Wabunge wanne wa CHADEMA waliokamatwa kwa kukiuka masharti ya dhamana wapewa onyo na kuendelea na dhamana yao

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaonya wabunge wanne wa Chadema waliokiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani bila taarifa yoyote.

Onyo hilo limetolewa leo Jumatano Novemba 20, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kusikiliza utetezi wao, kubainisha kuwa haukujitosheleza lakini hatowafutia dhamana kwa kuwa itakuwa hatua kali.

Novemba 15, 2019 mahakama hiyo iliamuru wabunge hao, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini); John Heche (Tarime Vijijini); Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda) kukamatwa baada ya siku hiyo kukiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili.

Mbali na kutoa amri hiyo, mahakama hiyo pia ilitoa hati ya wito kwa wadhamini wao kujieleza kwa nini hawakuwapeleka washtakiwa mahakamani.

Wabunge hao walianza kujisalimisha kuanzia Jumamosi iliyopita na leo mahakama hiyo ilipanga kutoa uamuzi kuhusu kukiuka kwao dhamana.

Wabunge hao pamoja na wenzao watano akiwemo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018 jijini Dar es Salaam.

Akitoa uamuzi huo Hakimu Simba amesema maelezo yaliyotolewa na washtakiwa hao pamoja na wadhamini wao hayajitoshelezi lakini kuwafutia dhamana ni hatua kali.

Amesema washtakiwa hao kujisalimisha polisi walikuwa wakiogopa kitakachowapata.

Ijumaa iliyopita Mbowe, katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji; naibu makatibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara) na Esther Matiko (Tarime Mjini) ndio waliofika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
 
Kesi za namna hii alitakiwe apewe "Judge 1,000 years" ashugulikie hawa wanasiasa wasiojitambua..
 
Mh. Hakimu Simba wa mahakama ya Kisutu amewataka wabunge Heche wa Tarime vijijini na Mchungaji Msigwa wa Iringa kufika mahakamani wakiwa na wadhamini wao siku ya tarehe 26/11/2019 na kama watashindwa kufanya hivyo watafutiwa dhamana zao.

Source: Eatv habari
 
Natamani ningesoma sheria ili nijue logic ya mtu kuwekewa dhamana. Niliwahi kuuliza jukumu la mdhamini ni nini? Niliambiwa ni kuhakikisha mshitakiwa anahudhuria kesi yake kwa muda wote itakapokua inatajwa au kusikilizwa

Aidha mdhamini ndio mwenye dhamana ya kuhakikisha mshitakiwa hatoroki au kuruka dhamana kwa kipindi chote cha kesi yake hadi hukumu itakapotolewa

Nikauliza tena kama ndio hivyo kwanini sasa kuna watu wengine wanaojulikana wakiwa na dhamana kubwa kwa jamii kama Ubunge na wanajulikana wapo wapi wakati wote nao pia lazima wadhaminiwe tena kwa shtaka la namna hiyo? Nikajibiwa kua sheria haitakiwi ibague mtu kwa kazi au hadhi yake katika jamii

Nililikubali jibu hilo kwakua sijui sheria na falsafa yake lakini mpaka kesho naamini kua yawezekana kufanya mambo kwa namna ya kwenu kuhakikisha katika kutekeleza sheria mlizojiwekea hamdhalilishi watu hasa wale waliopewa dhamana kubwa na Wananch wenyewe au Taifa kwa ujumla hasa wakiwa bado hawajakutwa na hatia ya kosa lolote
Ni mtazamo wangu wa ki layman tu
 
...kibaptist, ripota wa jumla toka lumumba, bado kidogo utaanza kutuletea habari za michezo, na biashara!
Hahahaaa........ Nawapa msisitizo kwa sababu niliumizwa sana na yaliyomkuta Mbowe last year na tarehe zilikuwa ni hizi hizi za majaji kuelekea likizoni!
 
Kama ukitaka kujenga umoja wa kitaifa...haya mambo ya visasi vya kisiasa ni ya kuachana mayo!!

Walimwengu wanatushangaa sana kwa sasa huu haukuwa utamaduni wetu wa ile Tanzania ya Mwalimu.
 
Kama ukitaka kujenga umoja wa kitaifa...haya mambo ya visasi vya kisiasa ni ya kuachana mayo!!

Walimwengu wanatushangaa sana kwa sasa huu haukuwa utamaduni wetu wa ile Tanzania ya Mwalimu.
Kabisa mkuu, ni aibu na fedheha kuna wajinga wanafurahia kutesa binadamu wenzao hata bila hoja ya msingi.
 
Back
Top Bottom