Wabunge Wapewe Meno Kuthibit Watendaji

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,721
21,778
Madiwani wapewe meno kudhibiti watendaji
David Azaria
Daily News; Tuesday,May 14, 2008 @21:01


Majuzi madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita mkoani Mwanza na wabunge wao watatu walifikia uamuzi wa kuwafukuza kufanya kazi wilayani humu Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya na msaidizi wake na kuwataka kwenda kutafuta wilaya nyingine ya kufanyia kazi kwa kuwatuhumu kwa uzembe uliosababisha miradi mbalimbali ya maendeleo kutotekelezeka.

Madiwani hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jeremiah Ikangala walifikia uamuzi huo kwa kauli moja, baada ya kujadili suala hilo kwa muda na kutoa madai mengine dhidi ya maofisa hao ikiwamo kwamba wataalamu hao wamekuwa na kiburi na hawasikilizi ushauri wa wataalamu wengine.

Walieleza kwamba Mhandisi huyo wa Wilaya Jackson Matabi na msaidizi wake Elly Mkwizu, wameshindwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na hasa ujenzi wa vituo vya afya, zahanati, nyumba za watumishi katika idara hizo, shule za sekondari na barabara.

Madiwani hao walikwenda mbali zaidi kwa kueleza kwamba wamekuwa wakimtumia mkandarasi mmoja katika ujenzi ama ukarabati wa barabara za wilaya hiyo, ambaye hata hivyo kwa maoni yao na ya wananchi ubora wa kazi zake ni mdogo na hivyo hapaswi kupewa kazi hali ambayo imewafanya wahisi kwamba wataalamu waliotimuliwa wana maslahi binafsi na mkandarasi huyo.

Wengi wa madiwani walilalamikia utengenezaji wa madaraja mbalimbali katika wilaya hiyo ambako walieleza kwamba pamoja na madaraja hayo kutumia fedha nyingi yamekuwa yakiharibika mara kwa mara huku kukiwa hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa katika kudhibiti hali hiyo.

Diwani mmoja alisema wakati Serikali inatoa fedha nyingi katika kuhakikisha kwamba miradi mbalimbali ya wananchi inatekelezwa ipasavyo, kuna watu ambao kazi yao ni kuangalia namna gani wanaweza kula fedha hizo. Nionavyo mimi uamuzi wa madiwani umechelewa.

Ulitakiwa kuchukuliwa siku nyingi zilizopita. Hakukuwa na sababu ya kusubiri mpaka sasa ili kuchukua uamuzi huo wakati tayari makosa yalikwishaanza kuonekana ikiwamo kutengenezwa kwa barabara ambazo hazidumu kwa miezi angalau mitatu kwani wanachokifanya wakandarasi ni kuparura barabara, kutoa mchanga pembeni na kuuweka katikati ya barabara.

Uamuzi wa madiwani hao, ingawa umechelewa, unaweza kutumika kama onyo kwa wataalamu wengine wa Geita na kwingineko nchini ambao wamekuwa na kiburi katika kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa madai kwamba wao si wanasiasa hivyo hawawezi kubabaishwa na wanasiasa.

Kuna wakati baadhi yao walifika mbali zaidi na kueleza kwamba wao ni wasomi ambao hawajaajiriwa na wanasiasa na kwamba wakikataliwa na kufukuzwa katika wilaya fulani watawahamishia maeneo mengine. Kwa kuwa nchi yetu kwa sasa ni ya wasomi wasio na kazi hakuna sababu yoyote ya mtu kama huyu ambaye amekataliwa na madiwani sehemu fulani kuendelea kuwa katika ajira ya Serikali.

Na kwa vile Serikali ya Rais Kikwete ilikwisha kutangaza kwamba mtumishi yeyote wa umma atakayekataliwa sehemu fulani na madiwani ama wananchi kutokana na sababu za msingi hatahamishiwa sehemu nyingine kwa kuwa hata huko atakwenda kufanya madudu tu kama aliyoyafanya huko alikotimuliwa, wakati umefika wa kuwapa meno madiwani katika kuwadhibiti watendaji wabovu. Na katika kuhakikisha kwamba hilo linatekelezeka serikali imewaambia madiwani kwamba kama watashindwa kuwashughulikia watendaji wabovu, basi watashughulikiwa wao.
 
Jamani Madiwani Nao Wanataka Kuvuna Vijisent Wameona Ujinga Huu Kukaa Kama Mazoba Tunawasubiri,,,nyie Bandugu Mna Meno Mnaiba Hivyoo Mkiongezewa Si Balaa Zaidi Mwenzenu Meya Londa Alitaka Kupeleka Familia Nzimamarekani Kama Si Wanaume Kuwashtua Mapema Ubalozi...mkiongezewa Si Balaa Zaidi .jk Nyie Endeleen Kula Hawa Wakila Hawatashiba
 
Ni sahihi kwa Madiwani kupewa meno ili kuweza kusimamia sera na mipango yao.
 
Yes Kibunango @ work .Haya yangu macho .Je kata zao zina maendeleo yapi kwa ubunifu wao wa kuleta maendeleo ?
Kamanda Lunyungu.
Kupitia kamati za maendeleo katika wadi hadi kufikia ngazi ya wilaya kuna mengi ya kufanyika ili kuondoa kero mbalimbali kama vilivyoainishwa kwenye mada mama ya bandiko hili.

Mengi yamekuwa yanashindwa kufanyika kutokana na kuwa watendaji wa Halmshauri walikuwa wanawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi badala ya madiwani, hivyo kujenga aina fulani ya kiburi ,uzembe na kufisadi mali za Halmshauri.

Watendaji kuwajibika kwa Madiwani ndio njia pekee ya kuweza kuwepo kwa ufanisi katika shughuli zote za kimaendeleo katika halmashauri. Ni wajibu wa madiwani kuja na sera na mipango ambayo ina lengo ya kuwanufaisha wananchi wao. Na kuwaachia wataalum wao(watendaji) kumalizia yale yote yaliyokusudiwa. Iwapo itashindikana lawama kamwe azitakwenda kwa mtendaji bali ni kwa Diwani. Hii kwa namna moja ni njia nzuri ya kuwabana madiwani wenye mawazo ya ajabu katika kuleta maendeleo katika wadi zao.

Nafikili bado unakumbuka kituko cha Diwani mmoja katika Jiji la Mwanza ambae alitaka mawe yote ndani ya jiji hilo yapakwe chokaa ilhali kuna kero chungu nzima zilizokuwa zikitakiwa kufanyiwa kazi...
 
Ilitakiwa hiwe hivi siku nyingi kwani watendaji wanakosa watu wa kuwawajibisha ndo maana wanatafuta watu wa kuwapa 10% hata kazi yake ni mbaya, lakini kwa sheria za tanzania sijui kama wana nguvu za kuwafukuza kazi au wanatakiwa kupeleka malalamiko POLAG kwanza.
 
Ni hadaa tupu. Wameingia council ili wale wakiona watendaji wanawazibia inawauma sana. Same with Wabunge, that is my take on this.
 
Back
Top Bottom