News Alert: Wabunge wawili wa Viti Maalum CHADEMA wahamia NCCR Mageuzi

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
310
500
Wabunge Joyce Sokombi na Sussane Masele (CHADEMA-VITI MAALUM) wametangaza kuhama CHADEMA na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sussane Masele ni mke wa ndoa wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA anayeitwa Tumaini Makene


=====
Wabunge Suzana Maselle (Mwanza) na Joyce Sokombi (Mara) wametangaza kuondoka CHADEMA mara baada ya kumaliza kipindi chao cha Ubunge, Juni mwaka huu

Wamesema, uamuzi wao wa kuondoka CHADEMA umetokana na chama hicho kutawaliwa na ubinafsi, matumizi mabaya ya rasimali za chama na ubabe wa kiongozi Mkuu wa chama hicho

Wamedai kuwa, “hali hii imekuwa mbaya zaidi baada ya Esther Bulaya, kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi yetu na kujipa mamlaka yaliyopitiliza

Maselle amesema “Kabla ya hapo, palikuwepo na kafursa kakuulizwa na kujipendekeza. Wakati huu, ni amri tu. Kwa kifupi, maamuzi mengi ni ya kibabe na yenye kudharau watu wengine na kwa bahati mbaya Kiongozi Mkuu wa chama na ambaye pia ni KUB haonyeshi kuchukua hatua kurekebisha hali hii"

Kuhusu suala la kutoingia Bungeni, wabunge hao wawili wamesema, “suala la kutoingia Bungeni kwa siku 14 lilianzishwa na Esther Bulaya, ambaye kwa sasa inawezekana ndiye Mshauri Mkuu wa Freeman Mbowe kwa mambo ya chama na Bunge"

Wameeleza “Kwamba, mheshimiwa Bulaya ndiye aliyeanza kutoa maelekezo kwa Wabunge kuwa wasiingie Bungeni kwa siku 14, lakini Wabunge wakahoji mamlaka ya kufanya hivyo ameyatoa wapi?

Aidha, “Baadhi ya Wabunge akiwamo wale waandamizi kabisa, wakataka kiitishwe kikao cha Kambi ya Upinzani ili tuweze kujadili jambo hilo kwa mapana kwa kuweka bayana hasara na faida zake”

Amesema, sisi Wabunge wa Chadema tulikuwa tunachanga Tsh. 1,560,000 kwa Wabunge wa Viti Maalum kila mmoja na Sh. 520,000 kwa Mbunge wa jimbo kila mwezi

“Hapa hoja siyo kuchanga, kwanza ni takwa la kikatiba, hoja ni jinsi fedha hizo za michango ambayo tuliambiwa zitatumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jinsi zilivyotumika nje ya mipango iliyokusudiwa, na bila idhini ya vikao vyenye mamlaka hiyo"


FB_IMG_1590146766831.jpg
 

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,387
2,000
Chadema kulikoni!?, hili sio la kufumbia macho hili uongozi wa chama ipo haja sasa ya kujitafakari, suala la kusema kuwa hawa watu wananunuliwa naona kwasasa halina mashiko inatakiwa wajitafakari kama chama wajue tatizo liko wapi kisha wafanye marekebisho makubwa kwa masilahi ya chama na watanzania kwa ujumla wenye imani na hiki chama.
 
Top Bottom