BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Wabunge wataka waongezewe fedha
Stella Nyemenohi
Daily News; Thursday,March 27, 2008 @00:02
WABUNGE wameishauri serikali iwaongezee bajeti kwa ajili ya Bunge kutoka asilimia 0.07 ya sasa hadi asilimia 0.1 ya bajeti yote.
Mapendekezo hayo, yalitolewa Dar es Salaam jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta katika kikao cha wabunge cha kupata maelezo kuhusu mwongozo wa kutayarisha mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2008/09 hadi 2010/11.
Hoja hiyo ya Sitta, iliungwa na asilimia kubwa ya wabunge waliokuwa wakichangia mada kuhusu mwongozo huo, iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.
Katika kikao hicho kilichofunguliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baadhi ya wabunge walisema hata kiasi kilichopendekezwa na Spika hakitoshelezi mahitaji.
Miongoni mwao ni Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi (CCM) aliyependekeza ifikie asilimia 0.5 na Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes aliyependekeza iwe asilimia 1.5.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (CCM), alishauri kiwango kiongezwe huku akitolea mfano wa Kenya, ambayo Bunge linapata asilimia mbili huku Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja, akisema utegemezi wa wahisani unadidimiza.
Wengine waliounga mkono mapendekezo hayo (wote wa CCM) ni Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, Mbunge wa Handeni, Dk. Abdallah Kigoda, Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai, na Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mng'ong'o. "Hili siyo ombi. Bajeti ya wabunge iongezwe. Tumechoka kunyanyasika. Hii ni kauli ya wabunge," alisema Msindai.
Akizungumza na HabariLeo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alisema Bunge halina budi kuwezeshwa ili liwe huru. Kwa mujibu wake, Bunge la sasa haliko huru kutokana na utegemezi wa kupangiwa bajeti na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katika hatua nyingine, suala la mikataba mibovu lilijitokeza pia katika majadiliano hayo ya wabunge ambako Mbunge wa Pangani, Mohamed Risherd (CCM), alishauri serikali ifungue kesi katika Mahakama ya Kimataifa kuipinga ili kukuza uchumi.
Naye Mbunge wa Handeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Dk. Kigoda, alishauri suala la mfumuko wa bei lichunguzwe kwa umakini kwa kile alichodai kuwa upo uwezekano mkubwa kuwa mikataba mibovu ya umeme ndiyo inachangia tatizo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliiomba Serikali itoe ufafanuzi juu ya masharti yanayodhaniwa kuwekwa na wahisani yakisema kuwa isipotatua suala la Mwafaka, kashfa ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na ile ya Richmond, haitachangia bajeti.
Zitto alihoji hivyo kutokana na kauli iliyotolewa na Waziri Mkulo kuwa katika hali halisi ya bajeti ijayo, haitakuwa na ongezeko ikilinganishwa na ile ya mwaka 2007/08.
Katika taarifa yake, Mkulo alisema serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara na Sh bilioni 1.45 zimetengwa kwa mwaka ujao ikilinganishwa na Sh bilioni 1.18 za mwaka 2007/2008.
Alisema katika bajeti hiyo fedha za wahisani na za ndani zimepungua kwa mwaka ujao ikilinganishwa na bajeti ya 2007/2008 kutoka Sh bilioni 2.3 hadi Sh bilioni 1.8. Majadiliano kuhusu mkutano huo wa mwongozo wa kutayarisha Bajeti ya Serikali yanaendelea leo.