Wabunge waulipua uongozi wa ATC; Ina ndege moja, watumishi 155 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waulipua uongozi wa ATC; Ina ndege moja, watumishi 155

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Wadai unanuka rushwa, siasa

  KUTOKANA na kusuasua kwa uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), wabunge wamelishukia shirika hilo wakisema limejaa rushwa na maamuzi ya kisiasa. Wamesema shirika hilo pia kwa sasa halina shughuli ya kibiashara inayofanyika kutokana na kuwa na ndege moja inayotoa huduma, huku likiwa na wafanyakazi 155.

  Kauli hizo zilitolewa jana, wakati kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokutana na uongozi wa wizara za Uchukuzi na Ujenzi. Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele (CCM), alisema uongozi wa ATC unanuka rushwa na kwamba, anashindwa kuelewa zilikopelekwa fedha zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kulipia madeni ya ndani, ili shirika liweze kujiendesha.


  .
  [​IMG]

  "Bodi na menejimenti ya ATC sijui zinafanya kazi gani, ni bora zikavunjwa na watu wakaacha kufanya kazi kwa mazoea. Wanalitia hasara shirika, kwa nini tunawekeza fedha nyingi kwenye viwanja vya ndege wakati hatuna hata ndege moja, viongozi wa ATC ni wala rushwa na hawawezi kufanya lolote," alidai.


  Masele alisema menejimenti ya ATC ni tatizo kubwa, kwani inapatiwa fedha na inazitumia vibaya, huku hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya jambo hilo kufahamika. Kwa mujibu wa Masele, iwapo viongozi wa bodi na menejimenti wataondolewa na kuwekwa wengine, hali inaweza kuwa nzuri na mabadiliko yataonekana.

  Naye mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Mohamed (CCM), alisema tatizo kubwa linaloyagharimu mashirika ya umma ni kuendeshwa kisiasa, hivyo alishauri viongozi kuwa makini na kutanguliza maslahi ya taifa mbele. Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruhwanya (CHADEMA), kwa upande wake alitaka kufahamu mikakati iliyowekwa na serikali katika kulifufua shirika hilo. Alitaka pia kufahamu zilikokwenda fedha za nauli zilizolipwa na abiria waliosafiri na ndege za shirika hilo.

  Naye Lucy Owenya, Viti Maalumu (CHADEMA) alitaka kufahamu shirika hilo lina wafanyakazi wangapi na ndege ngapi. Akijubu maswali hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Injinia Omar Chambo, alisema shirika hilo lina hali mbaya, na kwamba, serikali haitawekeza tena, bali mkakati uliopo ni kufanya kazi kwa ubia. Injinia Chambo alisema shirika hilo lina ndege mbili, moja ikiwa ya kukodi. Hata hivyo, alisema kati ya hizo, moja ipo Afrika Kusini kwa matengenezo, ambapo dola za Marekani 700,000 (zaidi ya sh. bilioni moja) zinahitajika.

  Alisema ATC ina wafanyakazi 155 na kuna mpango wa kuwapunguza. Kuhusu menejimenti na bodi alisema taratibu zinaangaliwa ili kuchukua hatua. Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Zainab Vullu, aliutaka uongozi wa wizara kutoa maelezo ya sh. milioni 40 zinazotumika kulipa pango la jengo.

  Alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa, na kuhoji kwa nini hawana jengo, wakati pesa zinazokusanywa ni nyingi. Chambo alisema ATC haina fedha za kujenga ofisi.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  It is painful to see how David Mattaka is destroying this Corporation Air Tanzania; I remember once while in Mwanza a way back we were at the airport for our flight to Dar and the phone call came to pick up the family of a certain Powerful Minister all of us passengers were left and told that we had to wait until either later that evening or next day by then they used to have 2 boeng 703 so one we were supposed board it pick up 18 members of that Minister only the plane with capacity of 133 people.

  No one has to compain then it was one party system - Ujamaa na Kujitegemea.
   
 3. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KWA KWELI HII KALI KWA HIYO MLIONDOKA BAADAE AU KESHO YAKE?

  Bado anaweza funguliwa mashtaka sema wa TZ waoga viongozi na wanakula wote. na ndio maana labda wanacheza game mbovu hizi
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  The next day
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Haingii akilini shirika la ndege lisilo na ndege liwe na waajiriwa 155 pamoja na mkurugenzi. Kwanza huyo mkurugenzi aliwahi kufukuzwa kazi enzi za Mkapa lakini ushkaji ukamnusuru. Wanalipwa mishahara kwa kazi gani waliyoifanya?
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ndio mlolongo wa ufisadi......................angalieni TRC,TTCL nk,wakati mwingine hali hii inasababishwa na viongozi wenye maslahi binafsi kwenye mashirika binafsi......mfano TTCL inakufa kwasababu ya njama chafu za baadhi ya viongozi wenye hisa makampuni binafsi................
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hiyo ndege itakuwa na ufanisi uliotukuka!
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Angekuwepo Mrema kwenye hiyo kamati angewashughulikia wala Rushwa wote.
   
 9. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Shame ndege 2 wafanyakazi 155??
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Shirika la Kizalendo lilitaka kuinunua ATC serikali inagoma sababu haitapata mahali pa kula -- Shirika hilo la Kizalendo ni Precision Air
   
 11. MWAKIGOBE

  MWAKIGOBE Member

  #11
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni ajabu na ni kama nchi ya kusadikika, Yaani tunashirika la ndege lisilo kuwa na ndege hata moja?. kuna uhalali gani wa kuwa na hili shirika?. je wapi tunapata pesa za kuliendesha shirika hewa?. mmmmmhhhh. hii ni kama kusadikika
   
 12. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwani David Matakka bado ni CEO wa hili ATCL? Naomba munijuze maana wengine hatujui kinachoendelea
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kila ndege moja ina hudumiwa na wafanyakazi 77!!
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  David Mattaka hayupo tena ATCL na kwa sasa ATCL inaongozwa na mtu mmoja anaitwa William Haji akiwa kama acting DG
   
 15. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu naona umesahau Kirefu cha ATC ni ''Any Time Cancellation'' Mi yalinikiuta pia, ilikuwa trip ya Mwanza / Zanzibar, nilisota DAR siku mbili no refund, no accomodation. halafu ilikuwa njoo kesho jioni usafiri utakuwepo, kila nikienda hamna kitu!
   
 16. k

  kinyongarangi Member

  #16
  Aug 3, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata DAWASCO inashindwa kufanya kwa ufanisi kwa mtindo huo huo. Inakusanya na kuhudumia managenet mbili, Board za wakurugenzi mbili na staff wa mashirika mawili (DAWASA na DAWASCO). kama lingekuwa shirika moja running cost zingepungua na shirika kuwekeza katika kuboresha miundombinu
   
 17. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  No commitment wajameni,watu wanaendesha mashirika ya umma kama vile ni duka la masawe ndugu zangu,uzalendo umekufa but hii ni kwa sababu mtu akiiba hapa anapelekwa kungine na wala hachukuliwi hatua.
   
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Sasa wizara nuda wote inafanya kazi gani? Hivi ukichaguliwa kua waziri au katibu ni lazima ukubali hata kama huwezi?
  Watu kila siku wanavaa tai kwenda ofisini, kufanya nini sasa?
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Watanzania jamani, vyombo vingi na blogs mbalimbali vimekazania kumsakama Nyerere, lakini hawaangalii mazuri yote aliyoanzisha Nyerere wakati wa utawala wake.

  Mashirika mangapi yamebaki yakipumua yaliyonzishwa na Nyerere?

  Pamoja na umaskini tuliokuwa nao wakati wa Nyerere lakini kodi zetu alizielekeza kwenye mambo ya msingi lakini hayo aliyoyafanya leo wachache wamefanya shamba la bibi.

  Hakika historia itawahukumu.
   
 20. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  hatuna ndege tuna vipepeo kipepe kikichoka kinakuwa mapambo ona sasa dege liko mwanza watu wanafanya utalii
   
Loading...