Wabunge wavae majoho kama madiwani ili kuepusha kufukuzana Bungeni kwa ajili ya mavazi

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,879
Spika wa Bunge amemfukuza mbunge kwa kutokuvaa mavazi yenye maadili kwa Bunge .

Ili kuepusha hilo nashauri wabunge nao waamue kuvaa majoho kama wafanyavyo madiwani kwani uamuzi huo utakuwa ndio tiba sahihi la kuvaa mavazi yenye kukidhi maadili yetu.

Pia maadili isiwe kwenye mavazi tu bali maadili yawe pia kwenye kuheshimu Katiba na Sheria za nchi kwani ndio utamaduni wetu. Hivyo basi Spika awe mfano wa kiongozi anayetakiwa kuwa na maadili ya kuheshimu katiba aache kuichezea.
 
Juzi SPIKA wa BUNGE Amemfukuza MBUNGE kwa kutokuvaa MAVAZI yenye MAADILI kwa BUNGE .Ili Kuepusha hilo Nashauri WABUNGE nao Waamue kuvaa MAJOHO kama Wafanyavyo MADIWANI kwani Uamuzi huo utakuwa Ndio TIBA sahihi la Kuvaa Mavazi yenye Kukidhi Maadili yetu.Pia MAADILI isiwe kwenye Mavazi tu Bali Maadili yawe pia Kwenye Kuheshimu KATIBA na SHERIA za NCHI kwani ndio Utamaduni Wetu.Hivyo basi SPIKA awe Mfano wa Kiongozi Anayetakiwa kuwa na MAADILI ya KUHESHIMU KATIBA Aache KUICHEZEA.
Manhood swafi hata ukiwa na hard on, no one will no. Msukuma anavaa majoho kila siku
 
Sasa itaitwa kwaya ya ndugai.
Majoho miezi mitatu wawapo bungeni.
Bora wavae share za chama,binge liwe LA kijani
 
Kumekuwa na mitazamo tofauti toka sakata la mjadala wa mavazi kwa wabunge hususani kwa wabunge wa jinsia ya kike kuibuliwa bungeni. Kila upande umekuwa ukitengeneza hoja ili kujenga uhalali. Kwa muono mpana, hili jambo halitakaa liishe leo wala kesho, litaendelea kuibuka kila mara.

Kwa mtazamo wangu, suluhisho sahihi na kamili ni wabunge kuvalishwa mavazi rasmi yenye kufanana (uniform), na kwa hilo ninapendekeza majoho mahususi yashonwe na wabunge wavalishwe kila wanapoingia kwenye vikao vya bunge na kamati. Suala la vazi gani avae mbunge akitaka kuingia bungeni liwe ni jukumu la bunge na sio jukumu la mbunge!
Na sababu zangu ni hizi.


1. Huwezi ukawafuatilia kwa haki na kuwadhibiti wabunge zaidi ya mia tatu kimavazi kila wanapoingia bungeni ikiwa kila mbunge anaweza kuvaa chochote wakati wowote akiingia bungeni.

2. Huwezi kuwa na viwango (standard) zenye kuweza kuwaridhisha wabunge zaidi ya mia tatu kila wanapotaka kuingia bungeni ikiwa kila mmoja ana uhuru wa kuvaa chochote anachokitaka.

3. Tafsiri ya mavazi yenye staha dhidi ya mavazi yasiyo na staha haina maana yoyote katika jamii yenye mitazamo mchanganyiko kuhusu imani, mila, tamaduni, jinsia, rika na mitindo ya kimaisha.
 
Naunga mkono.Sio mbunge anavaa kama anakwenda kwenye kigodoro.Hali pesa za suti wanapewa.
 
Kama hili😂👇
IMG_20210511_010957.jpg
 
unajua siku hizi WATANZANIA WENGI SANA huvaa kiuZINZI ZINZI sana, alafu wanajitetea sana kwamba nguo hizo hazina matatizo..hovyo sana!!. Nawapongeza waislam kwa mavazi yao
 
Nashauri pia wawe wana-parade halafu wakaguliwe kabla ya kuingia mjengoni.
 
ME, wavae kaputula
KE , wavae sketi za malinda tena
ndefu kama magauni ya Tulia.
RANGI,
Nyeusi,Kilimbulini,Bluu,Kaki
Kama za mbowe,kijani,kaniki

Wachague kiranja/monitor awapangie ratiba J3 hadi Ij ranging ipi itatumika.

WATUMISHI WABUNGE MBONA WAMEWEZA?

TATIZO LA WABUNGE WANAVAA KWA MASHINDANO BILA HOJA ZA MAENDELEO YA KIBUNGE
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom