Wabunge wataka TANESCO itumbuliwe

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua jipu shirika la umeme Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi licha ya kumiliki asilimia 20% ya hisa katika kiwanda cha Tansfoma cha Tanalec kilichopo jijini Arusha .

Kamati hiyo ya Bunge imebaini hayo wakati wa ziara yao ya kutembelea viwanda jijini Arusha ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa viwanda ambapo Wabunge hao wameshangazwa na kitendo cha Tanesco kutonunua transfoma katika kiwanda hicho ambazo huuzwa katika nchi jirani za Kenya ,Zambia Malawi na Burundi.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo alisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa Tanesco ambao ni wamiliki wa Tanalec na wako katika wakurugenzi wa bodi lakini bado wanaagiza transfoma nje ya nchi suala ambalo linapaswa kutazamwa kwa umakini na kupatiwa majibu.

“Tunashindwa kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni cha kwao na wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba yuko ndani ya bodi ya wakurugenzi ,hapa kuna mgogoro ambao unapaswa kuatatuliwa kwa wakati ili kunusuru kiwanda hiki” Alisema Lema

Naye Mbunge wa Singida Mjini Musa Sima wamesema kuwa uamuzi huo wa Tanesco kununua transfoma za nje ya nchi unazorotesha ukuaji wa viwanda vya ndani na kukiuka adhma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda nchini kwani ni vigumu kukuza viwanda wakati bila kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa za nje.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Vicky Kamata na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dalali Kafumu wameitaka serikali kuchukua maamuzi juu ya suala hilo la Tanesco ili kulinda viwanda vya ndani viweze kuchochea maendeleo ya Taifa.

Meneja Mkuu wa Tanaleck Zahir Salehe ameiomba serikali irekebishe sheria za manunuzi ili zitoe kipaumbele kwa viwanda vya ndani viweze kukua na kutoa ajira nyingi hivyo kukuza pato la nchi.

IL.JPG
 
Naunga Mkono Hoja, Tanaleck ni kiwanda Ambacho kilifanya kazi nzuri sana na nikiwanda Ambacho kinazalisha vifaa bora kabisa barani Africa, nakumbuka kipindi cha miaka ya nyuma tulikua tunatumia majiko ya umeme ya Tanaleck na yalikuwa ni moto wa kuotea mbali.

Tatizo la taifa hili katika Awamu ya Mzee mrisho, walizaliwa Michwa Ambayo ilikuwa ni Hatari kwa mustakabali wa Nchi.

Hawa walikuwa ni Wazee wa 10 pacent, ndio walio litumbukiza taifa kwenye ugonjwa wa ufisadi uliokuwa unalipeleka taifa hili kaburini.
 
Sasa kwanini hawanunui hapo?
Huenda tatizo likawa ni Sheria ya Manunuzi. Naona hapo Mkrugenzi wa TANLEC ameomba sheria irekebishwe. Huenda transformer zao ni ghali kulinganisha na za nje. Kwa mujibu wa sheria ya manunuzi kama quality ni sawa basi wanaangalia bei ambayo ni ya chini.
 
Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua jipu shirika la umeme Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi licha ya kumiliki asilimia 20% ya hisa katika kiwanda cha Tansfoma cha Tanalec kilichopo jijini Arusha .

Kamati hiyo ya Bunge imebaini hayo wakati wa ziara yao ya kutembelea viwanda jijini Arusha ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa viwanda ambapo Wabunge hao wameshangazwa na kitendo cha Tanesco kutonunua transfoma katika kiwanda hicho ambazo huuzwa katika nchi jirani za Kenya ,Zambia Malawi na Burundi.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo alisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa Tanesco ambao ni wamiliki wa Tanalec na wako katika wakurugenzi wa bodi lakini bado wanaagiza transfoma nje ya nchi suala ambalo linapaswa kutazamwa kwa umakini na kupatiwa majibu.

“Tunashindwa kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni cha kwao na wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba yuko ndani ya bodi ya wakurugenzi ,hapa kuna mgogoro ambao unapaswa kuatatuliwa kwa wakati ili kunusuru kiwanda hiki” Alisema Lema

Naye Mbunge wa Singida Mjini Musa Sima wamesema kuwa uamuzi huo wa Tanesco kununua transfoma za nje ya nchi unazorotesha ukuaji wa viwanda vya ndani na kukiuka adhma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda nchini kwani ni vigumu kukuza viwanda wakati bila kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa za nje.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Vicky Kamata na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dalali Kafumu wameitaka serikali kuchukua maamuzi juu ya suala hilo la Tanesco ili kulinda viwanda vya ndani viweze kuchochea maendeleo ya Taifa.

Meneja Mkuu wa Tanaleck Zahir Salehe ameiomba serikali irekebishe sheria za manunuzi ili zitoe kipaumbele kwa viwanda vya ndani viweze kukua na kutoa ajira nyingi hivyo kukuza pato la nchi.

View attachment 335010
wananunua india kwenye mabehewa mabovu..tumbombele kwanza. kama nguzo kama mabehewa..teh teh
 
mi jamni nalia mbona kia ukichja yanaibuka madudu? mi nataka nimtuyme CAG, kwenye jengo la Kakwete, akaodit, sio siri.
 
Vicky Kamata...

Wananchi wa nchi hii tunadharaulika sana. Sasa huyu dada ana sifa gani zilizomfanya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara? Kweli katika wabunge wote huyu ndiye waliona anafaa kushika hiyo nafasi?
 
Kiwl firmsanda hiki kilikuwa kina "export" bidhaa zake nchi za nje.Kwahiyo nafikiri bidhdaa zake zina ubora wa kimataifa.
ok, labda tanesco walitangaza international completion bidding where by local entities compete with international firms, usually there scale of margins preference provision to local firms
 
Wananchi wa nchi hii tunadharaulika sana. Sasa huyu dada ana sifa gani zilizomfanya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara? Kweli katika wabunge wote huyu ndiye waliona anafaa kushika hiyo nafasi?
ubunge sio profession
 
Hiyo ilikuwa last month only waziri akitoa maagizo hayo hayo sasa embu jiulize kuna monitoring zipi kati ya wizara na TANESCO kuhakikisha compliance?

Imagine supervision of other TANESCO expenditures na serikari inawapa ruzuku karibu ya billioni 500 kila mwaka. Systems za serikari ni mbovu sana kwenye usimamizi wa haya mashirika ndio sababu ya matumizi ya ovyo pia na ubadhirifu.
 
Sio kweli bidhaa ya

Back
Top Bottom