Wabunge wawatimua mawaziri wa Kikwete; Kamati za Zitto, Serukamba zachachamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wawatimua mawaziri wa Kikwete; Kamati za Zitto, Serukamba zachachamaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  • Kamati za Zitto, Serukamba zachachamaa

  na Betty Kangonga

  KAMATI za Bunge za Miundombinu na ile ya Mashirika ya Umma (POAC) kwa nyakati tofauti jana ziliwatimua katika vikao mawaziri wawili kwa kushindwa kutoa maelezo yanayoridhisha kuhusu mwenendo wa mambo ndani ya wizara zao.
  Mawaziri waliofikwa na zahama hiyo ni Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, na mwenzake wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, ambao walifika mbele ya kamati hizo zilizoanza vikao vyake Ijumaa iliyopita.
  Waziri Nundu alijikuta katika wakati mgumu kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi wiki moja, mbele ya Kamati ya Miundombinu inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, baada ya maelezo yake kuhusu mwelekeo wa bajeti ijayo kushindwa kukidhi matarajio ya kamati hiyo.
  Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na baadaye katika mahojiano kwa njia ya simu na gazeti hili, Serukamba alisema walifikia hatua hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ilikuwa imeshindwa kutenga fedha katika maeneo yaliyopaswa kupewa kipaumbele.
  “Tumemrejesha waziri serikalini ili wakapange upya bajeti yao ya 2011/2012 baada ya kubaini kuwa maeneo ya kupewa vipaumbele kama Shirika la Ndege Tanzania (ATC), Shirika la Reli na Wakala wa Meli hayakutengewa fedha ambazo zingeyawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
  “Shirika la Ndege lenyewe linahitaji sh bilioni 23 ambazo ni lazima serikali iziweke. Pia Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo anatakiwa kutoa sh bilioni moja kwa ajili ya kulipia deni la ndege iliyo nchini Afrika Kusini,” alisema Serukamba.
  Akiendelea kufafanua alisema ili nchi yoyote iweze kufanya vema katika uchumi ni muhimu suala la uchukuzi likapewa kipaumbele.
  Akitoa mfano mwingine, mwenyekiti huyo alisema ili Wakala wa Meli aweze kufanya vyema anahitaji kiasi cha sh bilioni 1.6 ambazo serikali inahitajika kuzitoa ili kuwezesha ufanisi jambo ambalo halijafanywa katika makadirio yaliyoandaliwa na wizara hiyo.
  Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa Shirika la Reli linatarajiwa kuendeshwa na wazalendo kutokana na kuvunjwa kwa mkataba na aliyekuwa mbia wa kampuni hiyo ya Rites ya India.
  Alisema kutokana na hilo serikali inahitajika kutoa kiasi cha sh bilioni 200 kwa ajili ya kulifufua shirika hilo fedha ambazo zitaendesha shughuli za utendaji kwa kipindi cha miaka mitatu.
  “Hatuwezi kupitisha bajeti hiyo lazima serikali ituhakikishie kwamba itatoa fedha hizo. Wapo wanaosema serikali haina fedha lakini sisi tunajua kuwa inao uwezo,” alisema Serukamba.
  Alisema kuwa bajeti ya mwaka jana wizara hiyo ilitenga bajeti ya ndani ya sh bilioni 95 na badala yake ikapata kiasi cha sh bilioni 45 tu.
  Kama hiyo haitoshi, Serukamba alisema wahisani ambao pia waliahidi kuchangia sh bilioni 65 wakishindwa kufanya hivyo na wakaishia kutoa kiasi cha shilingi bilioni mbili tu, hatua ambayo kwa kiwango kikubwa iliathiri ufanisi.
  Awali, wakichangia bajeti hiyo wajumbe wa kamati hiyo walitoa kauli zilizokuwa zikionyesha wazi kutokuwa tayari kupitisha bajeti hiyo iwapo vipaumbele hivyo havitapewa fedha.
  Akichangia, Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi (CHADEMA), alisema kuwa ana mashaka ya kiwango cha utekelezaji kwani kinaonyesha kuwa hakijafikiwa kwa kipindi cha miaka mitano.
  Akizungumzia kuhusu tatizo la kukithiri kwa msongamano wa magari jijini la Dar es Salaam, Arfi alisema hakuna hatua zozote zinazoonekana kuchukuliwa kulikabili tatizo hilo.
  “Usafiri wa ndege, maji na barabara ni matatizo matupu maana katika uchaguzi waliahidi kuboresha vitu hivyo kama kununua meli jambo ambalo halijafanywa hadi sasa na zilizopo ni chakavu,” alisema.
  Alisema atakuwa mtu wa kwanza kupinga bajeti hiyo katika kamati na ndani ya Bunge ikiwa serikali itashindwa kuweka fedha za uboreshaji wa reli ya kati.
  Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machali NCCR-Mageuzi alihoji serikali itaendelea kuwalipa mishahara wafanyakazi wa ATC mpaka lini wakati hakuna vitendea kazi na kuongeza kwamba hawezi kuiunga mkono bajeti hiyo iwapo haitawekea mkazo katika masuala ya reli.
  Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkiwa Kimwanga (CUF) alihoji juu hatua ambazo zimeweza kuchukuliwa na ATC kwa Watanzania ambao wana tiketi za kampuni ya ndege ya shirika hilo.
  “Kuna Watanzania ambao wana tiketi za ndege za ATC mikononi hadi sasa hawafahamu ni vipi watapata fedha zao au kupatiwa usafiri naomba Waziri halifafanue hilo,” alisema.
  Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF), alisema kuwa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa juu ya kupunguza ajali ingawa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imekuwa ikiandika mambo mengi katika tafiti zao.
  Mbunge wa Tunduru Abdallah Mtutula (CCM) alisema kuwa ni lazima serikali ifike sehemu na kuweka kiburi na kutekeleza vipaumbele makini.
  “Kuna neno kiburi naomba viongozi mlipokee…kama mlitaka tujenge bandari ndogo naomba zisijengwe ili tuboreshe reli naamini kuwa hilo litakiweka sawa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa 2015,” alisema.
  Kwa upande mwingine, Zitto alimtoa nje Waziri Chami aliyeongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Mauzo nje (EPZ), Dk. Adelhelm Meru, na watendaji wa mamlaka hiyo kwa madai ya ufisadi wa sh bilioni 41 katika mradi wa Benjamin Mkapa ulioko Mabibo, jijini Dar es Salaam.
  Dk. Chami na watendaji hao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya mjumbe wa Kamati ya POAC kuhitaji ufafanuzi wa matumizi ya fedha katika mradi huo kwa kutofautiana na ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
  Mjumbe huyo ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya (CCM), alisema kutokana na hali hiyo kamati inahitaji kupata maelezo ya kina kwani inaonyesha kuna matumizi yaliyofanywa na kuzidi gharama za ujenzi wa mradi huo ambazo ni sh bilioni 14 kama ilivyopangwa na serikali.
  Kwa mujibu wa taarifa za CAG, kuna matumizi ya zaidi ya sh bilioni 41.
  “Tunahitaji ufafanuzi juu ya mradi huu sasa; inanyesha hata kuna malipo yalifanyika katika ununuzi wa vifaa hakunyesha stakabadhi za malipo, sasa hali hii inajenga shaka, kwa kuwa mwenyekiti wa baraza ambaye pia ni Waziri wa Viwanda unaweza kutupatia majibu ya kina kuhusu hili,” alisema Bulaya.
  Kutokana na hoja hiyo Waziri Chami, alimtupia Dk. Meru ili atoe ufafanuzi mbele ya kamati hiyo ambapo alisema toka kuanza kwa mradi huo mwaka 2005 mamlaka iliurithi kutoka kwa iliyokuwa Wizara ya Uwezeshaji na Uchumi iliyokuwa ikiongozwa na waziri wa wakati huo Juma Ngasongwa ambapo mwaka 2008 ulihamishiwa kwao.
  Dk. Meru, alisema tangu kuanza kwa mradi wa Benjamin Mkapa wanawasiliana na serikali ili kuomba nyaraka zilizokuwa zinaonyesha malipo halali lakini hadi sasa bado hawajafanikiwa kuzipata.
  Hali hiyo ililamzimu Waziri Chami, kuingilia kati na kusema kuwa hivi sasa tayari wamewasiliana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kupata nyaraka hizo za matumizi ya fedha hizo na tayari wameahidiwa kuzipata.
  Hata hivyo majibu hayo yalipingwa na mwenyekiti wa kamati hiyo alimtaka Waziri Chami na watendaji wake kutoka EPZ kuondoka kikaoni na mara watakapopata nyaraka hizo waje tena mbele ya kamati hiyo na kutoa maelezo yao ya kina.
  “Lengo letu ni kujenga… kwa hili katika mradi huu wa Benjamin Mkapa, kuna kitu ambacho hakileti tafsiri nzuri kwenu hivyo tunawataka muondoke na pindi mtakapopata nyaraka hizo muhimu ndipo mje mbele ya kamati.
  “Pamoja na yote inaoyesha matumizi yenu katika mradi huu yalikuwa yakiongezeka kila mara bila hata kufuata taratibu; katika kitabu cha CAG inaonyesha mradi umegharimu sh bilioni 24… matumizi ya wali yalikuwa sh bilioni 14 iliyotengwa na serikali.
  “…Lakini sasa inaoyesha kuna malipo yalikuwa yakifanywa bila hata kufuata utaratibu hadi kufikia sh bilioni 41; tunapata shaka na matumizi ya fedha za serikali kuchezewa na wajanja wachache,” alisema Zitto. Kutokana na maamuzi hayo wajumbe wa kamati hiyo waliunga mkono hatua hiyo hali iliyomlazimu Waziri Chami na timu yake kunyanyuka na kutoka nje ya ukumbi huo. Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya EPZ, inaonyesha kuwa toka mradi huo ulipoanzishwa watendaji hao wa EPZ wamekuwa wakilalamikiwa kutokana na kufuja fedha za umma ikiwemo kujilipa mishahara mikubwa na hata kufanya matumizi ya ununuzi wa vifaa kinyume cha sheria.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Baada ya siku kitafanyika kikao cha Wabunge wa CCM chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, wakitoka huko bajeti za wizara zote zitapitishwa kwa kauli moja.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa mkuu na zitaonekana hazina kasoro hata kama asilimia za bajeti za maendeleo ni sifuri
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Ewaaa huondio mtindo wa CCM umelifikisha taifa mahali pagumu kwasababu ya kulindana.
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mtindo wa kukubali kila kinacholetwa na chama chao hata kama ni kibovu wapo ni kupitisha na kupiga makofi
   
 6. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133

  How sad!! Ni ukweli unaoumiza sana tena mchungu kuliko shubiri kuumeza.
   
 7. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wakomaliwe tu mpaka kieleweke, nchi hii si masikini kama tunavyodanganywa.
   
 8. H

  Haki Yetu Senior Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yuko wapi yule kasuku aliyesema kwamba JK ameanza kutekeleza ahadi zake? Ni lazima ifike siku watanzania tuseme BASI INATOSHA katika mambo ya kifisadi kama haya......!!!!
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu ahadi wakati bajeti ya wizara husika ya mwaka unaoisha ilipigwa panga na ya mwaka huu haijakaa sawa na unategemea hata ya mwakani itakaa sawa kweli
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nahisi kama hizi kamati za bunge na hawa wenyeviti wake wanatafuta umaarufu sana kupitia vyombo vya habari. Sidhani kisheria hizi kamati zina mamlaka ya kutoa maamuzi au adhabu wanazoongea au hata kufukuza mawaziri na watendaji wa serikali! wanachotakiwa kufanya ni kukagua na kutoa mapendekezo. basi!

  Hivi tuliwahi kumsikia wapi mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali akifukuza mawaziri au akitoa adhabu? kwa nini wabunge ambao kimsingi wako kwenye chombo cha sheria lakini wanashindwa kuishi ndani ya sheria na taratibu za kiutawala? Kama kweli hizi kamati zina nguvu hivyo kwa nini ile ya Mwakyembe na mapendekezo yake yako kabatini? Serukamba yuko kwenye special mission lakini nasubiri kwa hamu atembelee TICS na atoe each and every shortfall mbele ya vyombo vya habari.

  Office ya Spika inatakiwa itoe job description kwa hawa wabunge vinginevyo siku si nyingi wataumbuka, tena hadharani.
   
 11. H

  Haika JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa, na hao wanakamati walioshirikiana kuhoji watakuwa 'wameshaelewa ule upungufu waliodhani ulikuwapo' kwa hiyo wamebadili msimamo na wanakubali bajeti zipite. Watabaki wenye viherehere kama kina Zitto wakishangaa.
  It is like that, and will always be that, unless WE decide otherwise.
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  We have been doing so for the past 50 years, why should we change now? We are used "Mheshimiwa spika naunga mkono hoja lakini............." ukijumlisha hizo lakini kumbe alitakiwa aseme "siungi mkono hoja kutokana na sababu zifuatazo............"
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  For the past 50 years wameunga mkono hoja ila hatujaona matunda ya kuunga mkono hoja maana maisha yamezidi kuwa mabaya na kile walichokiunga mkono hakijafanya la maana katika kuhakikisha kuwa maisha ya watanganyika yanakuwa mazuri. Bunge lapaswa kuwa na utaratibu mwingine wa kujadili hoja na uwajibikaji maana hili la sasa nguvu za chama kimoja na uwepo wa wabunge wengi wa chama tawala unalifanya likose hata maana ya kujadili hoja za maana

  Wanakosa utashi wanakosa uhuru wa kusema yale yanayopaswa waseme maana mbunge anajua kuw awaziri hajatimiza malengo yake ya mwaka uliotangulia na kwenye bajeti ilipitishwa kuwa ni lazima hilo lifanyike ila the same waziri anakuja na maelezo kuwa miradi huo unashughulikiwa au sijui mchakato wake umeanza au litafanyika katika bajeti ya mwaka ujao na then mbunge anasimama anasema anaunga mkono hoja lakini....... haiingii akilini. Waziri hapo alipaswa kuwajibika na bajeti yake isipitishwe. Ila hata kama bajeti inazuiliwa wakikaa kama kamati ya chama mbunge analainishwa kwa the same ahadi anapitisha bajeti.

  Hakuna mbunge mwenye uwezo wa kusimamia hoja yake ya kutopitisha bajeti ya serikali hata kama moyoni mwake na dhamira inamsuta ila ataunga mkono hoja kwa kuwa anajua asipofanya hivyo anaweza asipitishwe tena kugombea uchaguzi unafuata
   
 14. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Inauma sana miaka yote si ndio hivyo hivyo nakugongea thanx
   
 15. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,354
  Trophy Points: 280
  Ni upuuzi mtupu kwa kweli hivi hizi kamati si zinatakiwa ziwe zinakaa kabla ya bajeti ndiyo majadiliano yaanze na mapendekezo yapelekwe kunako husika kabla ya wizara husika kuamua kutenga kiasi gani kutokana na uwezo wa kifedha.

  Kuna sababu gani ya watu kukaa chini kupanga matumizi wakati hela imeshatolewa ndio maana uzushi mwingi utokea baadae na wapinzani hukosa siasa halisi kukagua matumizi ya serikali mpaka kamati zikae.

  Aim ya kamati za bunge ni kuweka transparency by involving experts, wabunge wa upinzani na wabunge wa serikali kujadili masuala muhimu ya policies za serikali, sababu za maamuzi yao na kwanini seriakli inachukua maamuzi fulani.

  Hili linawapa upinzani huwezo wa kuwa na counterarguments kutokana na policy za serikali. Lakini hizi kamati zetu hata sizielewi kazi za body zingine ndio zinafanywa na kamati, waongozaji wa kamati wanapigiwa kura wakati kwingine waziri husika ndio mwenyekiti wa kamati.

  Sasa hata sijui huwa hela inatengwa vipi kwenye kila wizara au kupitia kanuni zipi au hata kama kuna prioritised policies kwenye bajeti za wizara (apart from per-diems kwenye nchi yenye viongozi wenye njaa) after that liwalo na liwe mi naona. Si ajabu kunakuwa na mambo kama haya na serikali huja na majibu ya mkato mkato na Mkullo huyo uenda unpunished.

  Kwa kweli siasa zetu ni hadithi za abunuwasi (vichekesho vitupu).
   
 16. DJ CHOKA FREDY

  DJ CHOKA FREDY Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaokubali bajeti hii ipite wanyoshe mikono,,,,, wasiokubali wanyoshe mikono.....waheshimiwa wabunge wanaokubali wameshinda,, jamani huu ndio muundo wa bunge letu chini ya spika wa magamba..:mimba:
   
 17. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naona mmesahau kuwa wabunge wa CCM ni wazee wa ndiyoooooooooooooooooo na wabunge wa upinzani wengi ni wazee wa hapanaaaaaa
   
Loading...