G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,593
- 36,012
Masikini wabunge hawa wa CCM. Bunge lililopita tulikuwa nao wanne tu ambao walikuwa-active nao ni Esta Bulaya, James Lembeli, Luhaga Mpina na Deogratius Haule Filikunjombe R. I. P
Kati ya hao wawili wapo Chadema kwa sasa ambako kabla kulikuwa na jeshi lukuki la wapiganaji e. g Lissu, Mnyika, Msigwa kiufupi ni jeshi kwelikweli na sasa nguvu imeongezeka! Mmoja katangulia mbele ya haki na mmoja sasa yupo serikalini ambae kwa cheo chake hawezi tena kusimamia serikali.
Sasa wabunge hawa wamechoka na kupauka pauuu!! Hawana tena hata mbunge mmoja mfia nchi! Wamechoka hao, wamechoka hao, wamechoka sana! Mbali na kuingiza vijana kama kina Juliana Shonza lakini bado ni zero. Hatutarajii lolote jipya kutoka kwao! Hawaijui falsafa ya mbunge na wala hawako tayari kuijua!
Bunge lililopita kina Bulaya na Filikunjombe walianza mapema kabisa kuungana na kina Tundu Lissu kulipigania taifa. Hawa wa muhula huu ni heri hata wasingekuwepo bungeni maana hamna jipya lolote kutoka kwao.
Mimi najiuliza hasa ni ipi faida yao kule bungeni zaidi ya kula fedha zetu bure?
Hili bunge la CCM muhula huu ambalo lipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ni janga kwa taifa!