Elections 2010 Wabunge Wengi Wakosea Viapo Vyao!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Nakumbuka Rais Obama aliapishwa mara mbili kwa sababu alikosea kiapo chake kwa sababu ya kuweka neno "faithfully" mahali ambapo si pake! Kiapo chake kilikuwa kama ifuatavyo:
ROBERTS: I, Barack Hussein Obama...
OBAMA: I, Barack...
ROBERTS: ... do solemnly swear...
OBAMA: I, Barack Hussein Obama, do solemnly swear...
ROBERTS: ... that I will execute the office of president to the United States faithfully...
OBAMA: ... that I will execute...
ROBERTS: ... faithfully the office of president of the United States...
OBAMA: ... the office of president of the United States faithfully...

ht_obama-2nd-oath_090121_mn.jpg

Chief Justice administers oath of office again to President Barack Obama at the White House

Kwa upande wa Wabunge wetu walioapa leo, naona wengi wamekosea viapo vyao, aidha kwa kuongeza maneno au kuyaruka au kuyabadilisha, lakini Mheshimiwa Spika, Anne Semamba Makinda amekubali viapo vyao bila matatizo yoyote.

Kiapo chenyewe kina maneno yafuatayo:

"Mimi......................................................, naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba, nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie."

Wafuatao ni Wabunge waliokosea kuapa:

1. Peter Joseph Serukamba: hakutaja neno "wa Tanzania" ie alisema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano (bila kutaja wa Tanzania)...
2. Haroub Mohamed Shamis: alisema Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
3. Said Musa Zuberi: alisema "na nitaitumikia" badala ya "na kuitumikia," pia alisema Ewe Mwenyezi Mungu, "unisaidie" badala ya "nisaidie."
4. Ayoub Jacob Hashim: alianza na maneno "Bismillah Rahman Rahim" ambayo hayapo kwenye kiapo na alimalizia kwa maneno "inshallah" ambayo hayapo pia kwenye viapo.
5. Asa Osman Hamad: alisema kwa mujibu wa Sheria "iliyoweka" badala ya "iliyowekwa."
6. Hamad Zahara Ally: alisema Ewe Mwenyezi Mungu "naomba" nisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
7. Shawalla Azan: alisema "nitahifadhi" badala ya "nitaihifadhi," pia alisema "nitalinda" badala ya "nitailinda."
8. Silima Musa Hamis: alitaja neno "sharia" badala ya "Sheria" ambalo lipo kwenye kiapo. Pia aliongeza neno "amin" ambalo halipo kwenye kiapo.
8. Salim Hassan Turkey: huyu alisema kwa mujibu wa Sheria, hakutaja neno "iliyowekwa."

Hayo ndio makosa niliyoyaona kwa leo, sikufuatilia viapo vya Waheshimiwa Wabunge jana, labda makosa hayo yalikuwepo pia.

Mimi naamini, nikiwa Mwanasheria, Waheshimiwa Wabunge waliokosea viapo vyao wanatakiwa warudie kuapa kwa mujibu wa Kanuni ya 24, Fasili ya 1 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, kama alivyorudia kuapa Rais Obama kwa Sheria za Marekani.

Tujadili.
 
wabunge wa kuchakachuliwa utawaona tu hata kiapo wanakosea...dahhh kazi kweli kweli
 
mkuu buchanan nimekukubali kwa attention yako to details,nafikiri kama kanuni inataka aliyekosea arudie kiapo basi kanuni zinapaswa kuheshimiwa.
 
Yap... hata jana... yalikuwepo mengi mfano "Naomba Mungu Unisaidie"
 
Mkuu ulirekodi nini ukawa unasikiliza taratibu!!
Mimi naona kama vile ni makosa minor sana, je yanaweza kuwa na implication huko mbele ya safari katika suala zima la kiutendaji?
 
Anyway heri wale waliokosea viapo maana at least wameapa! Kuna wabunge wengi sana hawakuwa wana-concentrate kwenye kiapo... wengine focus kubwa ilikuwa kwenye Kamera, wengine wakifiria wapendwa wao nyumbani (baba, mama, mchumba, mke, mume).... inasikitishwa unaona kabisa mbunge mteule ana haraka utadhani amekimbizwa.

Otherwise... it is okay... maana wamesaini viapo vyenyewe vile ndio binding.
 
Anayesema hapa jf wote ni mbumbumbu basi atakuwa mwenyewe ndo mbumbumbu. Najaribu kutatakari mkuu ulivyoyapata haya. Nimekukubali bwamkubwa. Kama mwanasheria nilijua ungeyapata tu kwani niwajuavyo wanasheria u r very exact and to the point. Thanx. Ila kwa Bongo hawa jamaa hawawezi kuapa tena labda ingekuwa kwa wenzetu!
 
Kazi kweli kweli. Hizi ni signs tu za kukosa umakini kwa Bunge la 10 na serikali ya JK. Mwanasheria alipashwa kurekebisha hilo lakini ndio hivyo tena.
 
Hii ndiyo aina ya mijadala yenye tija kwa taifa hili. Nakupongeza ndugu yangu Buchanan kwa 'post' hii. Binafsi nimeelimika sana. Thank you very much.
 
kama ni wageni labda walikuwa nervous kidogo
Mkuu,

Hii haikuwa kwa wabunge wageni tu, Cheyo (UDP) alikosea pia, alitamka maneno yake tu mradi kiapo kimefanyika.

Umakini wa wabunge wetu wengi ni mdogo, interview yao kabla ya kuajiriwa ni 60days, kidogo sana I may say!
 
Mkuu ulirekodi nini ukawa unasikiliza taratibu!!
Mimi naona kama vile ni kamosa minor sana, je yanaweza kuwa na implication huko mbele ya safari katika suala zima la kiutendaji?

Kwa bahati mbaya kwenye Sheria huwa hakuna dogo, nijuavyo! Kama umewahi kuhudhuria na kusikiliza kesi utakubaliana na mimi!
 
hakuna kosa minor hasa ukichukulia mtu ana tamka 'sharia' badala ya 'sheria' wakati kimsingi wa lugha ya kiswahili hivi vitu vina maana tofauti mno.

Japo kuwa kwa lahaja ya visiwani sheria na sharia hazina tofauti, lakini by law lazima litamkwe lile lililotakiwa kutamkwa na si vinginevyo.
 
Kwa bahati mbaya kwenye Sheria huwa hakuna dogo, nijuavyo! Kama umewahi kuhudhuria na kusikiliza kesi utakubaliana na mimi!

Hii ni kweli aisee. Mi nshawahi kuona watu wakiachiwa huru kwa vile tu tahajia ya jina lao ilikosewa.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom