Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,872
Kikao cha kamati kuu ya Chadema kilichoongozwa na mwenyekiti wake mh Mbowe kwa njia ya mtandao kimefanya maamuzi magumu mno.

Taarifa ya maamuzi hayo inategemewa kutolewa leo na Katibu Mkuu wa chama hicho Mh. John J. Mnyika.

—————
UPDATES
—————
Akitolea maamuzi hayo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema

Kamati Kuu CHADEMA imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama

Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama.

Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo.

F878B8B8-4933-4C4E-A7F5-60159F059390.jpeg

1D630E10-6696-4838-A760-F28DE16BFC1C.jpeg

A2172BA4-93B9-40D2-9F99-26CC4EBD42A9.jpeg
 
Kikao cha kamati kuu ya Chadema kilichoongozwa na mwenyekiti wake mh Mbowe kwa njia ya mtandao kimefanya maamuzi magumu mno.

Taarifa ya maamuzi hayo inategemewa kutolewa leo na Katibu mkuu wa chama hicho mh J J Mnyika.

Source: Tanzania Daima
Umeamka nao, loh! CHADEMA. CHADEMA inawahangaisha sana, what is your psychology behind CDM, you need psychological healing!
 
Mbona sehemu ya kukimbilia ipo tayari, ni sababu tu ya kuondoka ndio walokua wanatafuta. Waliogopa kuambiwa wamekwenda kuunga mkono juhudi...
 
Kikao cha kamati kuu ya Chadema kilichoongozwa na mwenyekiti wake mh Mbowe kwa njia ya mtandao kimefanya maamuzi magumu mno.

Taarifa ya maamuzi hayo inategemewa kutolewa leo na Katibu mkuu wa chama hicho Mh. J J Mnyika.

Source: Tanzania Daima
Kama wameshafanya maamuzi sasa mbona hawajayaweka kwa gazeti la mwenyekiti wao? Au ndio mikwara mbuzi?
 
Ni makosa makubwa kuendelea kuamini kwenye maisha kwamba watu wote unaoweza kufanya nao urafiki wasiwe wasaliti, Eti watu wote ambao unaweza kujenga nao Chama kusiwemo wasaliti!! Huo ni Ujinga mkubwa,

kuondoa usaliti mahali popote, ni meza huru isiyo na vitisho,

Watu Wana chalenji habari za Mungu sembuse Vyama ambavyo watu wake ni wale wenye kutumia akiri na Wakati wowote makosa hujitokeza, unategemea kusitokee usaliti

Na usaliti mwingine husababishwa na mwenye nyumba, pindi anapokosa busara na kuendekeza maamuzi ya mabavu,
 
Back
Top Bottom