Wabunge washauri siasa vyuoni zipigwe marufuku... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge washauri siasa vyuoni zipigwe marufuku...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 20, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Gladness Mboma, Dodoma

  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, imeshauri serikali kupiga marufuku viongozi wote wa vyama vya kisiasa kufanya mikutano ya kisiasa katika vyuo vya elimu ya juu, ili maeneo hayo yatumike kwa shughuli za mafunzo na utafiti pekee.

  Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Bungeni jana, Mwenyekiti wa Kamati, Bi. Margret Sitta, alisema mbali na hilo, ni vema serikali itafiti vyanzo vya migomo na migogoro katika vyuo vya elimu ya juu vya serikali.

  Akizungumzia mikopo, Bi.Sitta alisema ili serikali iweze kuimarisha suala hilo, inapaswa kutafuta mbinu mbadala za kupata fedha kuinua uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaoongezeka mwaka hadi mwaka.

  Alisema wakati wa kutoa mikopo, vigezo maalum vitumike kuwatambua walengwa wenye uhitaji ambao ni wanafunzi kutoka familia zenye kipato duni.

  "Ili kuimarisha urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa tangu mwaka 2006, kiundwe chombo mahususi chini ya bodi ya mikopo kufuatilia ukusanywaji wa marejesho ya mikopo iliyokwishatolewa.

  "Aidha, taarifa za mikopo husika zitambulike kwa walengwa ili kurahisisha ukusanyaji wa fedha hizo kwa ushirikiano wa mwajiri na bodi ya mikopo," alisema.

  Alieleza pamoja na hayo, fedha za marejesho ya mikopo hiyo na matumizi yake zitambulike bayana kwa kuonekana katika taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara kila mwaka wa fedha.

  Wakati huo huo Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw.Joseph Mbilinyi,(CHADEMA) amesema chama hicho kitaendelea kufanya maandamano ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kuendelea kugoma kutokana na serikali kushindwa kuwatimizia mahitaji yao.

  Akichangia mjadala wa hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi jana Bw. Mbilinyi maarufu kwa jina la (Mr Sugu) alisema hali hiyo itaendelea kuwepo kwa kuwa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimuya Juu imeshindwa kuondoa kasoro zinazojitokeza.

  "Maandamano ni poa na yanaruhusiwa, hivyo ruksa wanafunzi kuandama. Nashangaa baadhi ya waheshimiwa tena wamo humu ndani walikuwa wakipinga maandamano lakini juzi walikwenda Mbeya kufanya maamdamano wakiwa wameambatana na waasisi wa CCJ," alisema.

  Bw. Mbilinyi alisema kuwa hata wao CHADEMA wataendelea kufanya maandamano ya amani kwa kuwa CCM nao juzi wakiwa mjini Mbeya walifanya maandamano wakati walikuwa wakiyabeza.

  Akizungumzia malimbikizo ya walimu,Bw. Mbilinyi alisema Mbeya kuna walimu 300 wanaodai malimbikizo ya zaidi y sh. milioni 400 na kumtaka Waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa, kumweleza ni lini walimu hao watalipwa pamoja na kuitaka serikali kurudisha elimu bure nchini.

  Naye mbunge wa Viti Maalum,Bibi. Chiku Abwao (CHADEMA), alisema suala la maandamano ni silaha muhimu katika kufanikisha masuala mbalimbali nchini, kwani bila kufanya hivyo hakuna kitakachoendelea.

  "Walimu nchini ndio kielelezo cha umasikini, wanabembeleza kupata haki zao…tunasema maandamano hatayaisha na CHADEMA tutaandamana kwa ajili yao," alisema.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Tuliwahi kulisema hapa suala hili (nadhani kipindi Kikwete 'alipochangiwa' na 'wanafunzi wa UDOM' kuchukua fomu za kuwani Urais kwa muhula wa pili). Ikiwa kwa sisiemu kufanya siasa kwa wanafunzi (tena sio vyuo vikuu tu, kuna nyakati wanatumia hata watoto wa shule) ni sawa, vyama vingine vikafanya inakua 'nongwa'!

  Siasa vyuo vikuu haikuanza jana wala leo, imekuwapo....labda waseme tu wanaogopa kivuli cha CDM!
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwenye baraza la mawaziri sasa hivi wapo mawaziri waliowahi kusimimishwa masomo kwa sababu kugoma. Mmojawapo ni Dr.Ciril Chami. Sijui huu unafiki wa ccm unatoka wapi maana wao wenyewe ndio waasisi wa migomo.

  Practically, watazuiaje siasa kwenye vyuo? Yaani eneo la chuo lisitumike kwa mikutano ya kisiasa au wanafunzi wasiruhusiwe kuhudhuria kwenye mikutano ya siasa hata kama inafanyika nje ya 'geograohical sphere' ya chuo?!

  Kwa kushirikiana na NEC ccm walihujumu wanachuo haki yao ya kikatiba ya kupiga kura uchaguzi mkuu uliopita. sasa kupitia kamati hii inayoongozwa na mke wa muasisi wa CCJ -Sitta bado wanaonekana kuwafuatafuta wanachuo. Itakula kwenu ccm and this time itakuwa worse kuliko huko nyuma. Siasa za kizamani sana hizi hata sijui imekuwaje tukaongozwa na firka uchwara kama hizi kwa miaka yote hiyo!
   
 4. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Huyo mama na kamati yake wanatia maji kwenye gunia, siasa huwa hazifanyikii kwenye vyuo bali wanasiasa hufanya nje ya chuo na siyo kama magamba wanavyodai, tutapiga siasa hata kama wataweka sheria ya aina gani. kwana hao wanachuo ni watu wazima na wametimiza umri unaostahili kuwa na uhuru kwenda chama chochote kile.

  CCM imeefeli siasa za wasomi sasa wanatafutasababu za kipuuzi puuzi kuudaganya umma kuwa cdm wanaharibu watoto wao huko vyuoni wakati 2005 jk alijenga mtandao mkubwa wawanazuoni na 2010 aliunda timu ya wanafunzi wa vyuo vikuu kupitisha fomu yake ya udhamini kwa watanzania.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Mumewe mwenyewe katokea Chuoni kisiasa.........sasa watoto wetu wasijue siasa?
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  CCM waoga Wanachuo Wasomi Wengi walioko Vyuoni Sasa hivi mrengo wao ni Upinzani na wengi wao ni Chadema...

  Nape Nnauye alifanya ziara University of Dodoma akaenda kwenye Bweni Moja akaona Picha za Wilbroad Slaa, akasema hii haitakiwi lazimishwa kuondolewa, Mwanafunzi akagoma.

  It worries a lot Chama Cha Mafisadi...
   
 7. a

  ashakum Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NNACHOJUA MIMI NI KUWA SIASA VYUONI IMEPIGWA MARUFUKU. Lakini tumemwona Nnape, kijana wanayemtoa kafara chama cha Magamba yuko na wanavyuo wa vyuo vikuu Dar. Hili sio kosa? Kuna mwanangu anasoma kule UDOM alinipigia simu kuwa kuna wenzao wamefukuzwa chuo kwa kukutwa kwenye ice na skafu za Chama cha Magwanda-CDM. Hao waliokuwa na Nnape sio kosa ati?:nono::nono::A S shade:
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wao sio kosa
   
 9. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  wakati mwingine hawa wanaojiita viongozi wanapaswa waone unafiki wao. Kwa UDOM sio tu waliopanda kwenye costa na magwanda, lakini pia wale wote waliokuwa wanavaa gwanda wakati wote wa vipindi wameondolewa chuoni. sasa hawa wa c.c.m tunahitaji maelezo ya Nape, vipi hawajahusika na siasa vyuoni? au ndo hivyo kuny... any.... kuku, akinya bata kaharisha?
   
 10. lendila

  lendila JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2014
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 4,835
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  Maana ya siasa ni nini? Na nukuu maana ya siasa kutoka waraka wa kanisa katoliki mwaka 2009 siasa maana yake ni maisha ya kila siku ya mwanadamu, yahusuyo maji,elimu, afya, uchumi, na kadhalika je hilo jibu la waraka wa kanisa katoliki ni sahihi? Je kama ni sahihi mbona wanafunzi wa vyuo vikuu wanakatazwa wasishiki kwenye vyama? Naombeni msaada wenu
   
 11. A

  Agueromkuu Member

  #11
  Nov 22, 2014
  Joined: Nov 2, 2014
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kawaida kwenye nchi zilizopiga hatua ya kidemokrasia, wanafunzi wa vyuo ndo waletaji wakubwa wa mabadiliko katika mwenendo wa kisiasa wa nchi. Huku kwetu wameshaisoma hiyo ndo mana mambo yakianzishwa vyuoni inatumika nguvu kubwa sana kuizima...
   
 12. lendila

  lendila JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2014
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 4,835
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mkuu wanaofia uelewa mkubwa wa wana vyuo?
   
 13. d

  duanzi JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2014
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 16,455
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hawana hela
   
 14. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2014
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Bora hii mada imekuja kwangu, na mimi ni mmoja wa wanafunzi wa chuo. Mwezi uliopita nilikuwa napiga stori za siasa na muuza nyama ghafla akaja mzee moja na kuanza kuniuliza, je namjua ye ni nani? Akanambia kuwa yeye ni kada wa CCM, kabla ya kuniuliza hili swali mimi nilikuwa nakandania sana ni namna gani Serikali yetu inavyoboronga hususani Awamu hii ya Nne.
  Mbele kabisa ya maongezi nikamfahamisha kuwa mimi ni mwanafunzi, akaniambia kuwa nisome kwanza harafu siasa baadae nikishapata maisha yangu binafsi. Na hoja yake hii iliungwa mkono na watu wawili wa pembeni.
  Wanasema kuwa maisha ya Watanzania hususani sisi wanafunzi tunakosa kazi kutokana na fani tunazosomea na si Serikali. Pia wanasema hata iongezwe miaka 300 mbele, Slaa hawezi kushika nchi.
  Kubwa zaidi wameshikilia hapo kwamba nisome kwanza, niwe na maisha yangu binafsi kisha ndo nianze kufatilia siasa.
  Sasa Je, wanaJF na nyie mnanishauri vipi?
   
 15. QALLI MIZOH

  QALLI MIZOH JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2014
  Joined: Mar 19, 2014
  Messages: 2,088
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Tupambane kwanza kwenye hili swala la escrow haya mengine yatafuata ...
  Come-on guys let's do it!!
   
 16. M

  Magagi manonu Member

  #16
  Nov 22, 2014
  Joined: Nov 16, 2014
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yaacheni kwanza hadi tujilizishe suala la PESA ZETU za Escrow na wezi wamerudisha na hatua zaidi zimechukuliwa dhidi yao,ndipo turudi kwenye hoja kama hii japo inayofuata ni Katiba inayopendekezwa nayo watuambia 2/3 ya Zanzibar ilipatikanaje na kwa nini wameweka mfumo ambao wananchi hawakuupendekeza?
   
 17. Priddim

  Priddim Senior Member

  #17
  Jan 23, 2015
  Joined: Sep 25, 2014
  Messages: 156
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Unaktaza wanafunzi wasifanye siasa wakati vyuoni hapo hapi kuna masomo ya siasa?

  Kuna matawi ya vyama,kuna majengo kongwe ya chama,mikutano ya cha chama serukali inafanyia hapo hapo,Mawaziri wanakujaga kugawa kadi za vyama,

  Sasa unakataza nini.?
  WAJINGA SANA NYIE.
   
 18. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2015
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CCM futeni MKOA wa vyuo vikuu.
   
 19. lendila

  lendila JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2015
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 4,835
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  Tuchukuwe la kamati au la waziri mkuu?
   
 20. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2015
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hebu wazee wangepumzika sasa maana maono yao yamechoka kwa kweli!!!!
   
Loading...