Wabunge wawili wa Viti Maalum CHADEMA wahamia NCCR Mageuzi

Huna akili
Kwa hiyo huyo Makene naye alimpitia huyo mama ndio akapata ubunge!!?? Upinzani ktk nchi hii bado kuna safari ndefu. Hizi tuhuma na kukurupuka za kusajili wasaliti ndio zinaharibu chama. Itachukua miaka mingi sana kwa upinzani TZ kuimarika kama wataendelea kufanya upuuzi huu unaoendelea..
1. Matumizi mabaya ya pesa za michango ya wabunge
2. Rushwa ya ngono (viti maalumu)
3. Hakuna ofisi yake
4. Matumizi mabaya ya ruzuku
5. Ukabila
6. Kusajili na kuwapa nafasi mamluki

In God we Trust
 
Dar code ..wanawake kama hao kula kisamvu mapema... hawawezi kutapika kama hivi
 
Mkuu Dr Slaa,Zitto, Wangwe walikuwa na support zaidi ya 50% ya wanachama ila kulikua na madhara yeyote 2015?

CHADEMA wakisimamisha mgombea mzuri wa Urais walau apate kura million 2 pekee hayo ni majimbo walau 15 na viti maalum 20+ basi KUB itaendelea kuwa chini ya CHADEMA.

Siasa ni numbers sio viongozi, CUF aliondoka Lipumba 2015 ila kikaongeza kura sababu alihama Mtu sio wanachama.

Sasa nikuhakikishie chadema wamehama viongozi tu ila wanachama bado wapi loyal.
Kweli mikutano sio kipimo lakini ukiweza pata turnout kubwa walau inakupa fursa ya kuuza sera zako kuliko upuuzwe kabisa.

Hoja yangu ni HII: Wanahama sababu wanahofu CCM itachukua viti vyote kma kule zenji na serikali za mitaa ila sio kwamba Mbowe ndio shida. Mbowe ameshaitwa dikteta na mla ruzuku toka Silinde anasoma chuo bado ila leo ndio wamegundua, wiki chache kabla bunge halijavunjwa?

Hapana mimi ni wa mwisho kuamini Mbowe ndio chanzo. Hata 2015 kuna wengi tu hawakumtaka Lowassa ila kwakuwa walijua atasaidia washinde majimbo walikaa kimya. So hakunaga mwanasiasa eti anasimamia ukweli bali maslahi tu.
Ndoto za usiku for 2020! Let’s keep waiting!
 
Wabunge Joyce Sokombi na Sussane Masele (CHADEMA-VITI MAALUM) wametangaza kuhama CHADEMA na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sussane Masele ni mke wa ndoa wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA anayeitwa Tumaini Makene

=====
Wabunge Suzana Maselle (Mwanza) na Joyce Sokombi (Mara) wametangaza kuondoka CHADEMA mara baada ya kumaliza kipindi chao cha Ubunge, Juni mwaka huu

Wamesema, uamuzi wao wa kuondoka CHADEMA umetokana na chama hicho kutawaliwa na ubinafsi, matumizi mabaya ya rasimali za chama na ubabe wa kiongozi Mkuu wa chama hicho

Wamedai kuwa, “hali hii imekuwa mbaya zaidi baada ya Esther Bulaya, kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi yetu na kujipa mamlaka yaliyopitiliza

Maselle amesema “Kabla ya hapo, palikuwepo na kafursa kakuulizwa na kujipendekeza. Wakati huu, ni amri tu. Kwa kifupi, maamuzi mengi ni ya kibabe na yenye kudharau watu wengine na kwa bahati mbaya Kiongozi Mkuu wa chama na ambaye pia ni KUB haonyeshi kuchukua hatua kurekebisha hali hii"

Kuhusu suala la kutoingia Bungeni, wabunge hao wawili wamesema, “suala la kutoingia Bungeni kwa siku 14 lilianzishwa na Esther Bulaya, ambaye kwa sasa inawezekana ndiye Mshauri Mkuu wa Freeman Mbowe kwa mambo ya chama na Bunge"

Wameeleza “Kwamba, mheshimiwa Bulaya ndiye aliyeanza kutoa maelekezo kwa Wabunge kuwa wasiingie Bungeni kwa siku 14, lakini Wabunge wakahoji mamlaka ya kufanya hivyo ameyatoa wapi?

Aidha, “Baadhi ya Wabunge akiwamo wale waandamizi kabisa, wakataka kiitishwe kikao cha Kambi ya Upinzani ili tuweze kujadili jambo hilo kwa mapana kwa kuweka bayana hasara na faida zake”

Amesema, sisi Wabunge wa Chadema tulikuwa tunachanga Tsh. 1,560,000 kwa Wabunge wa Viti Maalum kila mmoja na Sh. 520,000 kwa Mbunge wa jimbo kila mwezi

“Hapa hoja siyo kuchanga, kwanza ni takwa la kikatiba, hoja ni jinsi fedha hizo za michango ambayo tuliambiwa zitatumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jinsi zilivyotumika nje ya mipango iliyokusudiwa, na bila idhini ya vikao vyenye mamlaka hiyo"

View attachment 1456596
Kwani uchaguzi mkuu ujao umeshapita?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema kulikoni!?, hili sio la kufumbia macho hili uongozi wa chama ipo haja sasa ya kujitafakari, suala la kusema kuwa hawa watu wananunuliwa naona kwasasa halina mashiko inatakiwa wajitafakari kama chama wajue tatizo liko wapi kisha wafanye marekebisho makubwa kwa masilahi ya chama na watanzania kwa ujumla wenye imani na hiki chama.
Bado una imani na wanasiasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka Akili zimkae sawa DJ Mbowe endapo anadhani wanachama wake wananunuliwa bila kutafakari atabaki Yeye na Hilda
 
Chadema kulikoni!?, hili sio la kufumbia macho hili uongozi wa chama ipo haja sasa ya kujitafakari, suala la kusema kuwa hawa watu wananunuliwa naona kwasasa halina mashiko inatakiwa wajitafakari kama chama wajue tatizo liko wapi kisha wafanye marekebisho makubwa kwa masilahi ya chama na watanzania kwa ujumla wenye imani na hiki chama.
Swadakta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri ni kwamba Mungu hatamuacha mbowe mpweke na mkiwa na atazidi kumuimarisha USALITI una malipo siku zote ni swala la muda mbowe kamanda kuwa na moyo mkuu wewe pamoja na wote mtakaosimama imara wengi wtanzania wengi wanawaunga mkono jasho na damu vilivyomwagika kwa kuijenga chadema havita potea bure.
 
Pia inanifundisha kwamba watanzania sio watu wa kuwaamini maana viongozi ndio taswira ya sisi wengine Kama taifa haiwezekani Mambo ambayo chadema wamefanyiwa mpaka kuuwawa Leo hii unaenda kwa mtesi wako haiwezekani kabisa hata ile kanuni ya Kama huwezi shindana nao ungana nao sidhani Kama inafaa hapa.
 
Uvccm shtukeni Hawa hamahama wako kimaslahi msifurahie kuhama kwao mkidhani mnaibomoa chadema ukweli ni kwamba wanakuja kuchukua nafasi zenu za ubunge na ukuu wa wilaya nyie mtàachwa yetu macho.
 
Kimsingi jwtz inatakiwa iangalie huu mchezo wa USALITI maana kiongozi hatakiwi awe hivi Sasa jeshi linapoajiri vijana wetu lijue pia tabia asili ya watanzania ni USALITI na majeshini USALITI hautakiwi.
 
Wabunge Joyce Sokombi na Sussane Masele (CHADEMA-VITI MAALUM) wametangaza kuhama CHADEMA na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sussane Masele ni mke wa ndoa wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA anayeitwa Tumaini Makene

=====
Wabunge Suzana Maselle (Mwanza) na Joyce Sokombi (Mara) wametangaza kuondoka CHADEMA mara baada ya kumaliza kipindi chao cha Ubunge, Juni mwaka huu

Wamesema, uamuzi wao wa kuondoka CHADEMA umetokana na chama hicho kutawaliwa na ubinafsi, matumizi mabaya ya rasimali za chama na ubabe wa kiongozi Mkuu wa chama hicho

Wamedai kuwa, “hali hii imekuwa mbaya zaidi baada ya Esther Bulaya, kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi yetu na kujipa mamlaka yaliyopitiliza

Maselle amesema “Kabla ya hapo, palikuwepo na kafursa kakuulizwa na kujipendekeza. Wakati huu, ni amri tu. Kwa kifupi, maamuzi mengi ni ya kibabe na yenye kudharau watu wengine na kwa bahati mbaya Kiongozi Mkuu wa chama na ambaye pia ni KUB haonyeshi kuchukua hatua kurekebisha hali hii"

Kuhusu suala la kutoingia Bungeni, wabunge hao wawili wamesema, “suala la kutoingia Bungeni kwa siku 14 lilianzishwa na Esther Bulaya, ambaye kwa sasa inawezekana ndiye Mshauri Mkuu wa Freeman Mbowe kwa mambo ya chama na Bunge"

Wameeleza “Kwamba, mheshimiwa Bulaya ndiye aliyeanza kutoa maelekezo kwa Wabunge kuwa wasiingie Bungeni kwa siku 14, lakini Wabunge wakahoji mamlaka ya kufanya hivyo ameyatoa wapi?

Aidha, “Baadhi ya Wabunge akiwamo wale waandamizi kabisa, wakataka kiitishwe kikao cha Kambi ya Upinzani ili tuweze kujadili jambo hilo kwa mapana kwa kuweka bayana hasara na faida zake”

Amesema, sisi Wabunge wa Chadema tulikuwa tunachanga Tsh. 1,560,000 kwa Wabunge wa Viti Maalum kila mmoja na Sh. 520,000 kwa Mbunge wa jimbo kila mwezi

“Hapa hoja siyo kuchanga, kwanza ni takwa la kikatiba, hoja ni jinsi fedha hizo za michango ambayo tuliambiwa zitatumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jinsi zilivyotumika nje ya mipango iliyokusudiwa, na bila idhini ya vikao vyenye mamlaka hiyo"

View attachment 1456596
Huyo Esther Bulaya muda so mrefu nae anaunga juhudi! Stay tuned!
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom