Wabunge wasifu muswada Serikali mtandao

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1567747611780.png

WABUNGE wamepongeza kupelekwa Bungeni Muswada wa Sheria wa Serikali Mtandao, utakaoweka mfumo thabiti wa kisheria utakaozuia urudufu wa mifumo na miundombinu ya serikali mtandaoni. Muswada huo pia utabadili Wakala ya Serikali Mtandao kuwa mamlaka, itakayokuwa na jukumu ya usimamizi uratibu na udhibiti, urekebu na utekelezaji wa serikali mitandaoni.

Wakichangia muswada huo baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Angella Kairuki kuwasilisha bungeni kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika bila kujali tofauti za vyama vyao, walisema muswada huo umekuja wakati wake.

Akichangia Mbunge wa Busokelo, Fred Mwakibete (CCM) alisema muswada huo ni muhimu kwa Tanzania kuingia katika mitandao na kuendana na maendeleo ya duniani katika mawasiliano mbalimbali. “Ni wakati sahihi kwa serikali kuleta mtandao huo ili tuanze kutumia IT na ICT kufanyuia kazi kwani sasa dunia ipo kwenye kiganja, hivyo biashara, viwanda, utafiti, kilimo, maji, fedha na zinafanyika kupitia mitandao,” alisema Mwakibete.

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) alisema muswada huo ni muhimu, hata kama umekuja bila kujiandaa vya kutosha, kwani elimu itolewe kwanza kwa wananchi na kujenga mazingira ya wananchi kuwa na simu za mikononi.

Mbunge wa Welezo, Saada Mkuya (CCM) alisema serikali inatakiwa kuwa makini na watu wasiopenda maendeleo ya serikali mtandao, ambao wataingiza mitandao feki kama vifaa vya umeme vilivyo feki. Alisema baadhi ya taasisi zilianza siku nyingi ikiwemo Hazina na NHC, hivyo kuwa na sheria hiyo kutasaidia kufanyika kwa ubora zaidi na kupanua huduma kwa jamii. Awali, akisoma maelezo, Kairuki alisema ni muswada muhimu katika kurahisisha matumizi ya serikali mtandao na kuongeza ufanisi na ubora wa huduma zinazodhibitwa na Wakala wa Serikali Mtandao.

“Muswada huo unakusudia kutunga kwa Sheria ya Serikali Mtandao ya Mwaka 2019 itakayoanzisha Mamlaka ya Serikali ya Mtandao itakayokuwa na jukumu la kisimamia na kudhibiti shughuli za serikali mtandao nchini,” alisema. Kairuki alisema Serikali Mtandao nchini itaimarisha ukusanyaji mapato ya serikali, kuimairisha usimamizi wa matumizi ya rasilimali za Tehama katika taasisi za umma.

“Utaboresha mazingira ya biashara (leseni, kodi, benki, usimamizi wa ardhi, utoaji wa hati za kusafiria) na kuimairisha utendaji kazi serikalini (uwazi, ufanisi, uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kudhibiti na kupunguza vitendo vya rushwa na utoaji wa huduma kwa ummoa kupitia Tehama,” alisema Kairuki.

Akisoma maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Dk Jasson Rweikiza alisema suala la usalama wa Serikali Mtandao, lizingatiwe kwa kiwango cha juu na iwapo litaamiwa linaweza kukwamisha shughuli za serikali zinazotolewa kwa kutumia mitadao. “Mtendaji Mkuu wa Mamlaka na wasaidizi wake, wawe ni watu wenye historia nzuri ya kiutendaji serikalini au katika taasisi za umma, wenye moyo wa kizalengo na wanaotanguliza maslahi ya taifa kwanza,” amesema.

Kwa kuzingatia kasi ya maendeleo ya mabadiliko ya teknolojia Tehama duniani, mamlaka hiyo inapaswa kuwezeshwa kifedha na kiufundi ili kuweza kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko hayo.

Akisoma maoni ya msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Catherine Ruge kwa niaba ya Ruth Mollel (Chadema) alisema pamoja na nia nzuri ya uanzishwaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, kambi hiyo inashauri kwamba malengo hayo yanaweza kukwamishwa, kama serikali haitarekebisha baadhi ya sheria ambazo zinadhibiti mawasiliano mitandaoni na upatikanaji wa taarifa na takwimu mbali mbali serikalini.
 
Wawe serious tu na kazi wanazofanya maana tatizo la serikali ni kwenda kununua software kwa wajinga, nahisi kuna watu wanapiga cha juu. Mfano website yenye details zako kwa wale wenye vitambulisho cha taifa, niliiona utadhani imetengenezwa na mtu aliyeanza kuprogram juzijuzi. Iko very slow, hakuna optimization zozote, watu hata 10 wakiingia kubrowse pamoja site inastuck balaa. Wangetoa basi hata tenda ningewatengenezea bure kitu professional sio kuweka uharo wa namna ile.
Hope they do better this time, sijawahi ona system ya Tanzania hata moja fully functional na very professional, zote ovyo.
 
Mkuu, badala ya kuponda hebu kuwa na constructive ideas!! Badala ya kusema wakufuate chukua muda huu kutengeneza hicho unachodhani ni functional, sijui ulimaanisha nini kusema professional. Muda ukifike kipeleke kwa mamlaka kikashindanishwe na vingine na labda chako kitashinda.

Ukiendelea na kuponda ponda hivi nitakuomba utoe ushahidi wa katika sehemu gani uliwahi kuwatengenezea website inayofanya kazi kwa kiwango unachotaka na ambayo inakidhi kila hitaji hata la baadae.
 
Sio kila mbongo unayemuona JF ni ovyo.
Kutengeneza scalable web application ni kitu nimefanya miaka zaidi ya 10 na kampuni kubwa duniani kama Google, ndiyo kazi yangu na ndicho kitu nimekulia nacho toka utotoni. So ninavyoona vitu unprofessional lazima niseme. Sina muda wa kukaa kwenda kudeal na ugoro wa serikali bongo, nishapeleka proposals mbili hawakuwa tayari kupokea hata moja simply because wanaamini software zao walizonunua toka kwenye kampuni za kijinga nyingine South Africa nyingine wamechukua India zimetengenezwa na amateurs, miezi michache system zinafail hawana cha kuongea. Kwani hata kadi tu za UDART ziliishia wapi? Big fail. Hadi leo mnavyokaa kuhisi mambo yamekua fixed, ukweli ni kua kazi wanapeana wanaojuana wanaishia kuja na product zinazofanya kazi wiki mbili then zinakufa. Sihitaji kupinpoint, in short website zote za serikali haziwezi handle concurrent users 100 tu, kitu ambacho hata amateur software developer angeweza kuscale.
 
Wawe serious tu na kazi wanazofanya maana tatizo la serikali ni kwenda kununua software kwa wajinga, nahisi kuna watu wanapiga cha juu. Mfano website yenye details zako kwa wale wenye vitambulisho cha taifa, niliiona utadhani imetengenezwa na mtu aliyeanza kuprogram juzijuzi. Iko very slow, hakuna optimization zozote, watu hata 10 wakiingia kubrowse pamoja site inastuck balaa. Wangetoa basi hata tenda ningewatengenezea bure kitu professional sio kuweka uharo wa namna ile.
Hope they do better this time, sijawahi ona system ya Tanzania hata moja fully functional na very professional, zote ovyo.
Kweli kabisa mkuuu, wamekusikia wahusika
 
Back
Top Bottom