Wabunge "Wastaafu" Kumwaga Vijisenti kwa Wingi Majimbonii, Nini Kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge "Wastaafu" Kumwaga Vijisenti kwa Wingi Majimbonii, Nini Kifanyike?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Jul 19, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wapendwa wanaJF,
  Wabunge waliomaliza ngwe ya kwanza ya awamu hii ya nne wanaranda sana majimboni kumwaga vijisenti ambavyo yumkini wamelambishwa toka Bungeni baada ya kutumikia Bunge kwa miaka takriban mitano. Ili kuepusha hali hiyo, je, siku zijazo, nini kifanyike kati ya hivi vifuatavyo?
  a) Kuweka ukomo wa ubunge (eg vipindi viwili tu) au,
  b) Kuwalipa mafao yao baada ya uchaguzi unaofuata (km mafao yao yangelipwa baada ya uchaguzi wa Oktoba, 2010) au,
  c) Kupunguza mafao yao Bungeni (maana imeonekana kuwa Ubunge au siasa kwa ujumla ni dili) au,
  d) Kuongeza adhabu dhidi ya wala rushwa (eg wachina wanawapiga shaba wala rushwa) au,
  e) Kutenganisha siasa na biashara au,
  f) Kufufua Azimio la Arusha na hatimaye kurudisha MIIKO YA UONGOZI au,
  g)....
  Tujadili!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ningeweka mada za udaku wachangiaji wangefikia 20 mpaka sasa!
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kupunguza mafao yao Bungeni (maana imeonekana kuwa Ubunge au siasa kwa ujumla ni dili)
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Buchanan,

  Ningependekeza vipindi viwili kwasababu wapo watanzania wengi wenye uwezo mkubwa wa kutuwakilisha vyema mjengoni.Tuliweza kuweka ukomo wa kipindi cha urais sijui ni kwanini tushindwe kuweka ukomo kwenye ubunge.Tumezalisha wabunge wa maisha majimboni si kwasababu ni wachapakazi wazuri bali mfumo uliopo unawapa urahisi kurejea tena kwenye ubunge.Mfano mzuri unawekwenda kugombea jimbo x na mbunge aliyelipwa mafao mazuri ambae haitaji kuandaa fund raise kukabiliana na gharama za uchaguzi.

  Nadhani ukomo wa ubunge ni suluhisho la kuondokana na wabunge aina ya Kimiti,Mzindakaya,Makweta na nk.
   
 5. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  HIvi unajua ktk vitu vinavyonishangaza siku zote ni hili suala la kutafuta kura za kutuwakilisha kwa njia za rushwa...hivi kama kweli unataka kwenda bungeni kutuwakilisha kwanini sasa unatupa fedha?sisi ndio tulipaswa kukupa wewe fedha kwa kuwa tunakutuma...Hapo dawa ni moja tu, malipo ya wabunge yawe sawa na kima cha chini cha mishahara ya watumishi wengine wa serikali na kwa hakika hapo tutafahamu kama kweli watu hawa wanalilia kwenda kutuwakilisha au kujiwakilisha na kujineemesha!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri, lakini je ni aani atapitisha sheria ya namna hiyo kuwabana wabunge? Unadhani kuwa bunge hilo hilo la Tanzania linaweza hata kupoteza muda wake kujadili kitu cha namna hii badala ya kwenda kula maraha hapo kwenye mehoteli ya Dodoma?

  BTW: Kwa marekani, Raisi anaweza kutunga sheria zake bila kuzipitisha bungeni; sheria inayotolewa na raisi hujulikana kama executive order. Najua kuwa kuna mipaka katika utoaji wa executive orders hizo, lakini ikishatolewa inakuwa ni sheria kamili kama iliyotolewa na bunge. Mara nyingine kama order hizo zinapingwa na raia, basi itabidi wafungue kesi mahakama kuu ambayo ndicho chombo pekee kinachoweza kuzitengua. Nakumbuka mwaka 1996 kulikuwa na kesi ya kupinga excutive order moja iliyotolewa na Clinton.

  Je Tanzania napo rais wetu ana legal powers za kutoa executive order? Na kama anayo, basi ndiye mtu wa kuweza kufanya hivyo.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180

  Wanatakiwa waitunge wao, Rais hawezi akatoa Executive Order mpaka apewe mamlaka na Sheria fulani ambayo inatakiwa itungwe na Bunge, kwa hiyo mambo yatakuwa ni yale yale tu! Shinikizo linatakiwa litoke kwa wananchi wenyewe!
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  a) Kuweka ukomo wa ubunge (eg vipindi viwili tu) au,
  Hili nakubaliana nalo kwa sababu moja kuu . Labda waalau itasaidia kutawanya mapato yatokanyo o na siasa katika familia mbali mbali na inawezakuaidia kuondoa mambo ya kurithishana ubunge kama ufalme

  c) Kupunguza mafao yao Bungeni (maana imeonekana kuwa Ubunge au siasa kwa ujumla ni dili) au,
  Hii pia nakubaliana nalo. Hivi iweje mbunge awe na kipatao kuliko mganga mkuu wa wilaya au mkoa, RPC , Au afia Elimu wa Mkoa au wilaya? Kweli Serikali yetu inaoenekana inachochea kutenngeneza kizazi cha wanasiasa zaidi kuliko watendaji. Hawa Hwa wanasiaa watakuja kutuletea vita siku si nyingi. Hivi kuna mbunge yeyote amewahi kupendekeza kuwepo na chombo huru cha kuangalia mafao yao? Nadhani hakuna. Kuna conflict of interest ambiguty na contradiction juu ya suala hili. Na pika ajaye anatakiwa hili suala aliangalia kwa umakini.

  Wakisiamama kuteatea malipo ya marupu rupu yao wanalingansiha na mabunge mengine ya Commonwealth. Imefikia wakati ni Peoples power ndo inayoweza kufanya kazi sababu hata bunge letu haliwakilishi mawazo ya wanachi . watu wakianza kuandamana kwenda mjengoni labda watashtuka.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Sina ujuzi mzuri na protocol za kikatiba lakini serikali kama ina dhamira ya kweli kuputia wizara husika may be wizara ya utawala bora si inaweza kuwasilisha muswada kuomba wabunge waridhie muundo wa ku asses kufanya malipo yao? wabunge wakigoma wanach tutajua wabaya wetu ni nani.
   
Loading...