Wabunge Washtushwa TCRA kutumia Bilioni 18 kwa Semina na Warsha

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1.jpg

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) imeshtushwa baada ya kubaini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitumia Sh18 bilioni mwaka 2013/2014 kwa ajili ya mafunzo, semina na warsha.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Lolesia Bukwimba alisema matumizi ya fedha hizo ni makubwa ikilinganishwa na kazi iliyofanywa na mamlaka hiyo kwa mwaka huo wa fedha.

Alisema wakati mapato ya TCRA kwa mwaka huo yalikuwa Sh79 bilioni, gharama za uendeshaji zilikuwa Sh76 bilioni.

“Hii ina maana fedha zilizopelekwa Hazina zilikuwa kidogo. Kama mamlaka ingepunguza matumizi, Serikali ingepata mapato ya kutosha,”alisema.

Bukwimba alisema hilo ni tatizo na kamati hiyo itatoa maagizo kwa mamlaka hiyo Jumamosi ijayo itakapoitembelea.

“Kuna mambo mengi ya kitaalamu ambayo tunahitaji kuona shughuli zake zinazofanywa na mamlaka, tutatoa maagizo siku ambayo tutaitembelea,”alisema Bukwimba.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Profesa Haji Semboja aliitetea mamlaka hiyo akisema kiasi hicho kilichotumika kwa ajili ya semina, mafunzo na warsha kinatokana na unyeti wa taasisi hiyo.

“Taasisi inasimamia kampuni zinazotoa huduma za teknolojia za kisasa ambayo ni ngeni hapa kwetu, hivyo wafanyakazi wetu wanatakiwa kuwa na ufahamu zaidi ya hao watoa huduma,” alisema Profesa Semboji.

Semboja, ambaye ni mchumi, alisema: “Pamoja na mambo mengine, wafanyakazi wetu wanasimamia kampuni za mitandao ya simu, matoleo ya simu yanatoka mara kwa mara, wanatakiwa kufahamu teknolojia wanayoisimamia. Hapa ni lazima waende darasani.”

Alisema wafanyakazi hao wakiachwa bila kupata mafunzo ya mara kwa mara watajikuta baada ya kipindi kifupi wanapitwa na teknolojia zinazozidi kuibuka kila wakati.

Kwa upande wake, Sabrina Sungura ambaye ni mjumbe na mbunge wa Viti Maalumu, aliitaka mamlaka hiyo kufanya marekebisho ya minara ya simu mkoani Kigoma.

“Hii ni hatari kwa usalama,” alisema.
 
hii mamlaka haizalishi bali ni watumiaji tu, Bora msajiri wa hazina aikalie rohoni. ukienda pal sura zao tu zinakujulisha kuwa ni wabadhirifu.
 
Pamoja na kutumia pesa hizo zote bado TCRA badala ya kuwasaidia watanzania bado ndo kwanza wamekuwa mawakala wa VODACOM, AIRTEL, na tiGO
Eti unanunua kifurushi chenye mb 1 kwenye mitandao karibu yote, halafu wanaona sawa tu! Simu fake kila siku zinaingizwa nchini wao wameshindwa kuzizuia zisiingie badala yake wanataka kuzifunga, nani atakayerejesha pesa zilizoenda nje ya nchi kwa kununua simu mbovu zitakazofungwa mwezi wa sita? Halafu profesa anasema wafanyakazi wao ni lazima waingie darasani kujifunza kuhusu aina mbalimbali za simu!!!
 
hii mamlaka haizalishi bali ni watumiaji tu, Bora msajiri wa hazina aikalie rohoni. ukienda pal sura zao tu zinakujulisha kuwa ni wabadhirifu.
Mkuu unajua unachoongea? Hawa wanajiendesha wenyewe wana pesa mingi sana sana....na wanachangia kwenye pool , serikali vizuri sana! Radio zote TV na Makampuni ya simu....(Masafa,leseni, usage-Simu) yaani leseni tu Telecom ni 400Mil kwa mwaka....nenda kwenye Masafa wanapiga sana tena kwa dola! Hawapewi hata centi na serikali! Wanajiendesha wenyewe hawa! Na ni kweli inabidi wasome waende technolojia inavyokimbia.....kila siku kinatoka kitu kipya kwenye mawasiliano...kuwasomesha ni nje na bei kubwa! Mfano kozi ya new innovation kwenye telecom inagharimu dola 25,000 kwa mtu mmj 3 weeks tu hapo bado kula posho na tickets! Inabidi engineers waende kwa awamu ili kuwa sawa! Ni sawa kabisa.....!!
 
Suala siyo kujiendesha... Ulitarajia mtaji wote waliopewa huo bado wapewe pesa tena nyingine na serikali? Wameachiwa wakusanye pesa toka mitandao yote ya simu... Radio na tv harafu wapewe pesa tena zingine za nn? Infact kwa kuoewa mtaji huo tulitarajia wachangie zaidi serikalini... Imagine mnakusanya 79 bil na mnatumia 76bil kwa mujibu wa hyo taarifa kama ni kweli Hope wataimprove...
 
Mkuu unajua unachoongea? Hawa wanajiendesha wenyewe wana pesa mingi sana sana....na wanachangia kwenye pool , serikali vizuri sana! Radio zote TV na Makampuni ya simu....(Masafa,leseni, usage-Simu) yaani leseni tu Telecom ni 400Mil kwa mwaka....nenda kwenye Masafa wanapiga sana tena kwa dola! Hawapewi hata centi na serikali! Wanajiendesha wenyewe hawa! Na ni kweli inabidi wasome waende technolojia inavyokimbia.....kila siku kinatoka kitu kipya kwenye mawasiliano...kuwasomesha ni nje na bei kubwa! Mfano kozi ya new innovation kwenye telecom inagharimu dola 25,000 kwa mtu mmj 3 weeks tu hapo bado kula posho na tickets! Inabidi engineers waende kwa awamu ili kuwa sawa! Ni sawa kabisa.....!!
Wanachangia nini?? Yaaani wanakusanya 79 bill halafu wanatumia 76 bill hakuna kitu hapoo
 
Wanashindwa kuibeba ttcl badala yake wanaweka mazingira ya kuiua kabisaa.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Huwa naweka MB 500 kwenye simu na zinakwisha bila kudownload chochote....hii mitandao ya simu inatuibia mchana kweupeee, na TCRA ipo inashangaa tuuu
 
Mkuu unajua unachoongea? Hawa wanajiendesha wenyewe wana pesa mingi sana sana....na wanachangia kwenye pool , serikali vizuri sana! Radio zote TV na Makampuni ya simu....(Masafa,leseni, usage-Simu) yaani leseni tu Telecom ni 400Mil kwa mwaka....nenda kwenye Masafa wanapiga sana tena kwa dola! Hawapewi hata centi na serikali! Wanajiendesha wenyewe hawa! Na ni kweli inabidi wasome waende technolojia inavyokimbia.....kila siku kinatoka kitu kipya kwenye mawasiliano...kuwasomesha ni nje na bei kubwa! Mfano kozi ya new innovation kwenye telecom inagharimu dola 25,000 kwa mtu mmj 3 weeks tu hapo bado kula posho na tickets! Inabidi engineers waende kwa awamu ili kuwa sawa! Ni sawa kabisa.....!!
Mzee acha kutetea ujinga. Yani wanachangia kwenye pool kwa kutumia 76B wakati mapato ni 79 B. Hivyo net income ni 3B kwa mwaka. Na kuhusu hizo kozi inamaana hata kazi hawafanyi kwani wapo mafunzoni muda wote. Kwa sababu ni upuuzi km kila simu mpya ikitoka au technology wanaenda tena darasani. Kila sekta technology inaenda kasi lkn ukisema ndio kila software mpya au mashine ikinunuliwa mafunzoni tena. Kwa 25,000 kwa 3 weeks itakuwa hamna maana ya kuwa expert katika eneo lako.
 
jamaa ni wapiga dili saaana wana maneno mengi utafikiri ni kweli wanajituma kumbe ni watu wa dili tu ! watumbuliwe tu maana hakuna namna
 
Tcra ni wezi wakubwa wanashirikiana na makampuni ya simu kuwaibia watanzania watumbuliwe
 
Wataendelea kushitushwa hivyo hivyo bila kuchukua hatua. Nakumbuka kama miaka miwili hivi iliyopita walishitushwa tena kwa hao hao TCRA kusomesha watu watatu masters kwa bilion moja nje ya nchi. Kuna maswali mengi walijiuliza, lakini ninalokumbuka ni je hao wanafunzi walijengewa chuo chao binafsi, maana hela ni nyingi sana
 
Back
Top Bottom