Wabunge wataka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ivunjwe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Bunge la 12, mkutano wa 9 kikao cha kwanza. Wabunge kadhaa wakichangia muswada wa elimu wametaka bodi ya mikopo ya elimu ya juu ivunjwe kutokana na utendaji usioridhisha.

Baadhi ya mambo waliyoyataja ni pamoja na Bodi ya Mikopo kuchelewesha mikopo au kutoa mikopo kwa ubaguzi.

Wabunge hao wameonesha umuhimu wa elimu na hali za watanzania ambao ni vigumu sana kujilipia ada. Mbunge mmoja ametoa wito kwa Serikali kuwasomesha bure wanafunzi wanaopata divisheni one ili kuwapa motisha
 
Watu pale wanapiga hela kama vile waliziweka. Full janja janja. Boss wa pale full kula Raha. Daily safarini Nje huku V8 anazunguka nalo bi Mdogo Dodoma.
NB: Kuna Mkurugenzi wa Fedha kaajiri ndugu yake kama Secretary safari zote Lazima amuweke Tena anakua kwenye V8 wakati boss kapaa na Ndege anaenda kupokelewa KIA/Mwanza/Dom (airport)
 
Hapo ni zaidi ya urefu wa kamba mzee
 
Nilishashauri muda mrefu hii bodi ifutwe, haina msaada wowote kwa elimu ya vijana wa kitanzania hasa watoto wa wanyonge badala yake imekuwa kero kwa kuwakosesha fursa ya elimu na kubambika madeni makubwa kwa hawa vijana, kijana anaanza kazi na deni la mil. 30......hii haiwezi kuwa sawa.
 
Kwahiyo Bodi ikivunjwa ndio tatizo litakuwa limetatuliwa??

Wabunge wa mihemko.
 
Nilishashauri muda mrefu hii bodi ifutwe, haina msaada wowote kwa elimu ya vijana wa kitanzania hasa watoto wa wanyonge badala yake imekuwa kero kwa kuwakosesha fursa ya elimu na kubambika madeni makubwa kwa hawa vijana, kijana anaanza kazi na deni la mil. 30......hii haiwezi kuwa sawa.
Bodi inafutwa na nani?
Watu wenye uwezo wa kumgomea waziri huoni kama wanaweza wakaambiwa bodi imevunjwa wakasema "HAPAVUNJWI BODI WALA HATOKI MTU HAPA"

Hapana chezea HESLB wewe
 
Ukiwaona maboss wa bodi hiyo sasa
Wmenenepeana sanaa matumbo makubwa kama mapipa

Ova
 
Back
Top Bottom