Tetesi: Wabunge wataka kupewa namba maalum za magari

Hayo yote wanayajua ila hao wanaoongoza nchi katu hawawezi kufanya hivyo kwasababu nawao ni wanufaika wa hizo mambo za kuumiza wananchi kwa maslahi binafsi.Aliyeanzisha utaratibu wa siasa ndio iongoze serikali alikosea sana.maana wanasiasa wametumia hio nafasi kujineemesha.Hadi kufanyike mabadiliko ya dola ndio tutakapoweza kujadiliana kurekebisha huu mfumo maslahi.
Kweli kabisa aisee naona sasa posho zimezidi hadi wamebaki kugonga meza tu kila kitu kwao sawa tu
 
Zamani wakati wa uspika wa Adam Sapi Mkwawa ilikuwa kama hivi ulivyoshauri. Siku hizi ndio maana kiongozi anajiuzuru u-DC au hata RC ili akagombee ubunge. TUJITAFAKARI KUNANI ?
Dah kweli kabisa yan imekua maslahi mbele matatizo ya wananchi nyuma yan hadi ma proffessor washashtuka kua maisha siku hizi yapo kwenye siasa na sio pengine ndio maana wote wamehamia kwenye kugonga meza
 
Ndio wanachojua hawa kenge, yaani badala ya kuhangaika kuishauri Serikali iondokane vipi na mfumuko wa bei na maisha magumu kwa wananchi wao wanawaza namba sijui saluti, yaani sijui sisi nani alituroga , kimsingi tumepigwa akikwambia mtu eti anaenda kule kwaajili ya kuwawakilisha wananchi muulize hao wananchi ni wa wapi kama sio wananchi wa nyumbani kwake na tumbo lake kubwa. Ovyo kabisa hawa , na ndio wanataka Bunge lirudishwe live ili wawaonyeshe wananchi upuuzi huu? Duh haya buana yetu wengine macho tu.
 
Ndio wanachojua hawa kenge, yaani badala ya kuhangaika kuishauri Serikali iondokane vipi na mfumuko wa bei na maisha magumu kwa wananchi wao wanawaza namba sijui saluti, yaani sijui sisi nani alituroga , kimsingi tumepigwa akikwambia mtu eti anaenda kule kwaajili ya kuwawakilisha wananchi muulize hao wananchi ni wa wapi kama sio wananchi wa nyumbani kwake na tumbo lake kubwa. Ovyo kabisa hawa , na ndio wanataka Bunge lirudishwe live ili wawaonyeshe wananchi upuuzi huu? Duh haya buana yetu wengine macho tu.
Yan ndugu yangu fikiria hawa kama
Kweli ni wawakilishi wa wananchi wangepitisha ile sheria kandamizi ya mifuko ya hifadhi ya jamii hasa kwa watu wa sector binafsi ambao sio pensionable eti mtu kamaliza mkataba wake aje apewe hela yake baada ya kufikisha miaka 60 kweli?? Bei za chakula zinapaa serikali ipo kimya wenyewe wanagonga meza tu?? Nchi nyingine upuuuzi huu hawavumilii
 
Hakuna haja ya kuwa na mwakilishi ambae anawaza kubadilishiwa namba za Gari Ili asisimamishwe na trafiki.
.
Ila Hawazi Jinsi Gani atatumia uwezo wake kuwakomboa wananchi wa Jimbo lake.
.
Hakuna haja ya kuwa na wabunge wa aina Hii
 
Hakuna haja ya kuwa na mwakilishi ambae anawaza kubadilishiwa namba za Gari Ili asisimamishwe na trafiki.
.
Ila Hawazi Jinsi Gani atatumia uwezo wake kuwakomboa wananchi wa Jimbo lake.
.
Hakuna haja ya kuwa na wabunge wa aina Hii
Ndio wapo!

Sasa tufanyaje?
 
Baada ya muda wataanzisha mjadala wa kuongezwa kwa posho wanazolipwa kutokana na mfumuko wa bei.
 
Anaandika Thadei Ole Mushi

Wabunge wa CCM leo kwenye Group lao la kibunge wamejadili na kukusudia kupeleka hoja bungeni wapewe privilege ya magari yao kuwa na Special number.

Sababu kubwa ya kutaka hilo ni kuwa wanasema matrafiki wanawasumbua sana njiani na hawataki usumbufu huo. Kuna mambo kadhaa nayaona hapa:

1. Tayari wameshajiona kuwa hao ni Raia Special nchini. Yaani wanajiondoa kwenye kuwa mwananchi wa kawaida kuwa VVIP. Wanataka kujitofautisha na wananchi wa kawaida.

2. Trafiki hawezi kukusimamisha kama huna makosa, tafsiri ya maombi haya ni kutaka kuhalalisha kufanya makosa.

3. Kila kundi likiomba Special number hapo barabarani kutakuwa ni vurugu tupu.

4. Nafikiri badala ya kujiombea wao Special number wangetuombea Sisi waalimu na Madaktari ambao huwa wanawahi shughuli nyeti za kijamii. Hebu fikiria Daktari anayemuwahi Mgonjwa asife anasimamishwa halafu mbunge anayekwenda kwa Mchepuko wake hasimamishwi.

5. Wabunge kwenye group siku nzima wanajadili kupewa Plate number Special wanaacha kubangua bongo wanaishauri vipi Serikali kutatua tatizo la mafuta ya kula na ya Petrol nchini ambayo yamepandisha vya kutosha maisha ya wananchi.

Wana Privilege nyingi sana hasa maslahi yao lakini hawajaridhika wanajipigania binafsi kuliko kuwapigania wananchi.

1. Mbunge hulipwa mshahara kwenye scale ya LSS (P) 2 ambayo mshahara wake ni Shilingi 4,600,000.

2. Atalipwa posho ambazo kwa Mwezi hufikia Shilingi 8,292,000 katika mchang'anuo ufuatao.

✓Atalipwa posho Kwa ajili ya mafuta ya gari yake Shilingi 3,750,000.

✓Atalipwa Posho Kwa ajili ya Matengenezo ya Gari yake Shilingi 1,500,000.

✓Atalipwa Posho inayoitwa (Posho ya Mbunge na matumizi mengine jimboni) Shilingi 1,000,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu ya siku 10 kama atajisikia kwenda Jimboni Shilingi 450,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu kwa Wasaidizi wake watatu Kwa siku kumi atakazokuwa jimboni Shilingi 900,000 hapa kama atajisikia kwenda Jimboni au kwa mchepuko Dar

✓ Atalipwa Posho ya watumishi watatu kama atajisikia kuajiri (Mhudumu wa Ofisi yake, Katibu wake, na Dereva) katika mchang'anuo ufuatao.

3. Katibu wake Shilingi 352,000 Mhudumu 170,000, Dereva 170,000. Jumla Shilingi 692,000. Hapa ni kama atajisikia kuajiri sio lazima.

Jumla ya Fedha zote zinafika Shilingi 12,892,000.Fedha hizi zote zinaingia kwenye account yake Mbunge.

Hii ni nje ya Posho za vikao vya Bunge.

2. Katika vikao vya budget mathalani Mbunge hulipwa Shilingi 240,000 kama sitting allowance, Shilingi 120,000 kama posho ya kujikimu kwa hiyo kwa siku ni Shilingi 360,000.

Bunge la budget pamoja na vikao vya Kamati kwa kalenda ya Bunge la budget la 2021/2020 lilianza na vikao vya Kamati Tarehe 6 march na kuendelea na Bunge lenyewe lililoisha June 30. Jumla ya siku zote ukitoa Jumapili ni siku 97 hizi siku ukizidisha mara 360,000 anazopata kwa siku unapata jumla ya Shilingi 34,920,000. Hii ni Fedha ya Bunge la budget tu. Hapa sijajumlisha na posho za Vikao vya bunge la mwezi wa 11.

Sifa kubwa ya kuwa Mbunge ni kujua kusoma na Kuandika. Nisaidie ku share kila mwananchi aone anachojadili mbunge wake leo.

Ole Mushi
0712702602.
Usishangae na Mama naye akawakubalia kwa kumtumia speaker memo. Yaani hii nchi huko tunakokwenda sijuwi tutakuwaje.
 
Madaraka Ya Kulevya Wanadai Mpaka Vitu Vya Hovyo
Number Za Nini Maalum, Kwa Jambo Gani Hasa
 
Back
Top Bottom