Wabunge, Waziri watunishiana misuli; Ni Kabaka, Jenista Mhagama, Mbilinyi (Sugu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge, Waziri watunishiana misuli; Ni Kabaka, Jenista Mhagama, Mbilinyi (Sugu)

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by nngu007, May 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  * Ni Kabaka, Jenista Mhagama, Mbilinyi (Sugu)
  * Wavutana katika kutembelea kiwanda
  * Kiwandani wabunge washuhudia ‘madudu’
  * Wafanyakazi wanalazimishwa kuvaa kaptura
  * Wabunge watokwa machozi kwa waliyoyaona


  Na Arodia Peter
  Dar es Salaam

  [​IMG]

  WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Gaudensia Kabaka jana alivutana vikali na wabunge wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii waliokuwa wanataka kutembelea Kiwanda cha Vyombo vya Nyumbani cha Jambo Plastiki kilichoko Dar es Salaam.

  Wakati wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa wamekwisha kujiandaa kwenda katika kiwanda hicho jana, ghafla Waziri Kabaka aliwaeleza kuwa ziara hiyo imeahirishwa hadi wakati mwingine.
  Kabaka alitoa sababu za kutaka kuahirisha ziara hiyo kuwa ni mgogoro wa wafanyakazi na mwajiri kiwandani hapo ambao upo mahakamani hivyo ziara hiyo itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.

  Baada ya kutolewa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jenista Mhagama alikuja juu na kumweleza Kabaka kuwa kamwe kamati yake haiwezi kuahirisha ziara hiyo bila kutolewa sababu za kuridhisha. Alisema kitendo alichokifanya Waziri kinadhalilisha kamati yake.

  “Mheshimiwa Waziri kitendo ulichokifanya unaingiza mgogoro mkubwa katika kamati ya Bunge… kwa mazingira ya sasa Watanzania hawana mahali popote pa kutolea shida zao zaidi ya bunge na hii inadhihirika wazi wataalamu wako hawakukushauri vizuri,” alisema Mbunge huyo wa Peramiho kwa tiketi ya CCM na kuongeza:

  “Basi kama ni hivyo, Mheshimiwa Waziri mimi nakupisha uwe mwenyekiti wa kamati ya Bunge maana naona hutaki kutuelewa.”

  Kuona hivyo, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alikwenda mbali zaidi kwa kusema kwa uzoefu uliopo nchini unaonyesha kuwa ziara hiyo tayari imekwicha kuchakachuliwa na wahusika kwa manufaa wanayoyajua wao.

  Alisisitiza kwamba kama ziara itaahirishwa basi yeye hatakuwamo kwenye orodha hiyo.

  Naye Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) alisema kama kamati haitaki kwenda kwenye kiwanda hicho yeye atapanga ziara yake kama mbunge wa Chadema na kwenda kusikiliza na kukagua mazingira kiwandani hapo.

  Asumpta Nshunju (CCM) ambaye ni Mbunge wa Nkenge, alisema kuna dalili za wazi watu wamepokea chochote kutoka kwa mwekezaji ndiyo maana kamati imepigwa ‘stop’ dakika za mwisho.

  Akimsaidia waziri wake, Ofisa Kazi Mfawidhi wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Josephat Rugakingira aliwaambia wabunge kwamba haingekuwa vizuri kutembelea kiwanda hicho wakati mgogoro kati ya menejimenti na wafanyakazi bado uko Baraza la Usuluhishi wa Migogogro (CMA) ikiwa imefunguliwa kesi namba DMA/DSM/ILALA/ 2009.

  Hata hivyo baada ya mvutano mkali hatimaye Waziri Kabaka alikubaliana na wabunge na kuamua kufanya ziara kiwandani hapo wakati huo ikiwa saa 7.00 mchana.

  Kiwandani
  Wabunge walipofika kiwandani walipangua ratiba iliyokuwa imeandaliwa iliyotaka wafanyakazi na menejimenti kukutana na kamati ya Bunge kwa pamoja.

  Kamati ya Bunge iliamua kukutana na wafanyakazi pekee, kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa moja. Waandishi wa habari wa menejimenti hawakuruhusiwa katika kikao hicho.

  Baada ya kumalizika kikao hicho, wabunge walitoka nje wakiwa wanafuta machozi na baadhi yao walisema waliingiwa na simanzi kubwa kutokana na mambo mazito waliyoelezwa katika kikao hicho.

  Hata hivyo, ilibainika kuwa katika kikao hicho ambacho Waziri pia alishiriki, kesi iliyokuwa inasemwa kuwa ipo mahakamani haikuwa kweli kwa vile ilikwisha kutolewa uamuzi tangu mwaka 2009.
  “Hii kama siyo rushwa ni nini, ndiyo maana walitaka kutuchakachua tusije hapa kwa maslahi yao, hii ni aibu. Wataalamu wa Wizara ndiyo wanaotufanya sisi wabunge wa CCM tuonekane hatuna thamani mbele ya umma… kumbe ni watu wachache waliojiwekea mtandao wa rushwa kwa njia wanazozijua wao,” alisema mmoja wa wabunge kwa sharti la kutotajwa jina.

  Waziri Kabaka akiri, aiomba radhi kamati
  Baadaye Waziri Kabaka aliomba radhi kwa Kamati ya Bunge kutokana na hali iliyojitokeza awali. Alisema yeye hakujua kama alichoambiwa na wataalamu wa Wizara yake kilikuwa ni uongo na uzushi.

  “Mheshimiwa mwenyekiti naomba radhi kwa yaliyotokea, nakiri nilidanganywa sasa nimejifunza kutoka kwenu,” alisema Kabaka kwa sauti ya upole.

  Alipoulizwa na waandishi wa habari ni hatua gani atawachukulia wataalamu waliomdang’anya, alisema:

  “Niachieni nitashughulika nao, tutaongea na wenzangu tuone ni kwa nini wamefanya hivyo”.

  Wafanyakazi wanalazimishwa kuvaa kaptura
  Kiwandani hapo wabunge walishuhudia wafanyakazi wakike na kiume wakiwa wamevaa kaptura na fulana ikiwa ndiyo sare za kiwanda hicho.

  Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wafanyakazi walisema hawaruhusiwi kuvaa nguo tofauti na hizo kiasi kwamba wakati wa baridi wanapata shidakubwa lakini hawana la kufanya.

  “Hizi ndiyo nguo zetu rasmi hapa kazini. Tukivaa tofauti na hizi tunafukuzwa kazi, tunashukuru mmekuja wabunge wetu mtutetee tunaangamia,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

  Kwenye mgahawa wa wafanyakazi, hali pia ni mbaya na wabunge walishuhudia uchafu uliokithiri huku vyombo vya kulia chakula vikiwa vya plastiki jambo ambalo ni hatari kwa afya za wafanyakazi hao.

  Baadhi ya wafanyakazi walisema licha ya kutumia vyombo vya plastiki pia wanalazimika kutumia vikombe kwa kupokezana kwa vile vilivyopo havitoshi.

  “Hata sisi tunaonekana kana mbwa, angalieni sehemu hii tunayolia chakula. Haifai hata kwa mnyama mbwa maana ni chafu kupindukia lakini hawatujali,” walisema baadhi ya wafanyakazi.

  Wafanyakazi wa kigeni
  Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Manoj Suchak aliulizwa kuhusu hatua ya kuajiri wafanyakazi wa kigeni katika nafasi zote za juu bila kuhusisha mfanyakazi mzawa hata mmoja.

  Akijibu swali hilo lililoulizwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM), alisema kati ya mameneja saba wa kiwanda hicho ni watano tu ambao ni wazawa.

  Hata hivyo Nkamia alipotaka amwone angalau mmoja ambaye ni mzawa, alitokea kijana mwenye asili ya Asia, jambo lililozua kicheko na miguno kutoka kwa wabunge.

  Ziara hiyo ya wabunge ilikuwa pamoja na mambo mengine kukagua mazingira ya kiwanda, kusikiliza mgogoro baina ya wafanyakazi na manejimenti ya kiwanda hicho ambao umedumu kwa muda mrefu.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,056
  Trophy Points: 280
  Baada ya kumalizika kikao hicho, wabunge walitoka nje wakiwa wanafuta machozi na baadhi yao walisema waliingiwa na simanzi kubwa kutokana na mambo mazito waliyoelezwa katika kikao hicho.

  Hata hivyo, ilibainika kuwa katika kikao hicho ambacho Waziri pia alishiriki, kesi iliyokuwa inasemwa kuwa ipo mahakamani haikuwa kweli kwa vile ilikwisha kutolewa uamuzi tangu mwaka 2009.

  "Hii kama siyo rushwa ni nini, ndiyo maana walitaka kutuchakachua tusije hapa kwa maslahi yao, hii ni aibu. Wataalamu wa Wizara ndiyo wanaotufanya sisi wabunge wa CCM tuonekane hatuna thamani mbele ya umma… kumbe ni watu wachache waliojiwekea mtandao wa rushwa kwa njia wanazozijua wao," alisema mmoja wa wabunge kwa sharti la kutotajwa jina.

  Mhhh! sijui walielezwa nini mpaka kimewatoa machozi! na kuingiwa na simanzi kubwa.
   
 3. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Kwa uongozi mmbovu uliopo hapa Tanzania hayo ni mambo ya kawaida sana kutokea na kutendeka waziwazi,huyo waziri Kabaka alishapokea rushwa ili asiende sema walimkaba sn koo ss kwa style hiyo maendeleo nchini mwetu yatabaki kama ndoto tu Tena za mchana
   
 4. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  mmmhmm...!!!!

  mimi napita tu...!!!
   
 5. n

  nyundo Senior Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2007
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama amepewa nafasi hiyo na kushindwa kuwatetea watanzania wenzake masikini na waliopigika aondoke na atakuja mwingine mwenye kujali watu. Kwanini viongozi wa aina hii bado wapo Tanzania? Na wanajiita viongozi wa umma? Umma gani wanaouongoza? Ameumbuka, amedhalilika, mbele ya wabunge na watanzania wote.
  Jk hatuna tena imani na kikaragosi wako huyu. Ameonyesha ni mla rushwa na ni mbabe, mtetea dhulma na muunga mkono ukandamizaji na msema uongo. Kama msamaha amewaomba wajumbe wa kamati, hajawaomba msamaha wafanya kazi hao wanaonyanyasika na kudhulumiwa ndani ya nchi yao, Naombeni muongozo jamani, kama waziri anasema uongo nichukue hatua gani?
   
 6. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This country!?
   
 7. n

  nyundo Senior Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2007
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi kama hawa ndio wanaoiletea ccm kuchukiwa na wananchi! Hongera jenista kwa kuepusha mgogoro, fikiria kamati isingeenda kiwandani, Chadema wangeenda pale, kitu ambacho kingetokea ni waziri kwa kutaka kuficha maovu yake angeagiza jeshi la polisi kuzuia chadema wasikutane na wafanyakazi! Vurugu ingeanza na watu wangeumia ama kufa, mwishowe magazeti yangeandika juu ya ukweli uliokuwa unafichwa, mwisho wake serikali ya ccm ingeonekana ndiyo chanzo, kumbe chanzo ni mpumbavu mmoja hivi ambaye ana maslahi binafsi na aliye tayari kuwaona wenzake wakiishi kama mbwa ili mradi yeye anpata maslahi binafsi.
  Nashangaa inakuaje kamati ya bunge isifanye kazi yake hadi waziri aamue? Huu ndio utawala bora unaotenganisha mihimili ya serikali, bunge na mahakama kufanya kazi kwa uhuru?
  Hongera sana Jenista kwa kushupalia na kuweza kufanikisha kufichua uovu huo, imani yako juu ya hilo umekufanya uonekane shujaa na mwishowe umeombwa samahani,
  Sugu pia big up, hiyo ndio kazi ya umma, jaribu pia kuwa makini na ukaribu na wabunge wa ccm ili upate support na upande huo kwa maslahi ya Taifa.
  Lusinde pia big up, lakini chunga kauli zako zisiwe za show off zikawa zinalenga kuchekesha sana, ila ukiwa na maana zinazotoka kwenye moyo ulioguswa basi tutasonga nawe. Kwani ukija kuzoeleka kuwa muongeaji sana itakuwa kama Mudhhir.
  Pigeni kazi ya umma, wote vijana nyinyi
   
 8. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Unajua mimi mambo ya kinafiki sipendi. Watanzania tunanyanyasika kwa ajili ya kitu gani jamani? Yaani hii habari imenichanganya ubongo, ukienda kwao unadhalilishwa, ukirudi nyumbani ni mara mia. Kwa nini tanzania tuteseke kama sisi ni masikini wa kutupwa. Hii inatokana na wasemaji wetu kutuona kama hatuna akili. Kama kuna kiongozi wananchi wanamjua ni mzembe, anadhalilisha watu afungiwe nje mpaka kikwete aende. Tuambizane ukweli hapo ndani palikuwa na nini mpaka wabunge kudondosha machozi si afadhali hicho kiwanda kifungwe?
   
 9. T

  Twasila JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Minister cheated! Nonsense. If the parliamentary committee can not be honoured, who will listen to the complaints of the poor workers? No wonder not the minister nor ps know their duties!! Aibu eh
   
 10. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tukilalamika utendaji mbovi wa mawaziri wa jakaya na ccm tunaambiwa nyie chadema haya sasa kwa uzoefu wangu sasa kamati za bunge ndizo zinazofanya kazi, je ni kwanini? Kuna wabunge wa chadema ndani ya hizo kamati angalia kamati ya nishati na madini j-makamba anaongea zaidi ya waziri mhusika...chama chetu cha mapindiziii cha bomoa nchi kikwete aaah.
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi kila kiongozi wa serikali yetu huwa anadanganywa tu? Wanashindwa kufanya kama mbayu wayu? Sijui nani hapa ni **** kati ya wananchi na viongozi!
   
 12. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tanzania tanzaniaaaaa nakupenda kwa moyi woteeee nnchiii yangu Tanzaniaaaa jina lako ni tamu saaaamaaa nilalapo nakuota wewe niamkapo ni heri mama weeeee......
   
 13. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Big up wanakamati, hilo suala lifike mbele lisiishie hapo tu.
   
Loading...