Wabunge wangi wa CCM hawajui kujadili na hawawezi kujenga hoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wangi wa CCM hawajui kujadili na hawawezi kujenga hoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Jul 5, 2012.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  1. Bajeti ya serikali ikisomwa bungeni, wabunge wanapaswa kusikiliza kwa makini, kuisoma na kuielewa ili waweze kuchangia/kuijadili vizuri.

  2. Kambi Rasmi ya Ushindani bungeni inatoa bajeti mbadala kwa ile ya serikali kwa kukosowa vipengere ambavyo Kambi imeona serikali imeshindwa kuviona na kuonesha namna gani vinaweza kutekelezwa. Kambi Rasmi ya Ushindani inaweza isikosowe au kupendekeza mambo mapya kama yote yanayotakiwa yako kwenye hotuba ya serikali. Labda tu pale inapohitajika kusisitiza zaidi.

  3. Baada ya haya, majadiliano yanaanza. Huu ni muda, ambao wabunge wanatoa mawazo yao kwa kuonesha ni mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa kwenye bajeti. Yanaweza yakawa yale yaliyoletwa na serikali na yale ya Kambi Rasmi ya Ushindani.

  4. Kujadili maana yake ni kuchangia hoja (kuonesha mazuri na mabaya ya bajeti) na na siyo kumshambulia mtu kwa yale aliyochangia kwani ni mawazo yake na wewe changia ya kwako. Kumshambulia mtu siyo kutoa hoja bali ni kwenda nje ya hoja.

  5. Kama kuna sababu ya kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya maeneo kwenye bajeti, kazi hii inafanywa na mawaziri/manaibu/mwanasheria mkuu wa serikali.

  6. Kwa hiyo, baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa wakikosa mwelekeo kwa kuanza kuwashambulia wabunge wa Kambi Rasmi ya Ushindani kwa mapendekezo yao mbadala. Mbunge anapaswa kuchangia kile tu achoona na kuamini kitajenga taifa letu na kitaondoa kero za wapiga kura wake. Nje ya haya ni kupoteza muda na kutojua nini kichangiwe. Nina hakika wabunge wa CCM wakisoma points hizi na hata wabunge kutoka vyama vingine, itasaidia kuboresha michango ya wabunge. Mbunge siyo msemaji wa serikali – kazi yake ni kuikosoa, kuishauri na kuisimamia serikali iboreshe untendaji na iwajibike vizuri zaidi.
   
 2. m

  muchetz JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Weka paragraphs isomeke kwa urahisi zaidi.
   
 3. kingfish

  kingfish JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni kweli kabisa.nimeshuhudia katika maeneo kadhaa hapa mjini iringa mfano katika kumbi za vyuo na katika baa mahali ambapo tv huwekwa,anapochangia hoja mbunge wa upinzani watu huwa makini kumsikiliza lakini akichangia mbunge wa ccm hakuna anayemzingatia.
   
 4. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mwizi hawezi kujenga hoja ndo maana anaamua kuiba
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Area ya specialization yao ni kuzomea na kutwanga meza kwa nguvu zoote!
   
Loading...