News Alert: Wabunge wawili wa Viti Maalum CHADEMA wahamia NCCR Mageuzi

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,354
2,000
Hata Mbowe naye aende huko huko ila furaha ni kuwa hawajaenda rasmi ccm. Huko ni mbinu tu za kubadili majina ili waweze kuja huku kuomba kula
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
29,083
2,000
Dooh!! Nimecheka sana, kwa aina hii ya propaganda basi tutegemee kushindwa kwa mara nyingine tena kwenye huu uchaguzi.

Ni kweli watanzania sio wajinga mkuu, vitendo vya Chadema wanaviona wazi kabisa.
Mfano ukurupukaji walio ufanya kuondoka bungeni kwa kisingizio cha corona. Watu makini hawawezi kufanya hivi.

Tunamuona leo mch Msigwa anakili na kuomba radhi kuwa alimsingizia Kinana tuhuma za ujangili kwa masilahi yake kisiasa, watanzania wanaona hayo na mengine mengi.

Huoni kama mambo kama haya ndio yanawaua kisiasa mkuu leo Msigwa atamuamini kwa uzushi kama huu?.

Mimi narudia tena kukwambia kuwa huu sio wakati wa kutupia lawama ccm bali ni wakati wa kiimarisha hiki Chama pendwa mkuu, lawama sio suluhisho.

Wewe una ushahidi gani kuwa hawa viongozi wananunuliwa mkuu??
Uje na ushahidi usije hapa kunambia eti kisa mh Mbowe hakualikwa Ikulu.

Umesema humtafanya uchaguzi wowote chini ya Rais Magufuli??
Hili nalo kosa lingine, kususia uchaguzi sio gia ya kuvuna wanachama bali ndio kuzidi kukiua chama.

Hujuma za kisiasa zipo hata Chadema wanafanya hivyo kwa vyama vingine, ila sio kila kinachofanyika ama mgogoro unao tokea Chadema basi useme ni hujuma mkuu.

Malalamiko ya viongozi wanao hama tunayaona na kama ni ya uongo mbona hoja zao hazijibiwi??

Tuhuma ya bil 8 mbona hazijibiwi??

Kukata mishahara ya wabunge mbona hazijibiwi.?
Tutegemee kushindwa kwani kuna ushindani au matumizi mabaya ya madaraka? Wananchi mbona tumeshaamka muda mrefu, ila hatuna muda wa kushiriki siasa za kishamba. Msigwa wa cdm, kama ana mambo yake yanamuhusu yeye. Kwani ni hayo ya Msigwa ndio yatainyima kura cdm, basi ccm isingekuwepo hata hii leo.

Siitupi lawama ccm bali nakuambia kwa sasa hamna siasa, bali kuna matumizi mabaya ya madaraka ndani ya siasa. Hatuhitaji kushiriki uchaguzi ambao anayetangazwa anatangazwa bila ridhaa ya wananchi, huku wapiga kura wa upinzani wakiachwa na vilema. Kuna njia nyingi za kupata viongozi na wali sio lazima hiyo njia ya kura, kwani hata ccm hawako hapo kutokana na kura.

Malalamiko yanaeleweka na sio hizo swagga za kuhama chama baada ya kuhongwa na kuahidiwa vyeo vya mteremko. Malalamiko yana sehemu husika ndani ya chama,nje ya vikao vya chama ni utapeli kama utapeli mwingine.
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,865
2,000
Wanaohamama ni wanasiasa kwa masilahi yao binafsi sio wananchi na wananchi ndio nguvu ya chama na ndio wapiga kura hivyo wahame tu sisi tunachohitaji ni Tume Huru ya Uchaguzi tu.

Wanamchafua Mbowe ili kutengeneza uhalali wa hawa kuhamia NCCR kwa faida ya CCM wanasahau wananchi tuna akili na kuelewa mchezo huu mchafu wa kisiasa unaoendelea.

CCM hii kwa miaka mitano imepuuza watu na maendeleo yao na badala yake imekumbatia maendeleo ya vitu kwa gharama ya watu hivyo hakina support ya umma kwani wamefanya maisha ya watu na maendeleo yao kurudi nyuma na kwa kujua ukweli huu, ndio maana sasa wanatumia nguvu kubwa kutaka kuua upinzani wanasahau upinzani ni matokeo ya wao waliopewa dhaman kushindwa ku-deliver.

Kama wanabisha na wanaamini wanakubalika,wakubali tume huru ya uchaguzi.

Waacheni waendelee na mchezo wao ila wakati unakuja watakuja kujua walikuwa wanatwanga maji kwenye kinu.
Mmetukana Lijuakali alipoibua matumizi mabaya fedha na maovu kadhaa ya Mbowe. Leo unawasakama akina mama, wazazi wetu. Mtu mxima hovyo.

Sikiliza kilio chao.

 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
86,522
2,000
Bring back our 1.5trillion
Mmetukana Lijuakali alipoibua matumizi mabaya fedha na maovu kadhaa ya Mbowe. Leo unawasakama akina mama, wazazi wetu. Mtu mxima hovyo.

Sikiliza kilio chao.

In God we Trust
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,980
2,000
Mojawapo wa sababu ambazo wamezitoa ni upendeleo uliokithiri CHADEMA kiasi cha kwamba walikuwa hawapewi nafasi za kuchangia Bungeni. Kwa vile wao hawakujikarantini kama wenzao ilikuwa nafasi muafaka wa kuonyesha uwezo wao wa kuchangia kwa hoja. Mbona hawakufanya hivyo? Kinachosikitisha ni kuwa wale waliochangia walionyesha wazi kuwa hawana uwezo wa kutimiza wajibu wao wa kuisimamia serikali na kutetea maslahi ya waliowatuma.

Amandla...
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
8,976
2,000
Wananchi tuwaweke alama hawa wote waliofanya hama hama. Dawa yao tunawakataa kwa kishindo kikubwa, wasubiri mbeleko na mbeleko ni miaka mitano tu, wangebaki katika vyama vyao vya awali hata kama ungefanyika ubabe october baada ya miaka mitano wangeweza kurudi na kuendelea kupeta.

Hizi tabia zao za kutokukomaa walizozionesha zinatengeneza kupuuzwa, tena vijana ndio wakuwasikitikia zaidi kwasababu wangevumilia kukosa kwa miaka mitano tu mingine wangerudi kwa nguvu na kasi ya ajabu na wangebaki kwa muda mrefu kwenye viti.
Wananchi ni Seti kubwa sana ikiwamo pamoja na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA wa kiti cha urais mwaka 2015.
 

Maige S Chagu

Senior Member
Sep 22, 2018
113
250
Wamekataa udikteta wa mbowe,ukatwe 30% ya mshahara kila mwezi halafu mtu fulani tu akatumbue hiyo hela ng'ambo.Utakuwa na akili timamu?Bora wasepe tu na hao waliobaki wamebaki kufanya nini?Ngoja jumba bovu liwaangukia October 2020 siyo mbali na ndio utakuwa mwisho wa siasa za kilaghai.
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,026
2,000
Chadema kulikoni!?, hili sio la kufumbia macho hili uongozi wa chama ipo haja sasa ya kujitafakari, suala la kusema kuwa hawa watu wananunuliwa naona kwasasa halina mashiko inatakiwa wajitafakari kama chama wajue tatizo liko wapi kisha wafanye marekebisho makubwa kwa masilahi ya chama na watanzania kwa ujumla wenye imani na hiki chama.
Hivi tangu 2015 mpaka awakujua makosa ya Ufipa?Awa ni walaghai tu
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
86,522
2,000
Kama kuungua nyumba ya cdm haikuanza leo, labda mtu mjinga tu ndiyo anaweza kuona kuwa yanayo tokea hii leo ni mapya kisiasa hasa kipindi cha kuelekea uchaguzi.

Kama mwenyekiti wa ccm alitangaza wazi wazi kuwa atahakikisha upinzani unakufa kabla ya mwaka 2020 wewe kajamba nani unashangaa kitu gani?
Wafia CHADEMA wanajitahidi kuuzima huo moto na Petrol.......
In God we Trust
 
Top Bottom