Wabunge wasiwe wajumbe bodi za mashirika ya Umma

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
2008-04-12

Na John Ngunge, Dodoma


Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyowasilishwa jana bungeni, imependekeza Wabunge waondolewe kwenye nafasi za ujumbe wa bodi za mashirika ya umma.

Kadhalika, ofisi ya CAG imebaini ukiukwaji wa taratibu za Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004 katika ofisi mbalimbali na katika Kitengo cha Kupakia na kupakua Kontena Bandarini (TICTS).


Mapema akiongea na waandishi wa habari jana, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utouh, alisema utaratibu uliotumika kuongeza muda wa mkataba huo kutoka miaka kumi hadi 25 ulikiuka taratibu.


Mbali na kupendekeza wabunge kuondolewa kwenye Bodi za Mashirika ya Umma, pia imependekeza kuboreshwa kwa nidhamu katika matumizi ya serikali.


Mapendekezo mengine kwa mujibu wa Bw. Utouh ni kupitia upya mfumo wa ubakizaji mapato yatokanayo na makusanyo katika mafungu na kurekebisha vipengele vya Sheria vinavyokinzana na kuimarisha ukusanyaji wa mapato utokanao na vyanzo vya ndani.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Bw. Zitto Kabwe, ambaye alihudhuria mkutano huo, aliunga mkono pendekezo la wabunge kuondolewa kwenye bodi za mashirika ya umma.


Alisema kuwepo kwa wabunge katika bodi hizo kunakiuka dhana nzima ya utawala bora na kwamba atahakikisha taratibu zinabadilishwa ili kuwaondoa.


Alisema anafanya mawasiliano na Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, ili watoe tamko kuhusiana na suala hilo ambalo alisema limekuwa likisababisha lawama kwa muda mrefu.


``Kuna Waraka wa Rais unaokataza wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ya umma lakini inashangaza hautekelezwi.

Hata hivyo, sasa kamati yangu itawataka mawaziri walifanyie kazi hili mara moja,`` alisema Bw. Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA).

Alisema hata katika hoja yake binafsi atazungumzia umuhimu wa wabunge kutokuwepo kwenye bodi hizo.


Kwa upande wake, Bw. Utouh, alisema kati ya mashirika na taasisi 91 zilizokaguliwa, 80 zilipata hati zinazoridhisha, 10 zilipata hati zenye shaka na shirika moja lilipata hati mbaya.


Alisema mashirika manne ambayo ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Shirika la Posta Tanzania, Bodi ya Biashara ya Nje na STAMICO, hayakuwasilisha kwa wakala husika makato ya kisheria yanayofikia Sh. bilioni 29.3.


Alisema hali hiyo inaweza kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi wanaohusika wakati wa kudai mafao yao wanapostaafu.


Alisema maagizo ya Rais Jakaya Kikwete, yamesaidia kuboreshwa kwa hesabu na utunzaji wa kumbukumbu katika sehemu nyingi.


Alitoa mfano kuwa halmashauri nyingi mwaka huu zimepata hati zinazoridhisha kulinganisha na mwaka jana.


Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Bw. John Cheyo, alipendekeza muswada wa kuipa nguvu Ofisi ya CAG uwasilishwe bungeni ili iweze kufanyakazi zake kwa ufanisi zaidi.


Alisema walishawahi kutoa pendekezo hilo muda mrefu lakini inashangaza halifanyiwi kazi.


``Huwezi kwenda kumkagua mtu halafu ukamwomba akupe nyenzo za kufanyia kazi, hiyo haiingii akilini hata kidogo,`` alisema Bw. Cheyo, ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki.


Alisema Kamati yake ilikuwa ikiisubiri ripoti hiyo kwa hamu ili iweze kuifanyia kazi.


Ofisi ya CAG iliwasilisha bungeni jana Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na ile ya Ukaguzi wa Serikali Kuu.


SOURCE: Nipashe
 
Naona bwana mdogo Zitto anaonyesha ukali wa makucha yake na meno yake.
Nje anaonekana kama mbwa aina ya Chihuahua kumbe ndani ni Dume kubwa aina ya BullDog.

Way to go Zitto Kabwe.
 
Naona bwana mdogo Zitto anaonyesha ukali wa makucha yake na meno yake.
Nje anaonekana kama mbwa aina ya Chihuahua kumbe ndani ni Dume kubwa aina ya BullDog.

Way to go Zitto Kabwe.

Am sure hii issue kama Zitto ataisimamia CCM will not like it .It will harm them na hasa ukubwa na posho zao .Go Zitto go we are behind you .
 
Naona bwana mdogo Zitto anaonyesha ukali wa makucha yake na meno yake...Way to go Zitto Kabwe.

Ni aibu kubwa kwa CCM kwamba katika wabunge wao wote 270 hakuna hata mmoja mwenye mwamko na uwanaharakati kama wa mbunge mmoja wa upinzani. Na sababu ni kuweka Chama mbele kuliko nchi. Hawaoni hata noma. Juzi Pinda kaulizwa swali na Zitto kuhusu Zimbabwe akamrudishia swali Zitto, 'wewe unaona tufanyeje'!
 
Ningependa kumuunga Mkono Mtoa hoja, maana matatizo ya wabunge kuwepo kwenye Board tunayaona, kama yale ya Siraji Kabyongo Mbunge wa Tabora kuwa kwenye Board ya TRL na Mkataba Mbovu wa RITES, matokeo yake anakuwa hapigani maslahi ya taifa bali ya yeye kupewa hicho cheo au madaraka.
 
Wizara ya Fedha imefanya maamuzi ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanasubiriwa ili kujenga uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa shughuli za serikali kwa kutangaza kwamba wabunge hawataendelea kuwa wakurugenzi katika bodi za taasisi za fedha za umma.

Tamko la wizara hiyo lililotolewa mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ni utekelezaji wa ushauri uliotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati alipowasilisha ripoti ya ukaguzi mwaka jana, akieleza kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi kwa wabunge kuwa wakurugenzi wa bodi za mashirika ya umma ambayo wanapaswa kuyasimamia.

Kutokana na mgongano huo, ripoti hiyo ilieleza kwamba wabunge waliokuwa wajumbe katika bodi hizo walikuwa wanashindwa kutekeleza wajibu wao kama wasimamizi wa shughuli za serikali kwa kuwa wanahesabika kuwa sehemu ya utawala wa mashirika husika.

Ni kwa kutambua umuhimu na maana ya mgawanyo wa madaraka katika kuhimiza uwajibikaji, tunaona kwamba hatua iliyochukuliwa na Wizara ya Fedha kwa kuitikia maagizo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya kuwaondoa wabunge kwenye bodi za taasisi za fedha ambazo serikali ina hisa, ni ya kupongezwa na kuungwa mkono hasa katika kipindi hiki ambacho harakati za kuhimiza uwajibikaji zimekuwa zikipewa umuhimu wa kipekee nchini.

Kwa hali hii, tunafarijika kwamba walau kuna hatua zinachukuliwa katika kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na CAG katika kuongeza uwajibikaji kwa mihimili ya mamlaka ya dola; kwamba sasa wabunge watafanya kazi zao za kikatiba ambazo ni kutunga sheria na kuisimamia serikali katika utendaji wake.

Pamoja na kutambua hatua hizi chanya, tungependa pia kuona wigo wa utekelezaji wa mapendekezo ya CAG ukipanuliwa kwa maana ya kuzingatiwa kwa mashirika yote ya umma. Hatutaki kuamini kwamba mgongano wa kimaslahi upo tu kwa mashirika ya fedha, kama benki au mashirika ya hifadhi ya jamii.

Kila shirika la umma linapaswa kusimamiwa kwa njia moja au nyingine na Bunge, usimamizi huu waweza kuwa kupitia kwa wizara husika ambayo hujibu hoja mbalimbali zinazohusu shirika husika.

Kwa maana hiyo basi ili wabunge na Bunge zima kwa ujumla wake liweze kuwa huru kutekeleza dhima ya usimamizi wa utendaji wa serikali, ni vema likakaa mbali na uwajibikaji wa siku kwa siku au wa kisera wa mashirika au taasisi za kiserikali. Kwa kuwa mbali wabunge watakuwa na ujasiri wa kuhoji utendaji na kushauri hatua za kuchukuliwa kama mambo yatakuwa hayaendi vizuri.

Lakini sasa inapokuwa mbunge amekirimiwa na shirika la umma iwe hata ni kwa kulipwa posho halali za vikao na njia nyingine za ukarimu unaoweza kuwa umetolewa kwake, ni ukweli usiopingika kwamba hoja ya shirika husika itakapokuwa mbele yake kuijadili hawezi kuwa huru kuizungumzia kwa sababu ni sawa na kujisemea mwenyewe. Uso umeumbwa na haya!

Pamoja na hatua hizo chanya ni vema tukakumbuka kwamba binadamu wana udhaifu wao, tuna kumbukumbu za baadhi ya wajumbe na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma ambao mara wapatapo nafasi hizo, huzichukulia kama ajira; zipo kumbukumbu za wenyeviti wa bodi waliotengenezewa ofisi za kudumu katika mashirika wanayosimamia.

Suala si ofisi tu, ila ni kujikuta kwa njia moja au nyingine mwenyekiti wa bodi wa namna hii anapewa gari, dereva na posho ya kujikimu kila siku, kwa staili hiyo anajikuta akimkwaza mtendaji mkuu wa shirika. Wengi walilalamika kuingiliwa mno na wenyeviti wa namna hii. Ipo mifano iliyo hai kama Tanesco na Bandari walipata kuwa na wenyeviti wa namna hii.

Ndiyo maana tunafikiri ushauri wa CAG na utekelezaji huu ambao umeanza sasa, ni hatua sahihi kabisa katika kuhimiza uwajibikaji na utawala bora. Lakini muhimu zaidi, kuwaepusha wabunge na kashfa ambazo zingeweza kuwanyemelea pasipo wao kujua. Hizi ni zama mpya na sote tukubali kubadilika.


NIPASHE
 
Na bado mimi nasubiri waondolewe kwenye payroll kabisa tunaweza kuwa na wabunge wasionjaa ambao watatumiA pesa zao wenyewe kushughulikia matatizo ya nchi. WABUNGE NJAA TULIONAO AMBAO NI ASILIMIA 90 WANAWAONGEZEA WATANZANIA UMASIKINI KWA UFUJAJI HAKI WALIOJIPA JUU PESA ZA WALIPAKODI.
 
Last edited:
mwanasiasa kuwa kwenye bodi za makampuni ni comflict of interests ndiyo maana nchi za wenzetu mtu aki gombania public office akishinda ana jiuzulu kwenye bodi zote na uongozi wa kampuni yoyote anayo husika nayo. Sasa sisi Tanzania mifano kama Celtel(sasa Zain) kuna vigogo kwenye bodi, Vodacom napo hivyo hiyo na mifano mingine mingi. Nadhani hiki nacho ni chanzo kikubwa cha ufisadi, kama kweli wataamua kufanya hivi watakua wamefanya kitu cha maana. Yetu macho, ngoja tuone kama hiyo plan itakua implemented.
 
Amri ya kuwaondoa wabunge kwenye bodi za mashirika ya fedha inafaa kutekelezwa across the board kwa mashirika yote ya UMMA; kwani mashirika yote hayo yako answerable kwa Msajiri wa hazina.
 
Waondolewe pia kwenye RC,DC na nafasi zingine wabaki na cheo kimoja tuu cha Ubunge vivyo hivyo kwa viongozi wengine wasishikilie cheo zaidi ya moja.
 
yaani serikali ikiamua na hili suala likipita bungeni ndio utakuwa mwanzo na ndio kweli nntaamini sasa ufisadi unaenda kun'golewa juu kwa sababu kama interview ya bwana mengi alivyosema utakua ni mchezo tu, yaani ni mchezo wa kuigiza kama atu-angaiki na chanzo cha matatizo.

ukiwatoa hawa huko ndio wataweza ku-scrutinize vizuri hoja bungeni bila kutetea maslahi. sasa iundwe na indepent body ya kuweza kukagua contracts zote independently, of government interference. Serikali hii allow tanzanians lawyer to form a law society to help them check their laws and how practical they can be, before rushing things.

mwisho lazima tukubali tatizo la ufisadi limeenea nchini na itakua vigumu under the current political weather kuwashtaki viongozi wa hali ya juu. kwa hivyo serikali lazima itunge constitution ambayo itaanza awamu ijayo indepent bodies will be checking all the government deals and tenders, anywrong doing by anybody the case should moved to the law society na ijadiliwe if its answerable then it should reach to the court and people should be made examples. therefore all the people running for the public office should declare their assets na tuanze upya yaliyopita yapite asipelekwe mtu yeyote mahakamani kwa makosa ya zamani, tuanze naa sera mpya vinginevyo utakua ni mchezo tu wa kuigiza.

ps. kwa wale wasioiona interview ya bwana mengi ipo You Tube, together na kiji interview kidogo cha Dr.Mwakyembe akiwa hospital Lowasa akwenda kumpa pole angalieni wenyewe

Mungu Ibariki Tanzania
 
JK, ninampenda kwa jambo moja ni rais ambaye hata kama hatafanya makubwa lakini ndiye anatupisha kwenye kipindi cha mpito!!! Ambacho ni kigumu kwa mkuu wa nchi yeyote
Yafuatayo kwa uchache hayakuwepo:-

-Polisi kumwona Mwananchi kama mteja na boss wake.
-Report ya CAG kuwa wazi
-Uhuru wa kuongea lolote lile bila woga
-Kukaribisha uwezo wa Mtumishi wa Umma kupingana na msimamo wa Serikali mfano Ndg. Ndulu.
-Nakumbuka issue ya EWURA, wanasiasa walikuwa wakiwabana sana EWURA kwamba hawafanyi kazi EWURA wakasema sheria mbaya ikabadilishwa haraka sana.
-Mabadiliko ya Sheria ya Rushwa
-Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi, kutenganisha biashara na siasa.
----
----
---
Nina ukakika JK akipewa kipindi cha pili haya yatawezekana.
-Mgombea binafsi
-Mchakato wa Kubadilisha Katiba.

Wajibu wa wananchi ni kupigia kelele yale wasiopenda JK anasikiliza atatekeleza tu...
 
Kasheshe: Hayo ni kweli au unampamba ili iwe kama kampeni za kuanzia hapa jamvini???????

Mpana mkuu, kama ilivyokuwa kwa Mwinyi, aliweza kuvumilia mageuzi sana. Na Kikwete naye yuko hivyo hivyo, kipindi cha Mageuzi unahitaji Rais mwenye kusikiliza wengi alafu baadaye tutaleta jeuri mara mbiliya Mh. Mkapa.
 
Kama ameshindwa kufanya mageuzi na kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA katika ngwe yake ya kwanza atawezaje huko mbele? Experience yetu imeonesha kuwa kama rais hakufanya vitu vya maana awamu yake ya kwanza , awamu ya pili ni wizi na hujuma kwa kwenda mbele; huwa hawana muda wa kufanya mambo mapya and Jakaya will not be an exception!!
 
Isiishie kuwaengua wabunge kwenye bodi za mashirika ya umma tu. Inafaa hata vyeo vya Uwaziri visitolewe kwa wabunge ili kazi yao iwe kuwatetea wapiga kura wao na watanzania kwa ujumla.
 
Katika pita pita yangu nime fanikiwa kuona jinsi wabunge walivyo katika nafasi sinazoweza zikawa namgongano wa kimasilahi (bodi za mabenki) kama mjadala ulivyovuma wiki iliyopita juu ya uwepo wao kwenye mabodi.

By the way kama kuna mtu mwenye details za huyu maria kejo mana yupo kila mahali.Yeye ni nani, anafanya nini ?mana niko suprise kuona karibu katika teuzi nyingi yupo.


SANDUKU LA BARUA 9111
DAR ES SALAAM
TANZANIA
27 Februari, 2009

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete,
ameteua wenyeviti wa Bodi za Mashirika na Taasisi chini ya Wizara ya
Fedha na Uchumi kama ifuatavyo: -

1. Bodi ya TIB – Prof. William Lyakurwa
2. Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha – Bibi Mwanaidi Mtanda
3. Bodi ya NBC Ltd – Dr. Mussa Assad
4. Bodi ya Twiga Bancorp Limited – Dr. Amon Y. Mbelle
5. Bodi ya Benki ya Posta – Dr. Lettice Rutashobya
6. Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania)– Prof.
Hassa M. Mlawa

Uteuzi huu wa wenyeviti ulianza rasmi tarehe 14 Novemba, 2008.
Aidha, Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo amewateua
wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi wa Mashirika/Taasisi hizo.

Bodi ya TIB
1. Bw. Haruna Masebu
2. Mhe. Mgana I. Msindai (Mb)
3. Bibi Edwina Lupembe
4. Bw. Bedason Shallanda
5. Bw. Adatus V. Magere

Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha
1. Bw. Patric Mwangunga
2. Dr. Suleiman Mohamed
3. Bibi Elipina Mlaki
4. Bw. Leonard Mususa
5. Mhe. Estherina Kilasi (Mb)
6. Prof. T. A. Satta
7. Dr. Clemence Tesha
8. Mhe. Felix Mrema (Mb)
9. Bw. Mugisha G. Kamugisha

Bodi ya NBC Ltd
1. Ponsiano Nyami (Mb)

Bodi ya Twiga Bancorp Limited
1. Mhe. Siraju Kaboyonga Juma (Mb)
2. Mhe. Abdallah Kigoda (Mb)
3. Mhe. Devota Likolola (Mb)
4. Mhe. Hulda S. Kibacha (Mb)
5. Bibi Mariam A. Nkumbi
6. Bw. Geofrey M. K. Msella

Bodi ya Benki ya Posta
1. Bibi Juliana Lema
2. Bw. Saidi M. Hussein
3. Bw. H. H. Mchangila
4. Bi. Bertha E. Mallogo

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania)
1. Bw. Dennis Muchunguzi
2. Bi. Suzan Mkapa
3. Bibi Maria Kejo
4. Mhe. Lucy Mayenga (Mb)
5. Mhe. Richard Ndassa ( Mb)
 
Back
Top Bottom