). Chanzo cha habari kinasema aliwasihi mno wabunge wenzake kuepuka kitendo hivyo haramu. Alipoulizwa na JAMHURI kwa njia ya simu, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alikwepa kuzungumzia suala hilo kwa maelezo yake kwamba alikuwa katika ziara ya kiofisi nchini Srilanka na hivyo akamtupia mzigo huo Katibu wa Bunge.

  "Hii tabia ya mtu kuwa mbali anazungumzia mambo ya Dar es Salaam si nzuri, mimi niko Srilanka kwenye mkutano… mtafute Katibu wa Bunge, sipendi majungu hata siku moja," alisema Spika Makinda kwa ghadhabu. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, juhudi za kuwasiliana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, hazikuzaa matunda baada ya JUMHURI kumpigia simu yake ya mkononi mara kadhaa ikiita bila kupokelewa.

  Wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ni Chana (Mwenyekiti), John Lwanji (Makamu Mwenyekiti), Abbas Mtemvu, Nimrod Mkono, Halima Mdee, Fakharia Khamis Shomar, Zahra Ali Hamad, Mussa Haji Kombo, Felix Mkosamali, Blandes, Azza Hilal Hamad, Mustapha Akunaay, Jaddy Simai Jaddy, Tundu Lissu, Deogratias Ntukamazina, Jason Rweikiza, Rashid Ali Abdallah, Mohamed Said Mohamed, na Dk. Haji Mponda.

  Hivi karibuni, Spika Anne Makinda alilazimika kuivunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini baada ya wajumbe wake kadhaa kutuhumiwa kupokea rushwa ili wakwamishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2012/2013. Pamoja na kuivunja, Spika aliagiza uchunguzi wa tuhuma dhidi ya wabunge hao uanze mara moja ili watakaobainika waweze kuwajibishwa. Pia aliahidi kuzifumua Kamati nyingine zenye vimelea vya rushwa.

  Ni dhahiri kuwa suala la rushwa bungeni sasa linaelekea kuwa jambo la kawaida. Rushwa imekuwa ikitolewa kwa baadhi ya wabunge, kwa ajili ya kusaidia kupitishwa kwa bajeti na hoja mbalimbali zenye masilahi kwa makundi ya wafanyabiashara.

  Uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika Aprili, mwaka huu, uligubikwa na rushwa ya wazi wazi. Licha ya vyombo vya habari kuandika na kutangaza habari hizo, hakuna hatua za dharura zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo.  Source: Gazeti la Jamhuri
   

  Attached Files:

 2. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Nashindwa kuliamini hilo gazeti la Jamhuri! No comments
   
 3. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hii nimeipenda sana.
  'Miongoni mwa waliokataa mwaliko na hundi hizo ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). "Nakuhakikishia kuwa sikupokea, mimi ni masikini jeuri, nilikataa kwenda kwa sababu nilijua ni masuala ya rushwa," amesema Mdee'.
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Huyo mfanyabiashara ni mwenyekiti wa moja ya klabu kongwe ya mpira wa miguu. Tusubiri rafu na rushwa itakayo itikisa soka la Tanzania hivi karibuni.
   
 5. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Halafu, hivi kwanini Wahindi wanapenda sana kutoa toa rushwa? Mimi nafikiri kwasababu ni wezi wa kila kitu, wanahamisha mapato kupeleka nje, na ndio maana wanashikia bango suala la uraia wa nchi 2 au zaidi waruhusiwe ili iwe rahisi kwao kusepa.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Taasisi ya Kuruhusu na kufagilia Rushwa nchini - TAKUKURU.....Alitakiwa awe lupango huyu maana kuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani lakini hili halitatokea kwa kuwa Serikali DHAIFU imeshika utamu.
   
 7. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  manji.!!!???? baniani mbaya kiatu chake dawa.!
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  ikiwemo kuinunua mechi ya october 3
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni tamu sana Mkuu!
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Maskini Yanga yetu!
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli wanasitahiri kuadhibiwa bila kujali chama wanachotoka wabunge hao
   
 12. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Kwahio hio Rushwa Asante aliitoa kwa ajili ya nini ?

  Je akisema hio ilikuwa ni motisha ya kazi yao nzuri ?
   
 13. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  kwa nini asingewaalika wanafunzi wa sekondari au shule ya msingi wakajifunze...hiyo ni rushwa na nina uhakika kuna magamba yamepokea...
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  bunge letu linakwenda wapi????????????

  bunge letu linaelekea wapi??????????????????
   
 15. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  safari hii zitto hakuitwa kupokea hummer lingine?? nonsense mbunge!
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Seriously, kamati ya Katiba na Sheria inafuata nini kwa wafanyabiashara?
   
 17. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Simple logic:

  Kama lissu ni mjumbe wa kamati na hakutajwa kuwa miongoni mwa waliokataa rushwa basi lisu .......................rushwa.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Hii sentensi umeielewaye?

  Mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia amewahonga wabunge kadhaa wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, JAMHURI imethibitishiwa.
   
 19. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napata shida kuhusu uhalali wa BUNGE hili na wengi walioko.
   
 20. papason

  papason JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Ragee, raage, umeishaanza mizengwe na fitna zako,ukishilikiana na friends of simbaa wenzako.......

  Tunakujua wee ni mzee wa fitna, majungu na uchonganishi!

  Kama tumewazidi 'maarifa' kwenye usajili usitake kulipiza kisiasa!
   
Loading...