Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,917
- 24,674
Nchi imekuwa ya kusadikika kweli, kila siku wanabuni mbinu mpya ya kuwakamua wasiojiweza, wenye uwezo mdogo wa kuendesha maisha yao ili matumbo yao yaneemeke.
Baada ya kubuni mbinu za kuwainua wananchi ili wapate walipa kodi wengi wao ndio wanazidi kuwakamua na kuwatia umaskini
Wawakilishi wetu (wabunge) wamekuwa sio wawakilishi tena bali ni watafutia Tumbo hawajari chochote kuhusu wananchi walio chini yao.
Leo hii baada ya kujadili jinsi ya kushusha mishahara yao, posho na kiinua mgongo chao pale bungeni ili pesa zikasaidie wananchi wa kima cha chini.
Wanaishia kupiga meza na kutaka mishahara yao minono iongezwe, "sio kuongezwa tu iongozwe na tena ilipwe kwa dora"
Hawa watu wana akili kweli? Wanawaza ata vizazi vyao vya tatu vitakavyokuja kutoka wao vitaishije?
Leo hii Vocha "Kiwanda kinachotengeza kinalipa kodi serikarini, mfanyabiashara wa jumla akienda kununua analipa kodi Mwenye duka la reja reja akienda kununua vocha kwa mfanyabishara wa jumla analipa kodi Mwanachi akienda kununua vocha dukani analipa kodi
Hiyo hiyo vocha akiikwangua na kuweka kwenye simu inakatwa kodi".
Bado kuna mtu na PHD yake akaona isiishie hapo kwenye hiyo hiyo vocha ambayo ilishalipiwa kodi kama mara nne punde tu ikimfikia mtu wa mwisho nae akiweka serikari ikishakata chao ile asilimia kadhaa, bado pia itataka imkate kiasi cha shilingi 100--200 cash mwananchi mnyonge ili ikalipe posho, mishahara na kiinua mgongo kwa aliyeleta hiyo dhahama kwa wananchi wa chini.
Nchi ina Rasilimali kibao, ina madini, mafuta, gas, mbuga za wanyama, Ardhi yenye Rutuba, bahari na N.k. Bado Mawazo ya viongozi wetu wenye PHD kama wanavyojinasibu yameganda mgando wakitegemea Rasilimali watu pekee tena wananchi wa hali ya chini kuendesha nchi.
Dubai ina mafuta pekee lakini kila mtu anatamani kwenda kula bata huko
Viongozi wetu waache kutegemea rasilimali watu pekee Wajikite zaidi kwenye kutanua wigo mzuri kwa wawekezaji Waweke sera rafiki,wapunguze masharti na mrundikano mkubwa wa kodi ila wawavutie wawekezaji.
Wakalibishwe ata ikibidi bila masharti na punguzo kubwa la kodi ili tufanye mapinduzi ya viwanda, ili watu ambao ni Rasilimali wajikite kwenye kufanya kazi ili kuinua taifa letu
Kama taifa tunatakiwa kuwa na sera, sheria dhabiti ya uwekezaji isiyohadhiriwa na uongozi uliopo madarakani ili tupate wawekezaji.
Tukiendelea kutegemea Rasilimali watu pekee hatutavuka hatua yeyote kama Taifa, siku zote tutabakia hapa hapa na pengine kuwa chini zaidi ya hapa.
Cc Zero IQ