Wabunge wapewe mazoezi ya kupunguza vitambi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wapewe mazoezi ya kupunguza vitambi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, May 20, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya wabunge jamani wanaitaji kupewa mazoezi muhimu ya kupunguza vitambi
  swala hili si tu litawasaidia kwenye afya zao bali hata kwenye kulinda ndoa zao
  katika swala la TLN...kila mtu anajua umhimu wa TLN na hasa pale unapomnyima mwenzio
  haki yake ruksa kulalama kwa wazee wa kanisa..je wangapi wabunge mko radhi kupoteza ndoa zennu..kufa ovyo na kugharimu bunge na maziko ya kujitakia

  embu ukiwa kama mmbunge unaejali afya yako jaribuni kwenda kupima mara kwa mara afya zenu na kupunguza vitambi mpate haja za mioyo yenu...

  all the best kwenye uchaguzi
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,005
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo wawadhulumu wananchi,wakipata vitambi wananchi wawalipie na mazoezi ya vitambi?Acha utani mkuu,
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  wenzio hawapendi tabu, ndo maana matumbo yana jaa kama yana upepo...mikuku, mishikaki,mayai,mapombe, mabia, mawhisk,maugali,matambi,mawali,machachandu,makuku,mang'ombe,madawa ya kienyeji,mahirizi ya kumeza kila kitu ukichanganya kwenye tumbo moja, lazima utakuwa tembo tu......wanapata shida kwelikweli...hahaha. laiti wangeenda hata kutembelea vijijini wakachoka kidogo hata kukaa kwenye magari yao tu pengine wangekuwa wanafanya zoezi, sasa kazi yao ni kula,kunywa,kusinzia na kulala tu. sitaki kuwataja majina hapa...
   
 4. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania/Waafrika wengi;moja ya dalili za mafanikio ni mtu kuwa na kitambi,overweight or even obese.Utasikia 'mambo yake safi siku hizi,juzi nimekutana nae,kanenepa huyo'...Ukiwa mwembamba hivi,na wasipojua deals zako,watakwambia umefulia.
  Kwahiyo wapo wengi wanaodhani kunenepeana ndiyo afya bora,huku wakitafuta sifa ya kuitwa vibosile kwa sababu ya vitambi vyao.Sasa siku mtu anapigwa na heart attack/stroke,anazimika ghafla,watasema kuna mkono wa mtu,ametupiwa 'jini',mbona hakuugua,alikuwa na afya nzuri kweli...!
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hiyo ndiyo tabia iliyojengeka Bongo, nyamachoma kwa kwenda mbele, michemsho, bia, halafu hakuna mazoezi. Hata hivyo wengi wanautafuta unene bila kujua kuwa ni hatari kwao..
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Kwa hili litakuwa gumu manake wengi wanapenda sana matumbo, fuatilia wengi wao wakiwa wanaongea au kuhutubia wanapenda sana kuyakuna!
   
Loading...