Wabunge Wengi Wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Wamepata ambacho hawakukitegemea

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,524
Kuna Wabunge wengi hususan wa kutoka CCM, miaka yote waling'ang'ania saana hizi nafasi za Ubunge ili wapate mwanya wa Kulinda Biashara zao au kupiga pesa bure bure kwenye Kamati za Bunge.
Awamu hii ya 5 Rais Magufuli kawabana kisawasawa mpaka wanapangiwa kipi cha Kufanya ama kutetea Serikali muda wote.

Kuna Wabunge wengi walitumia fedha kubwa saana kupata nafasi za Ubunge. Mbunge wa Rungwe Mashariki Ndg. Sauli H.Amon ambaye ni Mmiliki pia wa Super Market za Vipondozi maarufu kwa jina la S.H.Amon Enterprises Ltd, Hotels kwa Jina la LandMark Hotel pamoja na Lodges kwa jina la PATTAYA, hakika huyu ndugu hana hamu tena Ubunge maana Umedhoofisha saana Kiuchumi. Mfano moja wapo ni Kufungwa kwa Landmark Hotel ya Ubungo.
Sasa hivi Ubunge hauna deal tena kwa Wale walioingia kwa gia ya kulinda Biashara zao na Kuvuna visivyo na Jasho.

Poleni Wabunge wa CCM.
 
Tulio Na Akili Tunajua Hata Sasa Wataisoma Number Bila Kujali Ikiwa Waliitetea Ccm Kwa Gharama Na Pesa Nyingi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Zamani walitangaziwa wakitaka biashara zao zishamiri basi wajiunge na ccm na hata ikibidi waombe uongozi! Ngoja waisome for next 10yrs then akili zitatengemaa vyema
 
Lakini kuna aliyeahidiwa neema baada ya tv yake kutumika kupiga jalamba kwenye kampeini, nadhani yeye mambo yake bado ni supa.
 
Habari ziwafikie .......... wakiwa mahakama ya Bunda.

Ujumbe: kila jambo na wakati
 
Ndo vizuri ili wakome kuhonga ili kupata ubunge tena magufuli akaze hivi hivi ili 2020 kuhonga kanga na ubwabwa kupungue tupate wawakilishi halisi
 
Kuna Wabunge wengi hususa wa kutoka CCM, miaka yote waling'ang'ania saana hizi nafasi za Ubunge ili wapate mwanya wa Kulinda Biashara zao au kupiga pesa bure bure kwenye Kamati za Bunge.
Awamu hii ya 5 Rais Magufuli kawabana kisawasawa mpaka wanapangiwa kipi cha Kufanya ama kutetea Serikali muda wote.

Kuna Wabunge wengi walitumia fedha kubwa saana kupata nafasi za Ubunge. Mbunge wa Rungwe Mashariki Ndg. Sauli H.Amon ambaye ni Mmiliki pia wa Super Market za Vippndozi maarufu kwa jina la S.H.Amon Enterprises Ltd, Hotels kwa Jina la LandMark Hotel pamoja na Lodges kwa jina la PATTAYA, hakika huyu ndugu hana hamu tena Ubunge maana Umedhoofisha saana Kiuchumi. Mfano moja wapo ni Kufungwa kwa Landmark Hotel ya Ubungo.
Sasa hivi Ubunge hauna deal tena kwa Wale waliyoingia kwa gia ya kulinda Biashara zao na Kuvuna visivyo na Jasho.

Poleni Wabunge wa CCM.
Kwa hiyo unatuambia bora tuchague wabunge wa chadema wapiga dili sio?
 
Dooh do! Basi hatakiwi kuombewa tena kama ni muongo hivi!
Ni hatari, Jamaa kachanganyiwa, aliiondoa chanel yake kwenye startime, mpaka wamlipe pesa, wakati huo tra wanamdai kodi kama 4b na satellite alikuwa anadaiwa, ndio maana Kuna kipindi hakuwa hewani kwenye ving'amuzi vyote
 
Back
Top Bottom