Wabunge wawili wa Viti Maalum CHADEMA wahamia NCCR Mageuzi

Chadema kulikoni!?, hili sio la kufumbia macho hili uongozi wa chama ipo haja sasa ya kujitafakari, suala la kusema kuwa hawa watu wananunuliwa naona kwasasa halina mashiko inatakiwa wajitafakari kama chama wajue tatizo liko wapi kisha wafanye marekebisho makubwa kwa masilahi ya chama na watanzania kwa ujumla wenye imani na hiki chama.
Utaelewa wakati nccr watakapoamua kutokuweka mgombea wa Urais.
 
Mkuu kwanza naomba tuwe wakweli hapa kuwa mafanikio ya Chadema kwenye ushindi wa majimbo mengi na kura nyingi 2015 haikuwa nguvu binafsi ya Chadema pekee.

UKAWA ulichangia sana tena kwa kiasi kikubwa sana.

Pili ni ukweli ulio wazi kuwa mafanikio yale yalikuwa na nguvu kubwa ya kundi la wana ccm waliokuwa nyuma ya Lowasa.
Kwa hali ilivyo sasa jinsi Chadema inavyo suasua usitegemee wimbi kubwa la kura nyingi kama 2015 hilo halipo kabisa mkuu.

Mimi nitaendelea kuamini kuwa wanahama chama hiki kwasababu wanajua muelekeo mbovu wa Chama, kukosekana kwa maamuzi sahihi kwenye mambo ya msingi, mfano huu uamuzi wa hivi karibuni kuondoka bungeni kwasababu ya Covid-19,sera mbovu za Chama, kutokuwepo kwa maelewano ndani ya Chama n.k.

Sababu si hizo unazosema wewe mkuu, hii hoja ya kuwa eti uchaguzi utakuwa wa figisu, hapo ni kutaka tu kuhalalisha tu madhaifu ya Chadema kwa kivuli cha ccm.

Mimi nadhani Chadema wakae wafanye reform kwenye mifumo yao hili ndio la msingi na si kutupa lawama kwa ccm.
Usijichanganye, wanaoyumba ni wasaliti na wanaogopa mawimbi Wananchi wako imara wanajua wanachokitaka na hawatatishika kama ambavyo ungependa. UTAONA
 
Na ndo ujinga waliofanya mke wa makene mbunge wa viti maalumu, sijui Saidi kubenea mke wake mbunge huo ka si favoratism ni kitu gani. Wakati kulikuwa na watu Bora kuliko hao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati Zitto yuko CDM, marehemu mama yake alipewa viti maalum, Marehemu dada yake Tundu Lissu pia alipewa viti maalum 2015, kuna yule demu nyumba ndogo wa Mbowe aliyemzalia watoto wawili naye yumo viti maalum, etc etc etc.
Viti vyao maalum huwa wanavgezo vyao private vya kuvitoa.

Kwa nafasi ya Mdee, hata Bulaya atapewa viti maalum 2020 asipotoboa Bunda.
 
Chama Ni itikadi, unabadilishaje itikadi kama nguo? Siasa inafanywa kama biashara. Anyway kikatiba wanasema Ni haki yao
 
Wakati Zitto yuko CDM, marehemu mama yake alipewa viti maalum, Marehemu dada yake Tundu Lissu pia alipewa viti maalum 2015, kuna yule demu nyumba ndogo wa Mbowe aliyemzalia watoto wawili naye yumo viti maalum, etc etc etc.
Viti vyao maalum huwa wanavgezo vyao private vya kuvitoa.

Kwa nafasi ya Mdee, hata Bulaya atapewa viti maalum 2020 asipotoboa Bunda.
Kiujumla Viti maalumu vingefutwa, vyama vyote wanavitumia visivyo sio ccm wala upinzani.usipojulikana hupewi.Ccm Na chadema tuhuma za kingono Ni kubwa sana.Tukiweka hapa hatari
 
Wakati wa nyuma malalamiko yalikuwa ni kuibiwa kura jambo ambalo ni kweli, lakini kwa sasa sio wizi wa kura tena, bali ni kuagiza tume kumtangaza mgombea wa ccm bila kujali matokeo ya kura, kisha vyombo vya dola kutumia nguvu kulinda mshindi haramu. Kwa taarifa yako hakuna chama kisicho na mapungufu, ila hii trend ya kuhama sasa haitokani na huo udhaifu wa chama, bali ni nguvu ya ziada iliyo nje ya sababu za kisiasa.

Haya yanayoendelea kwenye hiki chama ni kweli tunayaona ila tunajua fika ni hujuma za wazi ili kuiua cdm. Wananchi wengi tuna uelewa mkubwa sana, usidhani tumelala na tunaweza kudanganyika na propaganda mfu za ccm. Lengo hasa la kuwanunua na kuwalaghai hao viongozi wa cdm ni ili kuharibu haiba ya cdm, ili kuweka uhalali wa hujuma zinazotaka kufanywa kwenye uchaguzi, lengo likiwa ni kuhadaa umma kuwa ccm inakubalika na cdm haikubaliki ndio maana imeshindwa. Na sisi kwa kulitambua hilo, ndio maana hatuko tayari kushiriki kwenye uchaguzi wowote chini ya Magufuli bila tume huru ya uchaguzi. Tuko tayari wahame viongozi wote wa cdm, lakini kuwepo na tume huru uchaguzi kisha uje uchukue mrejesho. Kizazi hiki sio cha ccm, ndio maana unaona hujuma za wazi dhidi ya cdm ili kukibakisha madarakani hicho chama za wazee. Kwa sasa hivi kuna kundi la wanaccm wamemwagwa humu mitandaoni ili kuteka ufahamu wa wanacdm, lakini wanacdm ni next level.
Dooh!! Nimecheka sana, kwa aina hii ya propaganda basi tutegemee kushindwa kwa mara nyingine tena kwenye huu uchaguzi.

Ni kweli watanzania sio wajinga mkuu, vitendo vya Chadema wanaviona wazi kabisa.
Mfano ukurupukaji walio ufanya kuondoka bungeni kwa kisingizio cha corona. Watu makini hawawezi kufanya hivi.

Tunamuona leo mch Msigwa anakili na kuomba radhi kuwa alimsingizia Kinana tuhuma za ujangili kwa masilahi yake kisiasa, watanzania wanaona hayo na mengine mengi.

Huoni kama mambo kama haya ndio yanawaua kisiasa mkuu leo Msigwa atamuamini kwa uzushi kama huu?.

Mimi narudia tena kukwambia kuwa huu sio wakati wa kutupia lawama ccm bali ni wakati wa kiimarisha hiki Chama pendwa mkuu, lawama sio suluhisho.

Wewe una ushahidi gani kuwa hawa viongozi wananunuliwa mkuu??
Uje na ushahidi usije hapa kunambia eti kisa mh Mbowe hakualikwa Ikulu.

Umesema humtafanya uchaguzi wowote chini ya Rais Magufuli??
Hili nalo kosa lingine, kususia uchaguzi sio gia ya kuvuna wanachama bali ndio kuzidi kukiua chama.

Hujuma za kisiasa zipo hata Chadema wanafanya hivyo kwa vyama vingine, ila sio kila kinachofanyika ama mgogoro unao tokea Chadema basi useme ni hujuma mkuu.

Malalamiko ya viongozi wanao hama tunayaona na kama ni ya uongo mbona hoja zao hazijibiwi??

Tuhuma ya bil 8 mbona hazijibiwi??

Kukata mishahara ya wabunge mbona hazijibiwi.?
 
Duh! Nepotism

Kumbe ndio maana sababu ya kutishia kumfukuza dogo Lijualikali CDM kaoa nje ya chama.

Dj zero na Mukya.

Mdee na Esther.

Makene na Masele.

Diwani wa sombetini na mkewe viti maalumu(jina nimesahau)

Mwaalimu na Matiko(walizaa tu) sina uhakika kama wanaendelea.

Mrema na mbunge wa viti maalum(jina nimesahau)

Lissu na viti maalum(marehemu dada yake)

Ndio tuwape nchi.
Tukikuwekea orodha ya upande Wa pili hapa unaweza kimbia ndugu(CCM), wanasiasa wasikie tu hatari
 
Uzuri ni kuwa ukitaka kupika wali kuna chuya huwa ukiweka maji tu zinajitoa zenyewe, karibuni jikoni.

Huyu dada Sussane hawezi hata kusoma kilichoandikwa, anasoma kama mtoto wa darasa la 3. Jamani CHADEMA mnapochagua wawakilishi muwe mnaangalia viwango. Makosa ya CHADEMA wenyewe, kwani hata hawa akina dada walichaguliwa kwa upendeleo. Na haya ndio matokeo yake.

Anadai hawakupewa nafasi ya kuchangia bungeni, hivi huyu dada atachangia nini katika bunge hili ngangali. Bora watoke tu, na nawatakia mema huko NCCR mageuzi.
 
Wananchi tuwaweke alama hawa wote waliofanya hama hama. Dawa yao tunawakataa kwa kishindo kikubwa, wasubiri mbeleko na mbeleko ni miaka mitano tu, wangebaki katika vyama vyao vya awali hata kama ungefanyika ubabe october baada ya miaka mitano wangeweza kurudi na kuendelea kupeta.

Hizi tabia zao za kutokukomaa walizozionesha zinatengeneza kupuuzwa, tena vijana ndio wakuwasikitikia zaidi kwasababu wangevumilia kukosa kwa miaka mitano tu mingine wangerudi kwa nguvu na kasi ya ajabu na wangebaki kwa muda mrefu kwenye viti.
 
N
Wabunge Joyce Sokombi na Sussane Masele (CHADEMA-VITI MAALUM) wametangaza kuhama CHADEMA na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sussane Masele ni mke wa ndoa wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA anayeitwa Tumaini Makene

View attachment 1456596
Naona kazi aliyopewa mbatia umeanza kuleta mafanikio. Watoke cadema - Nccr - ccm
 
Hata Mbowe naye aende huko huko ila furaha ni kuwa hawajaenda rasmi ccm. Huko ni mbinu tu za kubadili majina ili waweze kuja huku kuomba kula
 
Back
Top Bottom