Wabunge wateteao wananchi kufikishwa kizimbani kwa KARANDINGA, wezi kwa Basi MAALUM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wateteao wananchi kufikishwa kizimbani kwa KARANDINGA, wezi kwa Basi MAALUM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Jan 7, 2011.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thursday, 06 January 2011 20:55
  Source Mwananchi

  Waandishi Wetu

  UMATI wa wakazi wa mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani, jana ulifurika katika Viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kusikiliza kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.

  Vingozi hao pia walifikishwa mahakamani hapo sambamba na wabunge watatu wa chama hicho; Philemon Ndesamburo wa Moshi Mjini, Joseph Selasini wa Rombo, Godbles Lema wa Arusha na watu wengine 21.

  Watuhumiwa wengine watano akiwemo mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi walitakiwa kusomewa mashtaka katika hosipitali ya mkoa wa Arusha, Mount Meru walikolazwa baada ya kujeruhiwa juzi katika maandamano ya Chadema yaliyozimwa na polisi.

  Kwa pamoja walifikishwa katika viwanja vya Mahakama Kuu majira ya 8:40 mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali, huku Dk Slaa, Mbowe na Ndesamburo wakiwa kwenye gari dogo aina ya Landrover.

  Watuhumiwa wengine walifikishwa mahakamani hapo kwa karandinga. Waliokuwa kwenye Karandinga hilo ni Selasini, Lema na washitakiwa wengine.

  Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Zakaria Elisante alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Charles Magesa, kuwa watuhumiwa hao, wametenda kosa moja la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
  Elisante alisema kwa kufanya kosa hilo, watuhumiwa hao, wamevunja sheria namba 74 na 75 kifungu cha 16 kama ilivyofanyiwa marekebishoa mwaka 2002 na pia sheria ya polisi sura 45 kifungu cha 322 ambayo pia ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Hata hivyo, watuhumiwa wote walikana makosa hayo na wakili huyo wa serikali alisema hana pingamizi dhidi ya dhamana yao.

  Mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Arbert Msando, walisema mahakamani hapo kwamba, watuhumiwa wote wana wadhamini ambapo wote walidhaminiwa kwa thamani ya Sh 2 milioni kila mmoja.

  Hata hivyo kati ya watuhumiwa 31 waliotakiwa kusomewa mashtaka ni 29 pekee waliosomewa kufuatia watuhumiwa wawili kukosekana katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru walipokuwa wamelazwa.
  Watuhumiwa hao ni Frank Rogati na Swalehe Salum.

  Mchumba wa Slaa asomewa
  shtaka akiwa hospitalini
  Mchumba wa Dk Slaa, Josephine Mushumbuzi na watuhumiwa wengine watatu jana walisomewa mashtaka wakiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru wanakoendelea na matibabu kufuatia kujeruhiwa katika tafrani ya polisi na wafuasi wa Chadema juzi.

  Josephine tayari alikuwa ameshonwa nyuzi saba kichwani, huku watuhumiwa wengine wakiwa ni Kenedy Bundara, Juma Wambura na Richard Mtui ambao wote walikuwa na majeraha ya risasi.
  Lakini wote walipewa dhamana kama wenzao waliofikishwa mahakamani na kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Januari 21 mwaka huu.

  Nahodha: Vurugu za Arusha ni siasa
  Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema vurugu zilizotokea Arusha juzi ni tatizo la kisiasa ambalo pia litapaswa kushughulikiwa kisiasa.

  “Wote tunapaswa kulinda amani yetu. Tunapaswa kutuliza hali ya Arusha. Kilichotokea Arusha ni mgogoro wa kisiasa tutautatua pia kisiasa,” alisema Nahodha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, jana, jijini Dar es Salaam.
  “Biblia inasema ‘ni heri wapatanishi kwani wao watarithi nchi,’… sisi (serikali) tutawakutanisha pande zote ili tufikie muafaka na kutuliza hali ya Arusha,” alisema Nahodha.
  Wakati Nahodha akieleza kuwa tatizo la Arusha ni la kisiasa, IGP Mwema alitangaza kuyapiga marufuku maandamano ya Chadema akibainisha kwamba taarifa za kiintelijensia zimebaini kwamba kungekuwa na vurugu wakati wa kufanyika kwake.
  "Maandamano hayo ni marufuku, lakini wanaruhusiwa kufanya mkutano wao wa hadhara. Kuna taarifa za kiintelijensia kwamba kunaweza kutokea fujo na uvunjifu wa amani,” alisema IGP Mwema alipozungumza na waandishi wa habari.

  Lakini jana Nahodha alisema hatua ya maridhiano kwa sasa ni muhimu kwani, baada ya msuguano wa wiki kadhaa, pande mbili zinazosuguana mkoani humo, sasa zimeridhika kuwa kuna tatizo la msingi ambalo linapaswa litatuliwe.
  “Kunawakati wa kuchukia na wakati wa kufurahi, wakati wa kupenda na wakati wa kuridhiana, sasa wakati wa maridhiano umewadia,” alisema Nahodha ambaye pia ana taaluma ya diplomasia.

  Aliendelea kufafanua kuwa, kulingana na taaluma ya migogoro, usuluhishi hufanikiwa pale tu ambapo wahusika wa pande zinazosuguana kuona na kuamini kwamba kuna tatizo.
  Alisema kuwa, kwa muda sasa zilikuwepo juhudi za kusuluhisha mgogoro wa Arusha, ambazo zilikuwa zikifanyika chinichini, lakini kutokana na hali ilivyo sasa, itabidi usuluhishi huo kufanyika kwa uwazi.

  Kuhusu muda utakaotumika kufanya usuluhishi huo kisiasa, Nahodha alisema “Nadharia ya usuluhishi wa migogoro kwanza kabisa ni kutokuwa na haraka, suala la muda utakaotumika, utategemeana na msuluhishi pamoja na wasuluhishwaji. Unaweza kutumika hata second (sekunde) moja.”

  Akijibu swali kama serikali itakuwa tayari kufuta kesi mbalimbali zinazowakabili viongozi na wananchi waliokamatwa kutokana na tukio hilo, Naodha alisema hakuna na jibu la moja kwa moja ingawa swali hilo litachukuliwa kama ushauri.

  Kuhusu uwezekano wa kutengua matokeo ya umeya Arusha, suala ambalo pia Chadema wanalilalamikia, Naodha alisema “Sina uhakika kama tatizo la msingi lililopo Arusha linatokana na Umeya. Lakini katika mazungumzo tukibaini kuwa hilo ndiyo tatizo basi tutalifanyia kazi.”

  Naye IGP Said Mwema ambaye pia alihudhuria mkutano huo, alionekana kubabaika kujibu maswali mengi yaliyoulizwa na waandishi juu ya polisi kutumia nguvu kubwa kuwakabili Chadema mjini Arusha juzi.
  Alikwepa kujibu pia swali la waandishi wa habari iwapo kuna polisi anayeshikiliawa kutokana na kusababisha vifo vya raia wawili.
  Waandishi waliuliza maswali baada ya Waziri Naodha kumaliza kuzungumza, ambapo baada ya kuyaandika maswali ya waandishi alimtaka IGP kuanza kutoa majibu kwa yale maswali yanayowahusu polisi moja kwa moja.

  Katika awamu ya kwanza ya majibu yamaswali hayo, IGP hakujibu swali lililomtaka kueleza endapo madhara yaliyotakana na fujo hizo, ni madogo, makubwa au yanalingana na yale ya taarifa alizodai kuwa ni za kiintelijensia, ambazo walizitumia kutoa tamko la kisitisha maandamano.

  Kuhusu madai kwamba kuna kikosi cha polisi kutoka Ukonga jijini Dar es Salaam, Chuo cha Polisi Moshi (CCP) na Manyara vilivyopelekwa Arusha kudhibiti vurugu, alisema:
  “Hakuna askari tuliowachukua kutoka Ukonga, suala la polisi kutumia askari wangapi na kutoka wapi, hilo ni suala la taaluma ya polisi na hatuwezi kutangaza kwa kuwa hayo ni mambo ya security (kiusalama)."

  Hata hivyo alikiri askari wa ziada kupelekwa Arusha kutoka vikosi vingine ili kuongeza nguvu ya kulinda usalama wa raia.
  “Sisi kuweka mpaka askari wa reserve (waakiba) mgetupongeza, kuongeza askari sisi hiyo ni issue ya kiusalama, kuna mpaka askari waliondoka jana (juzi) kwa sababu ya ku-project hali leo (jana).

  Alisema kutokana na hali ilivyo katika mkoa huo, maafisa mbalimbali wa polisi walitumwa kwenda Arusha ili kuchunguza hali ilivyo.

  Kuhusu kuwepo kwa mkanganyiko wa amri ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ya kuruhusu maandamano pamoja na aliyoitoa ya kusitisha amaandamano, IGP alisema :
  “Kwa taarifa yenu kuna barua ya ruhusa na katazo la maandamano hayo kutoka kwa RPC wa Arusha, nilichokifanya mimi ni kutoa msisitizo tu,” alisema IGP Mwema.

  Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma Arusha na Fredy Azzah


  INASIKITISHA HALI INAYOENDELEA KATIKA NCHI HII. WEZI WANAOSABABISHIA TAIFA HASARA YA MABILIONI WANAPELEKWA KORTINI KWA BASI MAALUM. HAWA WATETEZI KWA KARANDINGA IMEKAAJE?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  hata firauni alikubali kuwatoa wana waisraeli, so hata haya yana mwisho.
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Frank robert and swalehe salum.we need to know where are they,are they dead or alive?
   
 4. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  IGP Mwema utendaji sifuri!Kapambene na majambazi...
   
 5. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I am sorry I did not understand your question? Can you please elaborate?
   
Loading...