Wabunge Wazalendo Someni Hapa Muone Ufisadi Mwingine Kupitia GPSA

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Waheshimiwa Wabunge na hasa Wabunge Wazalendo,

Salaam na poleni na majukumu ya kujenga taifa letu.

UTANGULIZI:
Kama kichwa cha habari hii kinavyosomeka, leo hii nimeamua kuwaeleza japo kwa ufupi kuhusu ufisadi mwingine unaoweza kuliangamiza taifa hili kupitia manunuzi ya umma ya bidhaa zinazoitwa "common use items". Kama mnavyofahamu, kwa takriban miaka miwili sasa idara za serikali na mashirika ya umma yanalazimika kununua bidhaa mbalimbali kwa wazabuni waliopitishwa na Wakala wa Serikali wa Huduma za Manunuzi (GOVERNMENT PROCUREMENT SERVICES AGENCY - GPSA). Utaratibu huu ni mpya na ni utekelezaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya 2004 ambayo imefanyiwa marekebisho hivi karibuni kuruhusu ununuzi wa bidhaa za mitumba kama vile ndege, meli, gari moshi, n.k. Chini ya utaratibu huu mpya, Idara za Serikali na Mashirika ya Umma yanalazimika kupeleka mahitaji yao ya mwaka ya bidhaa mbalimbali kwa GPSA ili iendeshwe zabuni kwa nchi nzima ya kupata wazabuni wa kusambaza bidhaa. Baada ya zabuni kuendeshwa, makampuni huteuliwa kutoa huduma ya usambazaji bidhaa mbalimbali na kwa bei iliyopitishwa na GPSA. Makampuni hayo huingia mikataba na GPSA unaofahamika kama FRAMEWORK CONTRACT unaobainisha pamoja na mambo mengine bei za bidhaa (unit cost) na mahali pa kufikisha bidhaa hizo (delivery point).

UFISADI UNAVYOFANYIKA:
Katika mwaka huu wa fedha (2012/2013) idara za serikali na mashirika ya umma yametumiwa orodha ya makampuni ambayo yamepitishwa na GPSA kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa mbalimbali na bei zake. Kisheria, idara za serikali na mashirika ya umma hayaruhusiwi kununua bidhaa hizo nje ya makampuni hayo labda kama bidhaa inayohitajika haipo kwenye orodha ya GPSA. Kinachoshangaza na kusikitisha ni mambo mawili yafuatayo:-

Kwanza, makampuni mengi ni ya mifukoni (brief case companies). Hayana ofisi na yale yenye ofisi hayauzi bidhaa zilizopo kwenye orodha ya GPSA. Kwa mfano, kampuni moja inaweza kuwa kwenye orodha ya makapuni yanayouza bidhaa za ujenzi (building materials) lakini ukienda ofisini kwake utakutana na ubao wa hiyo kampuni umeegeshwa kwenye duka linalouza vifaa vya kuandikia (stationery). Ukihitaji bidhaa za ujenzi, mwenye kampuni atakutaka umpatie orodha ya bidhaa unazotaka halafu ataondoka kwenda kwenye maduka ya bidhaa za ujenzi kununua kwa bei ya chini na kisha kukuuzia kwa bei ya juu iliyopo kwenye Mkataba wa GPSA. Jambo hilo hufanyika waziwazi bila kificho. Nachojiuliza ni je, kampuni hiyo ilipata kazi na kuingia Mkataba na GPSA kwa vigezo vipi ikiwa hata ofisi tu haipo? Kama huu siyo ufisadi ni nini!? Kwa nini watu tusifikiri kwamba kampuni hizo ni za wakubwa.

Pili, bei za bidhaa zilizopitishwa na GPSA ni kubwa kubwa kubwa kupita kiasi. Hata kama Mkataba ni wa mwaka mzima, lakini bado bei ni kubwa sana na Idara za Serikali na Mashirika ya Umma yanalazimika kununua bidhaa kwa bei hizo hata kama zinaumiza. Kwa mfano, mimi binafsi nililazimika kununia bidhaa fulani kwa bei ya Sh. 80,000 wakati ambapo mwenye kampuni niliongozana nae na nikashuhudia akinunua bidhaa hiyohiyo kwa bei ya Sh. 45,000. Duka jingine lilikuwa linauza bidhaa hiyo hiyo kwa Sh. 45,500. Ilibidi nitumie Sh. 1,600,000 kwa kununua bidhaa 20 badala ya kutumia Sh. 900,000 kwa kununua bidhaa hiyo hiyo kwa idadi inayofanana. Hii ina maana kwamba endapo ningeshindanisha maduka zaidi ya matatu tofauti, kama ulivyokuwa utaratibu wa zamani, ningeweza kupata bei ya ushindani chini ya Sh. 45,000.

Ndugu zangu waheshimiwa wabunge, inawezekana lengo la utaratibu huu lilikuwa ni kupunguza mlolongo mrefu wa mchakato wa manunuzi ambao idara za serikali na mashirika ya umma yanalazimika kufuata wakati wa ununuzi wa bidhaa. Pamoja na lengo hilo zuri, nataka niwahakikishie kwamba utaratibu huu tayari umetumiwa vibaya na wakubwa na athari zake zipo wazi. Badala ya kuleta nafuu kwa wananchi. utaratibu wa "common use items" umeleta gharama na mzigo mkubwa kwa walipa kodi kwani bidhaa sasa zinanunuliwa mara mbili na hata zaidi ya bei ya kawaida. Hivi kweli inaingia akilini kwa kisingizio cha mkataba wa mwaka mzima eti kitu kinachouzwa kwa bei ya kawaida ya Sh. 45,000 kiuzwe kwa Sh. 80,000 na mbaya zaidi kampuni yenyewe iliyopewa zabuni hiyo haina hata ofisi na haijihusishi kabisa na uuzaji wa bidhaa hiyo!!! Kwa akili ya kawaida, kinachoonekana hapa huu ni Mradi wa wakubwa. Wameshinikiza utaratibu huu utumike kwa malengo ya kuingiza kampuni zao za brief case.

OMBI KWA WAHESHIMIWA WABUNGE:
Waheshimiwa wabunge, ninyi ndiyo sauti ya wananchi. Nimewaeleza jambo hili kwa lengo moja tu la kuwaomba mpige kelele na ikiwezekana iundwe tume itakayopitia orodha ya makampuni yaliyopitishwa na GPSA kwa mwaka huu wa fedha na kuona kama kweli ni makampuni halali yanayojohusisha na bidhaa husika na kama yana ofisi. Wakati wa zoezi hilo, tume ipitie hata bei ili ione uhalali wa bei ili ibainishe namna fedha za umma zinavyotumika vibaya.
 
Ni kweli mkuu, mimi niko idara ya ugavi kwenye taasisi ya umma. GPSA ni janga kwa ustawi wa taifa hili. Makampuni mengi makini hayapo GPSA. Kampuni nyingi zilizopo huko ni za mfukoni na ukiwapa kazi ni aibu tupu. Hawajui chochote. Kuna haja ya PPRA kufuatilia suala hilo kwani serikali inapoteza pesa nyingi sana.
 
sio siri kampuni nyingi zilizopitishwa na GPSA ni za mkononi ingawaje wazo la ununuzi kupitia GPSA ni zuri sana lakini wajanja wanataka kuturudisha enzi za utawala wa awamu ya tatu
 
Ni kweli mkuu, mimi niko idara ya ugavi kwenye taasisi ya umma. GPSA ni janga kwa ustawi wa taifa hili. Makampuni mengi makini hayapo GPSA. Kampuni nyingi zilizopo huko ni za mfukoni na ukiwapa kazi ni aibu tupu. Hawajui chochote. Kuna haja ya PPRA kufuatilia suala hilo kwani serikali inapoteza pesa nyingi sana.
mkuu si swala la PPRA tu hata mamlaka zinazotoa leseni nazo ni za kuwajibishwa kwa kutoa leseni kwa kampuni zisizokuwa na makazi
 
Suala la COMMON USE ITEMS ni janga jingine la kitaifa. Huu ni ufisadi mkubwa na kama alivyoswma mtoa mada Dumelambegu, nawaomba sana waheshimiwa wabunge walivalie njuga suala hili kabla halijaleta madhara makubwa zaidi. Kuna ndugu yangu yupo Mjini Shinyanga na anahusika moja kwa moja na shughuli za manunuzi ya umma. Anasema hivi karibuni amelazimika kununua saruji kwa bei ya Sh. 23,000 kwa mfuko mmoja wa kg 50 wakati bei ya kawaida ni Sh. 19,000. Eti hiyo ndiyo bei ya GPSA. Kinachosikitisha ni kwamba alilazimika kununua kwa kampuni inayouza stationery ambayo ndiyo imepewa Mkataba na GPSA. Kwa kuwa oda ilikuwa kubwa mwenye stationery aliomba punguzo na akauziwa Sh. 18,800 kwa kila mfuko na punguzo hilo lilitolewa na ndugu yangu akiwa palepale.

Kwa mwendo huu, nchi hii tutafika kweli!
 
Technically, hii ni vita ya ulaji. Ukweli ni kwamba, maafisa ununuzi inawawia vigumu kupata 10 percent chini ya utaratibu wa GPSA, maafisa ugavi wa GPSA ndio wanakula hizo 10 kwa sasa, kwa sababu wao ndio wanapitisha hao wazabuni. Kuhusu bei kuwa juu ni kweli, na hilo linatokana na hizo 10 wanazopata maafisa wa GPSA.
 
Technically, hii ni vita ya ulaji. Ukweli ni kwamba, maafisa ununuzi inawawia vigumu kupata 10 percent chini ya utaratibu wa GPSA, maafisa ugavi wa GPSA ndio wanakula hizo 10 kwa sasa, kwa sababu wao ndio wanapitisha hao wazabuni. Kuhusu bei kuwa juu ni kweli, na hilo linatokana na hizo 10 wanazopata maafisa wa GPSA.
Kama ndivyo, ashakumu si matusi tumeruka MKOJO tumekanyaga MAVI.
 
Mimi mbona kila cku nagombana na watu wa manunuzi? Bei ya GPSA ni mara2 ya bei iliyoko sokoni. Hivi kwanini tunakariri sheria za manunuzi bila kuangalia madhara yake? Nchi zilizoendelea hii sheria inafanya kazi vizuri coz system yao iko iko clear co kama huku kwetu. Kuna haja ya kuiondoa kabsa ili tuweke kwanza system imara.
 
Hii serikali mpka kinyaa, hivi utaratibu uliokuwa mwanzo ulikuwa na kasoro gani mpaka kuunda kampuni ambayo haina tija hii? ndo maana watu tumechoka na CCM wenyewe sijui hawayaoni haya ama tuseme walishalewa madaraka.
 
Asante sana Dume,

Ni wazalendo wachache kama ninyi mnaofanya moyo wa serikali hii iliyo mahtuti uendelee kutwita.
 
Tatizo ni tofauti ya muda wa malipo kati ya hizi bidhaa zinazonunuliwa na serikali na hao mnaosema wapo chini.

Serikali inachelewesha sana malipo na ndio maana supplier wengi huwa wanauza zaidi ili ile cha juu kifidie muda ambao hela yake imelala hapo serikalini kwa muda ambao hana uhakika atalipwa lini.

If we realy need a change, basi serikali kama malipo ni after 30 days of receipt of the invoice, basi na iwe hivyo maximum wakichelewa mwisho siku 31.

Ni utaratibu tu ndo unagomba hapo wala sio wizi wala nini. Kuhusu makampouni ya mifukoni, I think kuna watu tunawalipa kwa kodi zetu, nadhani wafanye tu kazi yao, wakishindwa tuwatoe tu mana tunawalipa kodi zetu bure.
 
Ufisadi kama huu unajulikana tangu kitambo ila tu nani wa kuchukua hatu, ndio ishu yenyewe.
Atleast haya mambo yanavyo'leak kwa jamaii wahusika wanaweza wakaona aibu na kuchukua hatua stahiki.
 
Tatizo la wabunge wetu hawafikiri kwa ndani zaidi wanapitisha tu. hiki kitu nikweli wala hakina kipingamizi ni ulaji hauna utofauti na magari ya umma kutafutiwa sehemu ya kwenda kufanyiwa maintenance kinachofanyika wanaiba vifaa vipya na kuweka vikuu kuu na baada ya hapo gari linakuwa mkweche bado jipya au la kila baada ya muda mfupi linahitaji maintenance tena kwa gharama ya juu sana
 
Technically, hii ni vita ya ulaji. Ukweli ni kwamba, maafisa ununuzi inawawia vigumu kupata 10 percent chini ya utaratibu wa GPSA, maafisa ugavi wa GPSA ndio wanakula hizo 10 kwa sasa, kwa sababu wao ndio wanapitisha hao wazabuni. Kuhusu bei kuwa juu ni kweli, na hilo linatokana na hizo 10 wanazopata maafisa wa GPSA.
Ukweli ni kwamba mfumo huu umerahisisha ulaji kwa maafisa ugavi. Kwa sababu hawalazimiki ku pick lowest supplier. ile difference ya bei halali upigwa pasu ili supplier awe selected. Kimsingi ni mfumo wa hovyo kuwahi kutokea. GPSA uwezo wao wa kuchambua zabuni ni mdogo sana hali inayosababisha kuchukua watu wa hovyo
 
Hii ndiyo shida ya kudesa kila kitu!nadhani mfumo huu watu wa gpsa wameudesa kutoka nchi fulani ya nje.shida ya kudesa ni kuwa huwezi kupatia kama muasisi mwenyewe. Daa! Ufisadi ktk hii nchi hadi kichwa kinaniuma!
 
Manunuzi ya umma ni janga tu hata kama si GPSA. wakati maafisa ugavi walipokuwa wananunua kwa kupitisha at leat three quotations pia kulikuwa na janga. Walikuwa wakimpatia mtu wao hizo quotations zote tatu na yeye kuzijaza zote yeye peke yake na kuomba mihuri kwa wenzake na kupiga ili kuonyesha kwamba ni washindani kumbe hakuna ushindani wowote. Utakuta kifaa cha shilingi 50,000.00 kinauzwa kwa laki moja. Kinachofanyika ni kwamba yeye anajaza laki moja, mwingine anamjazia laki moja na ishirini na wa tatu laki moja na hamsini. Ikifanya evaluation unamchukua the lowest priced bidder ambaye ame quote laki moja! Hakuna ushindani wowote uliokuwa unafanywa.

Inabidi mambo yote yaangaliwe kwa ujumla wake. Kila mahala watu wanapiga tu si GPSA ama maafisa ugavi yaani Procurement Officers.
 
Sijui mwenzetu Kagame anafanyeje huko Rwanda manake nasikia yeye hana tabia ya kukopi vitu kutoka kwa wazungu na kupesti kwake bila kuangalia kwanza kama anachotaka kukopi kitaendana na mazingira ya kwake.
 
hivi nbaa nao wanatumia gpsa maana nimeona tenda zote imepewa kampuni moja na wasiwasi mambo ya mhando wa tanesco yamehamia huko
 
hivi nbaa nao wanatumia gpsa maana nimeona tenda zote imepewa kampuni moja na wasiwasi mambo ya mhando wa tanesco yamehamia huko

NBAA ni taasisi ya umma. Kwa hiyo, nayo inalazimika kutumia makampuni yaliyopo kwenye orodha ya GPSA. Inakera sana na kwa kweli kama wabunge hawatalipigia kelele suala hili, hela za umma zitaishia mikononi mwa wajanja wenye vikampuni vya mifukoni tu. Makampuni ya maana yote hayamo kwenye orodha ya GPSA.
 
Back
Top Bottom