Wabunge wataka rais anunuliwe ndege nyingine

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Date::4/1/2010Wabunge wataka rais anunuliwe ndege nyingineExuper Kachenje

WAKATI kelele kuhusu gharama za ndege ya rais zikiwa hazijapata majibu ya kuridhisha, Kamati ya Bunge ya Miundombinu sasa inataka mkuu huyo wa nchi anunuliwe ndege nyingine mpya kwa ajili yake na viongozi wengine.


Wabunge hao wanataka ndege hizo zitumike kwenye majanga ya kitaifa.Wabunge wa kamati hiyo walitoa ushauri huo licha ya kupewa taarifa fupi ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), iliyoeleza kuwa taasisi hiyo inaidai serikali deni linalofikia Sh6 bilioni.


Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Missanga alibainisha hayo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam ambako vikao vya kamati mbalimbali za bunge vinaendelea.


"Labda niseme 'observation', yetu (tulichokiona), sijui nisemeje lakini, haya ni ya ndani. Kwa kifupi tumeridhishwa na ufanisi wa wakala hasa suala la usalama. Kwa upande wa ushauri tumeishauri TGFA kuwe na helkopta itakayotumika na viongozi wa kitaifa, kuwezesha kutua hata pasipo na uwanja wa ndege," alisema Misanga.


Alifafanua kuwa pamoja na helkopta, tunashauri serikali inunue ndege mbili ili ziwe mbadala wa ndege nyingine mbili aina ya Fokker 28 na Fokker 50 ambazo ni za siku nyingi.


“Kwa mujibu wa taarifa ya TGFA tumegundua kuna ndege mbili za siku nyingi, Fokker 28 na Fokker 50, ingawa bado zinafanya kazi vizuri, ushauri wa kamati ni kuwa serikali inunue ndege nyingine ‘kureplace’ (mbadala wa hizo) hizo kwani zimetimiza muda wa kubadilishwa," alisema Missanga.


"Tunatahadharisha katika ununuzi huo isitokee kama ilivyokuwa kwa ndege ya rais. Zinunuliwe zinazoweza kutua viwanja vingi kulingana na mazingira ya nchi."


Taarifa iliyowasilishwa na ofisa mtendaji wa TGFA , Keenan Mhaiki inaonyesha kuwa Fokker 28, iliyonunuliwa mwaka 1978, ina zaidi ya miaka 30 na kwamba imeruka asilimia 48 ya saa zilizotarajiwa kitaalamu.


Pia Fokker 50, iliyonunuliwa mwaka 1992, imeruka asilimia 101 ya saa ilizopangiwa kuruka na wataalamu.Kwa mujibu wa Mhaiki, TGFA ina ndege nyingine aina ya PA31 Navajo ambayo imeruka kwa saa 28.40 huku ndege ya rais aina ya Gulfstream ikiwa imeruka kwa asilimia 37 ya saa ilizopangiwa kuruka hadi kufikia Machi 2010.


Kuhusu ndege ya rais, Missanga alisema kamati yake ilifuatilia utendaji wake wa kazi na kwamba wakala hao wameihakikishia kamati kuwa inafanya kazi vizuri na kuendelea kutumika kwa safari mbalimbali za rais, ikiwemo ya hivi karibuni ya Uturuki.


Mtendaji huyo wa TGFA alisema ndege hizo zimefanyiwa matengenezo ya kawaida na makubwa kufuatana na taratibu, zipo katika hali nzuri kuweza kuruka, lakini akasema ndege moja kati ya mbili aina ya Fokker ipo nchini Uholanzi kwa matengenezo ya siku 78 na itarejea nchini Juni mwaka huu.

Alibainisha kuwa ufinyu wa bajeti unakwamisha kufikia malengo ya chombo chake na kwamba serikali haijalipa deni la zaidi ya Sh6,250,743,663.82.
Kutokana na deni hilo, kamati ya miundombinu imeitaka serikali kuonyesha mfano kwa kuilipa TGFA fedha hizo ili iweze kuboresha huduma zake.
 
Back
Top Bottom