Wabunge wataka mgodi North Mara ufungwe, Ewura yapewa miezi mitatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wataka mgodi North Mara ufungwe, Ewura yapewa miezi mitatu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,237
  Likes Received: 5,621
  Trophy Points: 280
  Na Kizitto Noya, Dodoma

  BAADHI ya wabunge wameitaka serikali kuufunga mgodi wa North Mara ulioko Tarime mkoani Mara, unaomilikiwa na kampuni ya Barrick kwa kuwa unahatarisha mazingira na fya za binadamu.

  Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2009/10 jana, wabunge hao walisema mgodi huo unapaswa kufungwa kuepusha madhara kwa wakazi wanaouzunguka.

  Miongoni mwa wabunge hao ni Dk Harrison Mwakyembe (Kyela CCM) aliyeshauri mgodi huo ufungwe kuipa fursa kampuni hiyo ya Canada kurekebisha mifumo yake ya taka na serikali kuweka mipaka ya kuutenganisha na makazi ya watu.

  Dk Mwakyembe alisema kampuni ya Barrick ina rekodi duniani kote ya uchafuzi wa mazingira na kwamba iliwahi kufukuzwa nchini Australia kwa kushindwa kuhifadhi taka zake.

  “Pamoja na mapenzi tuliyonayo kwa wawekezaji, 'this time' (safari hii) dhidi ya Barrick, tuufunge mgodi wa North Mara mara moja,” alisema Dk Mwakyembe.

  Aliwataka wabunge wanaotokea karibu na eneo ulipo mgodi huo kuwahamasisha wananchi wafungue kesi mahakamani ili kampuni ya Barrick iwalipe fidia.

  “Hakuna sababu ya kuwaogopa wawekezaji kama wakwe. Wakazi wa kijiji cha Nyakabale wamepata shida hii kwa muda mrefu. Mimi nawaomba wabunge kuwahamasisha wananchi wafungue kesi kwani hatuwezi kuwasaidia wananchi hao kwa kuzungumza majukwaani,” alisema.

  Kauli hiyo ya Dk Mwakyembe iliungwa mkono na mbunge wa Ukerewe, Dk Getrude Mongella aliyetaka serikali kuwa makini na wawekezaji ili wasiharibu mazingira na kuhatarisha afya za wananchi.

  “Sumu ya madini ni jambo baya sana, madini yatatumaliza na tukianza kujali fedha na kusahau wananchi, hiyo ni 'blood money' (fedha inayotokana na damu). Mgodi huo ufungwe 'immediately' (mara moja),” alisisitiza.

  Kwa mujibu wa Dk Mongella mbali na athari wanazoweza kupata watu wanaoishi karibu na mgodi huo, sumu aina ya Zebaki inayotiririshwa majini na kuliwa na samaki inaweza kumwathiri mtu anayekula samaki hao.

  Hata hivyo mkurugenzi wa kampuni ya Barrick Deo Mwanyika alipuuza ushauri huo wa wabunge akisema hauna msingi kwa kuwa kilichotokea Barrick ni ajali kama ajali zingine.

  “Huwezi ukazungumzia kuufunga mgodi kwa sababu ya ajali iliyotokana na hujuma vinginevyo utafunga biashara zote katika nchi hii. Hujuma ile haina tofauti na hujuma ya kuiba miundombinu,” alisema

  Hujuma dawa yake ni kuwafikisha wahusika mbele ya sheria, lakini pia hawa waheshimiwa wanazungumzia historia kwani tatizo hilo halipo tena,” alisema.

  Katika mchango wake, Dk Mwakyembe pia alizungumzia tatizo la mafuta kuchanganywa na maji au mafuta ya taa na kuipa Mamlaka ya Udhibiti ya Nishati na Maji (Ewura) miezi mitatu kulimaza kabla hajaleta hoja binafsi bungeni kutaka watendaji wote wa mamlaka hiyo wawajibike.

  “Kuhusu suala hilo, nawalaumu Ewura kama mnashindwa kazi kwa nini msiwapishe wengine. Nawapa miezi mitatu nitakuja na hoja hapa bungeni kutaka makae pembeni. Kama mshiko unawasumbua katika hili kuweni makini,” alisema

  Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe alisema madini ya uranium yanayotarajiwa kuanza kuchimbwa nchini hayatakuwa na maana kama viongozi hawataacha ubinafsi na kuweka maslahi ya taifa kwanza

  “Kuanza kuzalisha uranium nchini ni jambo jema, lakini mimi naonya kwamba kama sisi viongozi hatutabadilika kwa kuacha ubinafsi na kuweka vipaumbele vya taifa kwanza, ni bora madini hayo tusiyachimbe, yaendelee kubaki ardhini,”alisema na kuongeza: “Uranium inaweza kuleta Richmond, rada na EPA nyingineni kama tusipokuwa waadilifu. Tukifikia hapo, ni bora tukayaacha madini hayo ardhini kama waanzilishi wa taifa hii walivyotuachia kuliko kuchimba bila faida kwa taifa,”.
   
 2. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyo Mwanyika mbona anaongea kana kwamba yuko sayari nyingine. Suala la mgodi wa North Mara limekuwa likisikika kila mara, wananchi wanaoishi karibu na mgodi huo wamekuwa wakilalamika kila mara lakini viongozi wetu ambao wamejawa na roho za kifisadi wanajifanya hawaoni wala kusikia. Nafikiri ili kuweza kuwabana waendeshaji wa mgodi huo ni vyema ufungwe ili wajipange upya, suala la kuwafungulia mashitaka kwa ajili ya kudai fidia ni muhimu pia, wabunge na wanasheria wasaidieni wananchi hao ili haki ipatikane vinginevyo mafisadi wataendelea kujineemesha tu.

  Kuhusu EWURA naona mamlaka hiyo imeshindwa kazi na sasa utendaji wake hauna tofauti na wafanyabiashara wengine wa mafuta. Kwa ujumla EWURA ni mzigo kwa Taifa na ninaamini mamlaka hii iko kwa faida ya wakubwa wachache na namna wanavyofanya kazi na kukusanya mapato yao ni mzigo kwa raia wa kawaida kwani imekuwa ikiongeza bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo ziko kwenye mamlaka yao (umeme, maji, mafuta ...)
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mwanyika si mwanasiasa...ni mwanasheria....na yuko kwenye bussiness ya uchimbaji na kwa maelezo yake.Yuko sawa sioni tatizo...unajua ukiongea bungeni ukataja jina barrick watu masikio yanawasimama...sikujua kama mwakyembe nae angeweza kuongea kwenye hili...badala ya uko kwao kuna matatizo gani.Ukweli ni kwamba kama ile ni hujuma na tatizo halipo tena...basi hata mifuniko ya sewage system dar inayo ibiwa na kuacha wazi mashimo barabarani....

  Tufunge biashara ya vyumba chakavu nchi nzima.Huo ndio ukweli ambao haujachanganyikana na siasa ambao watu hawataki kuusikia wanataka kusikia.
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu....
  [​IMG]

  hio ndio faida ya gold kwa watz.....soma..

  http://protestbarrick.net/downloads/North%20Mara%20Pollution%20Report.pdf

  Protest Barrick*:*Index
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,237
  Likes Received: 5,621
  Trophy Points: 280
  uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii jamani jakaya hiyo gold mbona inatutesa hivyo watanznia
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Halafu hata faida yake kwa huyo mtanzania wa kawaida ambaye ndiye m,wathirika namba moja hatuioni.
   
 7. N

  Ndaga Senior Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 164
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Buswelu,
  Jua jambo moja tu, hatukatai uwekezaji katika ngazi yoyote katika nchi yetu, kinachosemwa hapa ni uhalali wa kupoteza uhai wa watu kwa jambo linaloweza kuzuiwa,ni lazima tuwe na utu wa kiutendaji ili ubinadamu uchukue nafasi katika harakati zote za kimaendeleo,ikiwa kuna hali ya mwekezaji kutokujali utu na ubinadamu na kwakuwa wapo wanaoweza kuwekeza na kukidhi utu na ubinadamu basi tuna haja gani na mwekezaji huyo anayejali maslahi yake akituachia makovu ya uhasama kati ya mwananchi na viongozi wetu,hilo ndilo linalopigiwa kelele.
  Nani hataki uwekezaji? Hata mimi hata wewe Buswelo unapenda pia,lakini atakubali awekeze katika hatari? Nani yuko tayari apoteze maisha yake ili mwekezaji afanikiwe? Je wewe (Buswelo) uko tayari ufe kwa ajili ya mwekezaji itakapobidi kama utakuwa katika eneo la uwekezaji?
  Unajua hawa ndugu wa North Mara wako mbali nasi kimaeneo, na athari zake sisi tulio mbali hazitupati katika hali halisi, yamkini ndiyo maana watu wenye mitazamo yako wamezungumza hivyo bila kutazama ukali wa jambo lenyewe, Mwanyika lazima atetee hivyo maana haathiriki na sumu hiyo wala hataweza kuathirika, maana akipata malaria tu anapelekwa Nairobi kutibiwa, sasa atajueje maji yale yanaathiri nini katika jamii fukara kabisa inayotaabika.
  Mitazamo na tafakuri ni nzuri endapo zitabeba maudhui ya kiutu na kibinadamu na kutazama kama kweli ‘’ Biashara ni lazima ifanywe tu hata kama watu wahusika wataathirika na hiyo biashara’’ kwani biashara ni kuuwa watu? Msifanye watanzania hatuwezi kuchimba madini! Tunaweza ni suala la muda tu! Kama siyo sisi basi ni kizazi chetu kijacho cha 2,3 au cha 4 kitakuja chimba.

  Mungu wa Mbinguni atusaidie.

  Joune,
  Ndikupasya Buno Malafyale anganile Kangi ambokile.
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Unajua sio kuamka na kufunga tu....tatizo si limedhibitiwa?Nikiwa na maana kuwa huo mtiririko haupo tena!!Ingekuwa wanaendelea kutiririsha maji kwenda kwa wananchi...pure ingekuwa another side of the story.

  Lakini mie ninacho sema hapa ni kuwa kufunga sio solution...Mwakyembe jana anasema ufugwe Geita na North Mara?Inaingia akili kweni mnafikiri kwa bongo hili linawezekana?Ikiwa waziri anakwenda na ujumbe wake kwenye migodi hii,barrick wanaghalimikia kila kitu,na posho pia ya kuwaita uko....kisha mtu waziri anasema watanzania wezi?>Ndio maana vyeo vingi wanawapa wazungu?!!!!!!

  Angalia hili katika mapana yake...sio kuishi kulia lia tu hapa mgodi ufungwe...angalia economic impact kama sasa tu mtikisiko wa uchumi vijana wako mtaani baada ya kampuni nyingi za utafiti kufungwa...hao hao vijana waambie kuna kazi ... utawakuta kwenye malango ya migodi wakisubuli kwenda kufanya kazi kwenye sehemu hizo.Ndaga....katika structure mbovu ya mgodi au migodi tanzania basi North Mara inaongoza....ni 10m mpaka 1km kuna wananchi wanaishia karibu na mgodi...walijaribu kuombwa kuhamishwa kwa malipo...baadhi walikubali...lakini pesa anakabidhiwa mume anakwenda kuoa kwingine. mwanamke hapati kitu na hakubali kuhama....wewe kama wewe utamlipa the same amount na mke?

  Kuna mambo mengi sana ambayo si wananchi wa kawaida hatuyajui uku tuliko....ambayo yanaendelea kwenye migodi...ukitembelea Resolute ni almost 25Km kutoka Nzega mjini...vijiji vinavyo zunguka kama mwaluzwiro..ni 2km from mine.Geita the same,tulawaka ndio porini..ndio maana matatizo mengi unayasikia North mara...na hii wazee haikuanza leo ni toka enzi za africa mashariki Gold mine,Placer dome ambayo ilinunuliwa na barrick...so it was too laite kuhamisha watu baada ya uchimbajiwa miaka kama kumi...barrick ndio wakachukua.
   
 9. N

  Ndaga Senior Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 164
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Nadhani umemnukuu visivyo Mwakyembe, Nanukuu ‘’ alisema; ni wakati muafaka kwa serikali kufunga mgodi wa North Mara hadi hapo utakaporekebisha mfumo wa maji taka ya kemikali yanayotiririka na kudhuru wananchi wa eneo hilo’’
  Sasa tatizo liko wapi? Ndiyo lazima wafunge ili warekebishe! Nasisitiza haijalishi mwekezaji yuko mjini au kijijini au karibu au mbali na jamii au wamelipwa fidia au hapana siyo chachu ya kuwadhuru! Utu na ubinadamu vichukue nafasi ya kwanza.
  Kutokuwa na uwezo wa kutafiti na kuchimba madini siyo mwisho wa safari,ukifika wakati yatachimbwa na opportunities nyingine za wananchi kujiwezesha zitapatikana! Kwani migodi hiyo kabla walikuwa wanafanya nini?

  Mungu atupe kuona.
   
 10. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
Loading...