Nkundwe Sr
JF-Expert Member
- Nov 30, 2014
- 6,104
- 9,210
Dooh!! Nimecheka sana, kwa aina hii ya propaganda basi tutegemee kushindwa kwa mara nyingine tena kwenye huu uchaguzi.
Ni kweli watanzania sio wajinga mkuu, vitendo vya Chadema wanaviona wazi kabisa.
Mfano ukurupukaji walio ufanya kuondoka bungeni kwa kisingizio cha corona. Watu makini hawawezi kufanya hivi.
Tunamuona leo mch Msigwa anakili na kuomba radhi kuwa alimsingizia Kinana tuhuma za ujangili kwa masilahi yake kisiasa, watanzania wanaona hayo na mengine mengi.
Huoni kama mambo kama haya ndio yanawaua kisiasa mkuu leo Msigwa atamuamini kwa uzushi kama huu?.
Mimi narudia tena kukwambia kuwa huu sio wakati wa kutupia lawama ccm bali ni wakati wa kiimarisha hiki Chama pendwa mkuu, lawama sio suluhisho.
Wewe una ushahidi gani kuwa hawa viongozi wananunuliwa mkuu??
Uje na ushahidi usije hapa kunambia eti kisa mh Mbowe hakualikwa Ikulu.
Umesema humtafanya uchaguzi wowote chini ya Rais Magufuli??
Hili nalo kosa lingine, kususia uchaguzi sio gia ya kuvuna wanachama bali ndio kuzidi kukiua chama.
Hujuma za kisiasa zipo hata Chadema wanafanya hivyo kwa vyama vingine, ila sio kila kinachofanyika ama mgogoro unao tokea Chadema basi useme ni hujuma mkuu.
Malalamiko ya viongozi wanao hama tunayaona na kama ni ya uongo mbona hoja zao hazijibiwi??
Tuhuma ya bil 8 mbona hazijibiwi??
Kukata mishahara ya wabunge mbona hazijibiwi.?
Mmetukana Lijuakali alipoibua matumizi mabaya fedha na maovu kadhaa ya Mbowe. Leo unawasakama akina mama, wazazi wetu. Mtu mxima hovyo.Wanaohamama ni wanasiasa kwa masilahi yao binafsi sio wananchi na wananchi ndio nguvu ya chama na ndio wapiga kura hivyo wahame tu sisi tunachohitaji ni Tume Huru ya Uchaguzi tu.
Wanamchafua Mbowe ili kutengeneza uhalali wa hawa kuhamia NCCR kwa faida ya CCM wanasahau wananchi tuna akili na kuelewa mchezo huu mchafu wa kisiasa unaoendelea.
CCM hii kwa miaka mitano imepuuza watu na maendeleo yao na badala yake imekumbatia maendeleo ya vitu kwa gharama ya watu hivyo hakina support ya umma kwani wamefanya maisha ya watu na maendeleo yao kurudi nyuma na kwa kujua ukweli huu, ndio maana sasa wanatumia nguvu kubwa kutaka kuua upinzani wanasahau upinzani ni matokeo ya wao waliopewa dhaman kushindwa ku-deliver.
Kama wanabisha na wanaamini wanakubalika,wakubali tume huru ya uchaguzi.
Waacheni waendelee na mchezo wao ila wakati unakuja watakuja kujua walikuwa wanatwanga maji kwenye kinu.
Mmetukana Lijuakali alipoibua matumizi mabaya fedha na maovu kadhaa ya Mbowe. Leo unawasakama akina mama, wazazi wetu. Mtu mxima hovyo.
Sikiliza kilio chao.
Wafia CHADEMA wanajitahidi kuuzima huo moto na Petrol.......Ufipa hali siyo shwari, nyumba inaungua moto hiyo.
Wananchi ni Seti kubwa sana ikiwamo pamoja na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA wa kiti cha urais mwaka 2015.Wananchi tuwaweke alama hawa wote waliofanya hama hama. Dawa yao tunawakataa kwa kishindo kikubwa, wasubiri mbeleko na mbeleko ni miaka mitano tu, wangebaki katika vyama vyao vya awali hata kama ungefanyika ubabe october baada ya miaka mitano wangeweza kurudi na kuendelea kupeta.
Hizi tabia zao za kutokukomaa walizozionesha zinatengeneza kupuuzwa, tena vijana ndio wakuwasikitikia zaidi kwasababu wangevumilia kukosa kwa miaka mitano tu mingine wangerudi kwa nguvu na kasi ya ajabu na wangebaki kwa muda mrefu kwenye viti.
Asisahau kumchukua Lisu waende naye pamoja.Hata Mbowe naye aende huko huko...
Kumbe mnashindana? Sasa kipi kitawatofautisha?Tukikuwekea orodha ya upande Wa pili hapa unaweza kimbia ndugu(CCM), wanasiasa wasikie tu hatari
Ila wamechelewa aisee eti baada ya Bunge kuhitimishwa...sio vizuri waje ata leo bhana.Viti maalumu wote wanahama chadema baada ya kutumikishwa sana na mbowe na genge lake
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi tangu 2015 mpaka awakujua makosa ya Ufipa?Awa ni walaghai tuChadema kulikoni!?, hili sio la kufumbia macho hili uongozi wa chama ipo haja sasa ya kujitafakari, suala la kusema kuwa hawa watu wananunuliwa naona kwasasa halina mashiko inatakiwa wajitafakari kama chama wajue tatizo liko wapi kisha wafanye marekebisho makubwa kwa masilahi ya chama na watanzania kwa ujumla wenye imani na hiki chama.
Ndio munavyo jidanganya hivyo.Wamehamia CCM B kwa ufadhili wa CCM!!
Wafia CHADEMA wanajitahidi kuuzima huo moto na Petrol.......
Kama unalijua hilo mbona yanakutoka mapovu kibao?Wacha kife tu.
Alikua CUF nae alipita itakua hiyo sacos ya mtu mmoja?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi tangu 2015 mpaka awakujua makosa ya Ufipa?Awa ni walaghai tu