Wabunge watadhalilishwa kwa kipigo mpaka lini?

batazoba

Member
Apr 3, 2012
58
29
Tulishuhudia kipigo kwa wabunge wa upinzani wa jimbo la ilemela Mhe.Highness Kiwia na Mbunge wa ukerewe Mhe.machemli walivyo jeruhiwa mpaka kufikia kulazwa ktk hospitali ya rufaa ya taifa muhimbili.swali la kujiuliza ni kwanini wamekuwa wakipigwa wabunge wa upinzani kiasi ambacho hupata majeraha na kuhatarishiwa maisha yao kama ilivyo tokea jana kwa Mbunge kijana pengine kuliko wote bungeni,mbunge wa arumeru Mhe.Joshua Nassari.hata hivyo ukiangalia ktk chaguzi ndigo za madiwani sehemu nyingi ambapo chama tawala kinapata upinzani mkubwa ndipo vurugu na hata kutarisha maisha ya wananchi kwa kutumika kama vile risasi za moto tunaelekea wapi jamani kwani tusifanye uchaguzi usiokuwa na vitisho wala vurugu ili tupate chaguo la wananchi?mpaka lini wabunge watakuwa wakipigwa tu wakati wapiga kura wao wamesimama tu wakiangalia wawakilishi wao wanadhalikishwa?
 
Back
Top Bottom