Wabunge waunga mkono 100% Ni janga la Taifa

bensonlifua92

Member
Dec 9, 2010
84
33
Nawasikiliza wabunge wa pande zote mbili yaani wa CCM na wale wengine wa CHADEMA, CUF, NCCR, n.k. Ninachokiona kutoka kwa wale wa CCM ni siasa na kutozingatia nini kinaendelea sasa katika taifa letu. Waheshimiwa wabunge wananchi wana changamoto kubwa za maisha sivyo mnavyodhani nyie wabunge. Hamko serious kabisa wabunge mnaounga hoja 100%. Utaungaje hoja 100% yaani kweli 100% huo ni upungufu kabisa na hii naungana na Mch Msigwa "....AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA...."

Wabunge wa CCM hawajitofautishi wao na Serikali yao ya CCM, .....wabunge nyie siyo watendaji wa serikali acaheni ushabiki.... Wao wanadhani wanawakomoa CHADEMA kwa kusema yale yote wanayosema bungeni...... naunga mkono 100%......Kwa ujumla wanawakomoa wananchi na siyo Chadema...

Ushauri wangu wabunge wote wanaounga hoja 100% wasiendelee kuchangia tena maana baada ya hapo wanakuwa wanapoteza muda tuu maana hana mapya zaidi ya hoja yenyewe. Pia wengi wanaounga 100% hoja na wanaendelea kuchangia wanaishia kujichanganya na kutoeleweka kabisa maana anaishia kukosoa hiyo bajeti tena na anakosa msimamo wake ni upi. Hivi hawa watu wanajua kama sisi watanzania tunawaona na kwamba tunakuja wahukumu jinsi walivyo? Mfano mtu anaunga 100% bajeti halafu anasema hii bajeti imekuja na vipaumbele vilevile why? sasa mtu kama huyu utamwitaje..... mpe jina wewe.....

Nawasilisha
 
Shida nyingine watanzania mnazitaka wenyewe!!! Si hao wabungue mliwachagua ninyi wenyewe? Acheni wafanye kazi yao! Tulieni mliwe vizuri hadi hapo mtakapopata akili na mang'amuzi ya kuondoa ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa!!
 
WAJINGA NDIO WALIWAO. WAUNGE TU MKONO TUNAWASUBIRI NJE. BUDGET MPOVU AVAI KUONGA MKONO KABISA. MWENYE KUSEMA UKWELI NDANI YA BUDGET NI MHE. SANYA. THE REST ARE HOPELESS KABISA.

NI JANGA KUBWA NA LAZIMA AITAELEWEKA. WAJARIBU TUU HAWA WAFISADI --- SAFARI HII ATUKUBALI KUDANGANYUA
:A S-devil4:
 
Wana JFChadema bao ni 90% ya wana JF wote,mliomo humu pandeni mabasi muende Dodoma kusaidia kambi yenu Bungeni, imelemewa.
Sisi wabunge wetu wana fanya tulichowatuma kufanya.
 
washachimbwa mkwara hao ndo maana wametepeta kama unavyowaona...ila one day tutafika tu ninicho amini MUNGU yupo na anayaona haya yoote
 
Nadhani ikiwa mtu anaunga mkono hana haja ya kupoteza muda wa kuikosoa bajeti, Unakuta mbunge katika kuchangia anaiponda bajeti asilimia 100 then anamalizia eti naunga mkono hoja mia kwa mia. Huwa nachoka kweli nikisikia hivyo. Sijui wana mtetea nani na kumkomoa nani??
 
Back
Top Bottom